• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Ng'ombe wa Wafugaji Waliokuwa Mapori ya Akiba Wakiwa Wamezuiliwa Katika Mojawapo ya Kambi

Imewekwa : September 14th, 2017

Taarifa ya Mkuu wa Mkoa Kagera Kwa Vyombo vya Habari Kuhusu Serikali Kuwapatia Wafugaji Malisho Eneo la Mwisa II

Ndugu Waandishi wa Habari,   Nimewaiteni hapa ili kutoa maagizo na Maamuzi ya Serikali juu ya ubainishaji na uendelezaji wa nyanda za malisho katika eneo la Mwisa II katika Wilaya za Muleba na Karagwe. Uendelezaji wa eneo la Mwisa II kwa ajili ya ufugaji ni mpango ulioanza miaka ya nyuma na ulianza kwa mradi wa kuzuia ndorobo  ulioendeshwa  na Wizara yenye dhamana ya Mifugo kwa wakati huo kwa lengo la kuufanya uwanda wa Mwisa II kuwa na ufugaji wenye tija na endelevu. Eneo la Mwisa II ni eneo linaloanzia katika mipaka ya Ranchi ya Kagoma, kupitia Bonde la Ziwa Burigi hadi Pori la Akiba la Burigi.

 Ndugu Waandishi wa Habari, Lengo la uendelezaji wa eneo la Mwisa II ni kuviendeleza vijiji vinavyogusa eneo la Mwisa II na kuongeza kipato kwa kupunguza umasikini kwa wananchi katika ngazi za Vijiji, Halmashauri husika, Mkoa na Taifa kwa ujumla. Mpango huu ni fursa kwa Mkoa wa Kagera kujikwamua kiuchumi na kutoka nafasi unaoshika kwa sasa ambayo ni ya tatu toka chini kwa kipato Kitaifa.

Mpango huu utaondoa ufugaji holela na ukataji wa miti ovyo na kuwezesha uzalishaji mifugo kisasa na kibiashara bila kuharibu mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Pia, mpango huu unatarajiwa kuwezesha upatikanaji wa maeneo ya malisho kwa ajili ya wafugaji wa Kitanzania walioondolewa kwenye Misitu ya Hifadhi na Mapori ya Akiba na hivyo kutatua migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Ndugu Waandishi wa Habari, Mpango huu wa uendelezaji wa Mwisa II ni utekelezaji wa Maagizo na Maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Serikali ikiwa ni pamoja na Mheshimiwa Rais wakati wa ziara yake Mkoani Kagera mwezi Julai, 2017 ambaye alisisitiza hifadhi endelevu ya Misitu ya Hifadhi na Mapori ya Akiba na wananchi kupunguza mifugo yao na kufuga kisasa na kibiashara kufuatana na ardhi waliyonayo.

Aidha, utekelezaji wa mpango huu unaenda sambamba na Maagizo yaliyotolewa na Mheshimiwa Makamu wa Rais mwaka 2016 kwa Mikoa kutenga maeneo ya wafugaji pindi agizo litakapotolewa la kuondoa mifugo toka kwenye maeneo ya Hifadhi ambapo Mkoa uliainisha eneo la Mwisa II kuwa ni nyanda za malisho. Aidha, Mwezi Juni 2017, Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokutana na Maafisa Mifugo wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Mkoanii Dodoma aliagiza maeneo ya wafugaji yatengwe, yapimwe na yamilikishwe kwa wafugaji.

 Ndugu Waandishi wa Habari, Mpango huu wa uendelezaji wa Mwisa II utawezesha upatikanaji endelevu wa mali ghafi za viwanda vya nyama, maziwa na bidhaa zake, ngozi na bidhaa zake na kadhalika. Pia mpango huu ni utekelezaji wa Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya uwekezaji wa viwanda ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kuongeza ajira kwa Watanzania.

Ndugu Waandishi wa Habari, (angalizo) Ili kutekeleza azima ya uendelezaji wa eneo la Mwisa II hatua mbalimbali zitatekelezwa bila kuathiri mipaka ya Vijiji, kunyang‘anya ardhi ya Vijiji au kuathiri miradi iliyopo ikiwa ni pamoja na mradi wa umwagiliaji wa IKAKI unaogusa vijiji vya Itunzi, Kashalala na Kiteme. Hatua hizo ni kama zilivyoainishwa hapa chini:-

Ndugu Waandishi wa Habari, Hatua ambazo tayari zimechukuliwa au zitakazochukuliwa ni kama ifuatavyo: Kwanza Timu ya Wataalam ngazi ya Wizara, Mkoa, na Halmashauri husika tayari imekutana na wajumbe wa Halmashauri za Vijiji na Madiwani kwa ajili ya kuwaelimisha juu ya zoezi la ubainishaji wa eneo la Mwisa II katika maeneo yao na elimu inaendelea kutolewa.  Pili, Wataalamu kwa kushirikiana na Watendaji wa Vijiji na viongozi wa Vijiji wanaendelea  kubaini  eneo la Mwisa II na kuliwekea alama kwenye mipaka ya nje.

Tatu, Baada ya Timu kukamilisha hatua mbili za mwanzo eneo la Mwisa II litagawiwa katika Vitalu kwa kuweka alama kulingana na jiografia ya eneo husika, upatikanaji wa nyanda za malisho, maeneo ya maji, maeneo ya makazi, huduma za kijamii na miundombinu mbalimbali inayopatikana katika eneo hilo.

Ndugu Waandishi wa Habari, Hatua ya Nne itakuwa ni kukamilisha kazi ya Upimaji kwa kutumia (GPS set). Tano, ni kusajili vitalu na kuvipa namba za usajili utakaofanywa  na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Hatua ya Sita na ya mwisho itakuwa ni ushirikishwaji kuanzia ngazi za Vijiji, Wilaya na Mkoa kwa kuwatambua wananchi watakaopendekezwa kumilikishwa vitalu aidha, kipaumbele kitakuwa kwa Wanavijiji watakaojiunga katika ushirika wa wafugaji.

Ndugu Waandishi wa Habari, (Maagizo) Ili kufanikisha mpango huu ambao upo kwa ajili ya faida ya wananchi, Vijiji husika, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla naagiza yafuatayo yatekelezwe;

Moja, Viongozi, Watendaji na Wataalam wa ngazi zote washirikiane wakiwa na msimamo na Dira moja.

Pili, Waheshimiwa Mawaziri wa Sekta zinazohusika naomba watoe ushirikiano na uwezeshaji unaohitajika ikiwemo Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Kagera, na Wawakilishi wengine wa Wananchi.

Ndugu Waandishi wa Habari, Mwisho napenda kuwakumbusha wananchi wote kuwa ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwajibika ipasavyo katika kulinda, kuhifadhi na kutunza maliasili za misitu, Mapori ya Akiba, Maeneo ya Hifadhi na vyanzo vya maji ili kuepusha Mkoa wetu kugeuka jangwa na kuendeleza ufugaji wenye Tija na Kibiashara.

 

Imetolewa na;     Mhe. Meja Jenerali (Mst) Salum M. Kijuu

                             Mkuu wa Mkoa

                             KAGERA

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa