• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Profesa Kamuzora Ashauri Seminari ya Katoke Kuanzisha Masomo ya Programu za Talakilishi Ili Kuendana na Dunia ya Sayansi na Teknolojia

Imewekwa : May 20th, 2019

Wahitimu Kidato cha Sita 24 Sita Tu Kuendelea na Wito wa Upadre 

Profesa Faustin Kamuzora Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera aushauri uongozi wa Seminari ya Mtakatifu Karoli Lwanga Katoke alikosoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kuanzisha maabara ya Talakilishi (Computer Labaratory) na kutoa elimu juu ya ubunifu na uanzishwaji wa programu (software) mbalimbali badala  ya kujikita kwenye matumizi  ya talakilishi tu (yaani namna ya kutumia Computa tu).

Profesa Kamuzora alitoa ushauri huo katika maafali ya 29 ya kidato cha sita katika Seminari ya Katoke Wilayani Biharamulo alipokuwa mgeni rasmi Mei 18, 2019 ambapo alisistiza kuwa Seminari hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwa taifa la Tanzania ni lazima iendane na ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia mfano kuanzisha program za  wa watu kuweka ulinzi majumbani mwao kwa kutumia simu au kuwasha na kuzima umeme ukiwa mbali na nyumbani.

Katika mahafali hayo Profesa Kamuzora aliwaasa wahitimu 24 wa kidato cha sita pamoja na wananfunzi wanaobaki kuchapa kazi kwa bidii sana kuheshimu misingi ya maadili waliyofundishwa na walimu wao ili kuyafikia mafanikio kama wanafunzi waliotangulia katika Seminari hiyo walivyopata mafanikio katika sehemu mbalimbali ndani na je ya nchi.

“Naomba kujitolea mfano mimi mwenyewe ambaye nilipita katika Seminari hii ya Katoke mwaka 1977 hadi 1980 kwa kufuata malezi na maadili ya Seminari hii nimeweza kusoma hadi ngazi za juu sana na kuwa Profesa  na nimefanya kazi sehemu mbalimbali lakini siri kubwa ni malezi na maadili niliyoyapata hapa. Pia Mhe. Rais Magufuli alipita hapa sasa unaweza kuona namna ya utendaji kazi wake ni kutokana na alichokipata hapa.” Alitoa ushuhuda Profesa Kamuzora.

Katika mahubiri yake wakati wa ibada takatifu ya kuwapongeza wanafunzi 24 wahitimu wa kidato cha sita Padre Fortunatus Bijura alisema kuwa ibada hiyo iliadhimishwa ikiwa ni ibada ya Mtakatifu Joseph mchapakazi ili kuwakumbusha vijana hao 24 pamoja na wanafunzi wengine wanaosoma katika Seminari hiyo kuwa kuchapa kazi ndiyo msingi wa mafanikio ya kila kitu katika maisha ya mwanadamu.

Padre Bijura pia aliwapongeza na kuwakumbusha wahitimu wa kidato cha sita katika ibada hiyo kuwa Mungu hujua wito wa kila mtu kabla hajazaliwa na kumaliza kidato cha sita ndiyo mwanzo wa wito wa upadre kwani baada ya hapo kuna miaka minane au tisa mpaka mtu awe padre. Wanafunzi walitakiwa kuchapa kazi kwa bidii hasa katika masomo yao na kuzingatia misingi ya maadili waliofunzwa katika Seminari hiyo.

“Maisha si starehe tu, sisi Watanzania bado tupo nyuma sana katika kuchapa kazi nitatoa mfano kwa wenzetu Wajerumani na Wamarekani hawa wanachapa sana kazi, wanakula sana na wanakunywa bia sana lakini wanaheshimu sana muda wao wa kupumzika. Lakini hapa Tanzania utawasikia vijana wakisema hebu twende kijiweni kupoteza muda kidogo, sijui muda huo wanautoa wapi.” Alisisitiza Padre Bijura ambaye ni mwalimu wa somo la Kiingereza Katika Seminari ya Katoke.

Padre Bijura alimalizia mahubiri yake kwa kuwaasa vijana 24 wahitimu wa kidato cha sita kwa kuwataka kuwa mfano bora wa kuchapa kazi na wale ambao walichagua kutoendelea na wito wa upadre kuwa mabalozi wema uraiani kwa kuchapa kazi, pia wakitunza muda wao vizuri na kutokuchagua kazi bali kuthamini na kuipenda kazi (Sense of Belonging)  lakini kazi hiyo isiwafanye wakamsahau Mungu.

Kwa upande mwingine Padre Jovine Bampabula ambaye ni Padre mlezi wa wanafunzi wa Seminari ya Katoke lakini pia alisoma katika Seminari hiyo kuanzia mwaka 1975 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akihojiwa juu ya Seminari hiyo kuzalisha viongozi bora alisema kuwa ni kutokana na malezi na maadili yanatolewa katika Seminari hiyo ya Katoke.

Seminari hii inazalisha Mapadre na wataalam wengine ambao huja kuwa watu wakubwa katika fani mbalimbali kwenye taifa letu na nje ya nchi. Mfano mimi nilisoma na Rais Magufuli tangu mwaka 1975 hapa mimi nilipata upadre yeye sasa ni Rais wa nchi, watu wengi wanashangaa ujasiri  wa kutoa maamuzi na kupambana na Mafisadi lakini mimi sishangai kwani najua kuwa ujasiri ule ni kutokana na maadili na malezi bora aliyoyapata kutoka katika Seminari yetu hii ya Katoke.

Wafanyakazi katika shamba la Bwana ni wengi lakini Wateule ni wachache; Wanafunzi waliohitimu kidato cha Sita Seminari ya Katoke mwaka 2019 jumla ni 24 lakini walianza kidato cha tano wakiwa 27 katika mahafali yao ya kuhitimu Mkuu wa Seminari hiyo Padre Datius Rwegoshora alisema kuwa wanafunzi ambao walikuwa tayari wamejitafakari na kuamua kuendelea na wito wa upadre kati ya 24 ni sita tu ambao walipewa barua kuendelea na wito na kuitwa Mafrateli kuanzia siku hiyo.

Tuwaombee vijana hawa ili waifikie ndoto yao ya kuwa wachungaji wa Kondoo wa Bwana na kuhudumu katika shamba la Bwana. Seminari ya Mtakatifu Karoli Lwanga Katoke ilianzishwa mwaka 1964 Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera ikiwa chini ya Jimbo Katoriki la Rurenge.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa