UTANGULIZI
Sehemu ya maji ni miongoni mwa Sehemu nane zilizopo katika muundo wa Sekretarieti ya Mkoa. Sehemu hii ina Wataalamu wa maji wanaotekeleza shughuli mbalimbali za uendelezaji wa Sekta ya maji Mkoani Kagera. Wataalamu hawa wana jukumu la kumshauri Katibu Tawala Mkoa na Mheshimwa Mkuu wa Mkoa juu ya utekelezaji wa sera na miongozo ya Sekta ya maji ikiwa ni pamoja na kuzishauri na kuzisimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu Sekta ya maji. Sehemu hii inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sera, Sheria, Dira na Mipango ya maendeleo kama yafuatayo:-
Sera ya Taifa ya maji ya mwaka 2002, Sheria ya maji na usafi wa Mazingira Na. 12 ya Mwaka 2009, Sheria ya Utunzaji wa rasilimali za maji Na. 11 ya mwaka 2009, Mpango wa maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals 2030), Dira ya Taifa inayoishia mwaka 2025, Mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka mitano, pia na Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Maji ambao utafika ukomo wake mwaka 2025.
Majukumu ya Msingi ya Sehemu ya Maji (Sekretarieti ya Mkoa)
Jukumu la kwanza kuchambua, kuratibu na kushauri juu ya utekelezaji wa Sera mbalimbali za sekta ya maji Mkoani Kagera. Pili, Kuzijengea uwezo Halmashauri za Wilaya katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya sekta ya maji hasahasa ujenzi wa Miradi ya maji na usafi wa mazingira katika ngazi za vijiji. Tatu, Kuwa kiunganishi muhimu kati ya Serikali kuu (Wizara ya Maji pamoja na TAMISEMI) na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Nne, Kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuandaa mipango inayotekelezeka ya kuendeleza miundombinu ya maji katika ngazi za vijiji na maeneo ya mijini.
Tano, Kufanya ufuatiliaji wa ujenzi wa Miradi ya maji inayotekelezwa katika ngazi zote kuanzia vijijini hadi mijini ili kusudi miradi hiyo itekelezwe kwa ubora na viwango vinavyokubalika. Sita, Kuhakikisha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaainisha, zinafundisha na kusajiri vyombo huru vya watumiaji maji ili miradi ya maji katika ngazi za vijiji iwe endelevu. Saba, Kuhakikisha kuwa Mamlaka za maji katika Mji Mkuu wa Mkoa, Miji Mikuu ya Wilaya na Miji Midogo Mkoani Kagera inatoa huduma ya maji iliyo bora kwa Wananchi wa maeneo hayo Aidha, Kuhakikisha Vyanzo vya maji vinalindwa na vinakuwa endelevu.
Hali ya Huduma ya Maji Katika Mkoa wa Kagera
Tangu mwaka 1961 Mkoa wa Kagera umekuwa ukitekeleza miradi mbalimbali ya maji katika ngazi ya vijiji na miji, ambapo hadi kufikia Mwezi Juni, 2017 hali ya huduma ya maji ni kama ifuatavyo: Hadi mwezi Juni 2017 asilimia 59.3 ya Wananchi waishio vijijini walikuwa wanapata huduma ya maji Safi na Salama. Hata hivyo, miradi ya maji mingi ya vijiji kumi bado inaendelea kutekelezwa, ambapo ikikamilika mnamo mwezi desemba 2017 huduma ya maji kwa Wananchi waishio vijijini itaongezeka hadi kufikia asilimia 72.23 na kufanya jumla ya Wananchi 367,437 kunufaika na miradi hiyo.
Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa Wananchi waishio katika Manispaa ya Bukoba imeongezeka hadi asilimia 86 Mwezi Juni, 2017. Hata hivyo mikakati iliyopo ya kufanya upanuzi wa mradi mkubwa wa maji katika Manispaa ya Bukoba ikikamilika mnamo mwezi Desemba 2017 asilimia 95 ya wakazi wote wa Manispaa ya Bukoba watapata huduma ya maji hivyo kufikia malengo ya Serikali yaliyowekwa kabla ya mwaka 2020.
Aidha, wananchi waishio katika Miji Mikuu ya Wilaya za Mkoa wa Kagera, huduma ya upatikanaji wa maji umeongezeka hadi kufikia asilimia 62 Desemba, 2016. Miradi mingi ya maji inaendeshwa na vyombo huru vya watumiaji maji (COWSOs) katika ngazi ya vijiji, vyombo 84 vilikuwa vimeundwa hadi kufikia Mwezi Desemba 2016 vyenye jumla ya Tsh. 115,957,658.00.
Matanki ya kuvuna maji ya Mvua 1,157 yamejengwa na mafundi sanifu 172 wamefundishwa na kujengewa uwezo jinsi ya kujenga Matanki ya aina mbalimbali ya kuvuna maji ya mvua hadi kufikia mwezi Mei 2016. Aidha, Halmashauri nyingi zipo kwenye mchakato wa kutunga Sheria ndogo zinazohusiana na uvunaji wa maji ya mvua na utunzaji wa vyanzo vya maji.
Jedwali namba 1 hapa chini linaonesha hali ya upatikanaji wa Huduma ya maji mijini na Vijijini kwa kila Wilaya kam aifuatavyo:-
Jedwali namba 1:
Halmashauri
|
Idadi ya vijiji |
Idadi ya watu kwa sensa ya 2012
|
Makadirio ya Wakazi waishio maeneo ya Vijijini, Juni 2017
|
Idadi ya watu wanaopata huduma ya Maji Vijijini hadi kufikia Juni, 2017
|
Asilimia ya watu wanaopata huduma ya Maji Vijijini hadi Juni, 2017
|
Asilimia ya wanaopata maji Maeneo ya Mijini
|
Bukoba DC
|
94 |
289,697 |
322,061 |
199,678 |
62 |
- |
Bukoba MC
|
66 |
128,796 |
143,185 |
89,920 |
84.6 |
86 |
Ngara
|
75 |
320,056 |
355,812 |
214,555 |
60.3 |
76 |
Missenyi
|
77 |
202,632 |
225,270 |
124,800 |
55.4 |
- |
Karagwe
|
77 |
332,020 |
369,112 |
177,174 |
48 |
45 |
Biharamulo
|
80 |
92 |
359,625 |
222,968 |
62 |
62 |
Kyerwa
|
99 |
321,026 |
356,890 |
151,721 |
43 |
- |
Muleba
|
168 |
540,310 |
600,672 |
354,396 |
59 |
65 |
JUMLA
|
736 |
2,134,629 |
2,732,627 |
1,535,212 |
59.3 |
|
Mpango wa Kuongeza Upatikanaji wa Huduma ya Maji Vijijini
Miradi inayoleta Matokeo ya Haraka
Awamu ya kwanza ya mpango huu ilianza mwaka wa fedha 2007/08 ambapo Fedha zake zilitolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa lengo la kutekeleza Miradi midogo midogo inayoleta matokeo ya haraka (Quick wins projects) na kuzijengea uwezo taasisi zinazotekeleza mradi huu ikiwa ni pamoja na ujenzi/ukarabati wa ofisi na ununuzi wa magari. Ambapo, katika mpango huu jumla ya Miradi 527 ilitekelezwa ikiwemo ujenzi wa visima 147, ukarabati wa visima 124, ukarabati wa Miradi ya bomba 36, ujenzi wa Miradi mipya ya bomba 12, uboreshaji wa vyanzo vya maji vya asili 82 na ujenzi wa matanki 17 ya kuvuna maji ya mvua. Ambapo jumla ya shilingi 3,410,619,635/- zilitumika na kunufaisha Wananchi wapatao 451,877.
Utekelezaji wa Miradi ya maji katika vijiji kumi
Utekelezaji wa miradi ya maji kwenye vijiji kumi kwa kila Halmashauri ya Wilaya Mkoani Kagera umefikia katika hatua mbalimbali, ambapo hadi mwezi Juni 2017 jumla ya miradi 34 kati ya 63 inayotekelezwa ilikuwa imekamilika na kutoa huduma ya maji kwa Wananchi wapatao 205,202 kwenye vituo vya kuchotea maji vipatavyo 514. Hata hivyo miradi 29 ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake kama ifuatavyo:
Jedwali Na 2: Vijiji vilivyopewa kipaumbele na Halmashauri katika kutekeleza
Halmashauri
|
Vijiji vilivyopendekezwa
|
BUKOBA MC
|
Ijuganyondo, Kagondo, Ihyoro, Kyamyosi, Bushaga, Rwazi, Bulibata na Bunkango
|
BUKOBA DC
|
Ibwera, Bituntu, Kibirizi, Katale, Lukindo, Kibona, Kyamulaile, Kitahya, Itongo na Mashule
|
MULEBA DC
|
Kangaza, katoke, Karutanga, Kishoju, katembe, Kyota, Kabare, Kinagi na Iroba
|
BIHARAMULO DC
|
Bisibo, Nyakanazi, Katoke,Mabare/Mihongora,Nyabusozi, Kasozibakaya, Nyantakara, Kasato, Kagondo na Mubaba
|
NGARA DC
|
Muruvyagila, Muhweza/ murugalama, Kanazi/Kabalenzi, Mbuba, Mukubu, Rulenge, Ngundusi, Rwinyana na Munjebwe
|
KARAGWE ** DC
|
Chamchuzi, Chabuhora, Kayungu, Nyakakika, Chaanika na Nyaishozi
|
KYERWA DC**
|
Kigorogoro, Iteera, Rwabikagati na Kibingo
|
MISENYI DC
|
Ruzinga, Igurugati, Kakunyu, Bugango, Kenyana, Kilimilile na Rukurungo
|
Jedwali Na. 3 Hali Utekelezaji kwa kila Halmashauri
Halmashauri za Wilaya
|
Jumla ya miradi
|
Miradi iliyokamilika
|
Miradi ambayo haijakamilika
|
BUKOBA MC
|
8 |
7 |
Bushaga (98%)
|
BUKOBA DC
|
10 |
4 |
Ibwera 75%, Bituntu 80%, Kibirizi 85%, Katale 90%, Lukindo 80%, Kibona 95%
|
MULEBA DC
|
9 |
5 |
Kangaza 98%, Katoke 95%, Karutanga 80%, Katembe 98%
|
BIHARAMULO DC
|
9 |
6 |
Bisibo 90%, Nyakanazi 92%, Katoke 90%
|
NGARA DC
|
10 |
5 |
Muruvyagila 60%, Muhweza/ Murugalama 65%, Kanazi/Kabalenzi 75%, Mbuba 50%, Mukubu 60%
|
KARAGWE ** DC
|
6 |
2 |
Chamchuzi 85%, Chabuhora 70%, Kayungu 90%, Nyakakika 65%
|
KYERWA DC**
|
4 |
2 |
Kigorogoro 90%, Iteera 98%
|
MISENYI DC
|
7 |
3 |
Ruzinga 70%, Igurugati 79%, Kakunyu 75%, Bugango 80%
|
JUMLA
|
63 |
34 |
54% |
Ujenzi wa Miradi Mingine ya Maji Vijijini
Halmashauri za Wilaya Mkoani Kagera zinatekeleza miradi mbalimbali nje ya vijiji kumi. Miradi hii inahusisha miradi ya maji kwenye vijiji vya nyongeza yaani Quick win projects pamoja na miradi inayofadhiliwa na wadau wengine wa maendeleo. Taarifa ya miradi hii imeoneshwa kwenye jedwali namba 4 na namba 5 hapa chini
Jedwali Na 4: Miradi ya maji ya Quickwin
H/wilaya
|
Mradi
|
Utekelezaji
|
Muleba
|
Ruhanga
|
Mradi umetekelezwa na kukamilika, Aidha Wananchi wanapata huduma ya maji
|
Kamachumu
|
Mradi umetekelezwa na kukamilika na Wananchi wanapata huduma ya maji
|
|
Ilogelo
|
Utekelezaji umefikia asilimia 95
|
|
Izigo/Itoju na Kabare
|
Utekelezaji umefikia asilimia 15
|
|
Karagwe
|
Chonyonyo
|
Ujenzi wa Mradi (Visima 2,ujenzi wa mradi wa kutumia nguvu za jua) umefikia 50%.
|
Omukakajinja
|
Mradi (Visima 3 na pampu za mkono) visima vimechimbwa na vinatoa huduma ya maji.
|
|
Missenyi
|
Nyabihanga
|
Uchimbaji wa visima vifupi na vya kati 20 umekamilika na Wananchi wanapata huduma ya maji
|
Jedwali Na 5: Miradi ya maji inayofadhiliwa na Wadau wengine
Jina la Mradi
|
Mdau wa maendeleo
|
Gharama
|
Malengo
|
% Utekelezaji
|
Mutukula (Misenyi DC)
|
UN-HABITAT/MOWI |
830,000,000
|
-Kuhudumia watu 7,231
-Kuchimba visima 2, kulaza mtandao wa mabomba wenye urefu wa km 8.9, kujenga vituo 15 vya kuchotea maji, kujenga tankilenye ujazo wa 120m3, kupeleka umeme kwenye chanzo, kujenga mtambo wa kutibu maji pamoja na kunua na kufunga mashine za kusukuma maji |
100 |
Rusumo (Ngara DC)
|
TAN-ROADS (Makao Makuu)
|
249,869,900.00
|
-Kuhudumia watu 2,021
-Kujenga chanzo, DP6 na tenki 1 (40m3), - Kununua na kulaza mabomba yenye urefu wa km 11 |
100 |
Fedha za Utekelezaji wa Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira
Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi ya maji kwenye vijiji kumi na ile inayotekelezwa kwenye vijiji vya nyongeza yaani QUICK WIN projects. Hali ya utoaji wa fedha na matumizi yake kwa kila Halmashauri ni kama ilivyooneshwa kwenye Jedwali namba 6 hapa chini:-
Jedwali namba 6: Mapokezi na Matumizi ya fedha za WSDP kwa kila Halmashauri ya Wilaya Mkoani Kagera
Jina la Halmashauri
|
Gharama ya Mikataba ya miradi ya Maji
|
Kiasi kilichopokelewa na Kulipwa hadi desemba 2016
|
Deni
|
Bukoba MC
|
2,422,641,190 |
2,422,641,190 |
- |
Bukoba DC
|
5,340,127,640 |
3,309,788,517 |
2,030,339,123 |
Muleba
|
6,247,849,420 |
4,628,859,420 |
1,618,990,000 |
Biharamulo
|
5,347,882,933 |
3,676,854,174 |
1,671,028,759 |
Ngara
|
4,360,798,980 |
2,379,688,980 |
1,981,110,000 |
Karagwe
|
8,146,928,854 |
3,571,688,980 |
4,575,099,000 |
Kyerwa
|
3,555,315,889 |
2,918,122,589 |
637,193,300 |
Missenyi
|
4,122,758,968 |
2,442,873,964 |
1,679,885,004 |
Jumla
|
39,544,303,873 |
25,350,517,814 |
14,193,645,186 |
Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Maji Awamu ya Pili.
Kuanzia Mwezi Julai mwaka 2016 Serikali imeanza kutekeleza awamu ya pili ya Programu ya maji itakayotekelezwa kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2019/20 Awamu hii imelenga kufanya yafuatayo Mkoani Kagera.
Kwanza ni kumalizia utekelezaji wa miradi 29 ya maji katika vijiji kumi na kukamilisha ujenzi wa miradi 3 ya Quickwin, Miradi hii ipo katika hatua mbalimbali ya utekelezji wake. Pili, Kujenga na kukarabati Miradi mipya 83 katika Halmashauri za Wilaya Mkoani Kagera. Miradi hii itagahrimu kiasi cha shilingi 47.3 bilioni na itatekelezwa hadi mwaka 2020. Tatu, Kuendeleza Kampeini ya Kitaifa ya usafi wa Mazingira. Nne, Kukamilisha usanifu na kuanza ujenzi wa miradi ya maji katika makao makuu ya Wilaya za Missenyi, Karagwe, Ngara, Biharamulo, Kyerwa na Muleba kwa lengo la kuboresha huduma ya maji katika miji hiyo, ikiwa ni pamoja na kuanzisha Bodi ya maji katika mji wa Kyaka/Bunazi
Tano, Kufanya usanifu na ujenzi wa mradi mkubwa wa maji utakaohudumua kata 15 kwenye vijiji 57 Wilayani Kyerwa. Mradi huu ukikamilika utahudumia jumla ya Wananchi 132,000 hivyo kumaliza kabisa tatizo la maji katika Wilaya hiyo. Sita, Kukamilisha usanifu wa mradi Mkubwa wa kutoa maji katika ziwa Rwakajunju kwa ajili ya miji ya Kayanga/Omurushaka pamoja na vijiji 30 Katika Wilaya ya Karagwe. Saba, Kuanza utekelezaji wa mradi wa kuondoa na kutibu maji taka katika Manispaa ya Bukoba. Mradi huu utafadhiliwa na Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo la AFD. Aidha, Kuendelea kuimarisha vyombo huru vya watumiaji maji (COWSOs) ili viweze kuendesha miradi ya maji katika ngazi za vijiji, pia Kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa sekta ya maji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa