• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba Akiwa Mkoani Kagera Kutatua Kero za Ununuzi wa Kahawa ya Wakulima

Imewekwa : April 27th, 2018

Serikali Yasisitiza Mfumo Mpya Kutumika Vyama Vya Ushirika Haviruhusiwi Kununua Kahawa ya Mkulima Bali Kukusanya Tu – Waziri Tizeba

Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba atatua changamoto kubwa sita za mfumo mpya wa ununuzi wa zao la kahawa Mkoani Kagera uliopendekezwa na Serikali utumike msimu wa mwaka huu 2018 ili mkulima aweze kunufaika na zao la kahawa kupitia Vyama vya  Ushirika na siyo Vyama hivyo kumnyonya mkulima.

Akiwa Mkoani Kagera kwa ziara ya siku moja katika kikao cha wadau wa zao la Kahawa kilichofanyika Aprili 26, 2018  Dkt. Tizeba alisema amekuja kutatua changamoto sita ambazo zimeanza kujitokeza mara baada ya Serikali kutangaza mfumo mpya utakaotumika kununua kahawa ya wakulima ili waweze kunufaika na zao hilo.

Akiongea na Wadau hao Dkt. Tizeba alisema kuwa kwanza ieleweke kwa kila mwananchi hasa wakulima  wa kahawa kuwa Vyama vya Ushirika KCU 1990 LTD, KDCU LTD na NGARA FARMERS haviruhusiwi kununua kahawa za wakulima bali jukumu lake ni kukusanya kahawa za wakulima na kuzipeleka kwenye mnada kuziuza kahawa hizo  kwa bei ya soko la dunia  na wakulima watalipwa fedha zao kwa bei ya soko la dunia.

“Haiwezekani Vyama vya Ushirika ambavyo vinaundwa na wakulima wenyewe viwe tena wanunuzi wa kahawa na kuwanyonya wakulima, jukumu lao ni kukusanya kahawa za wakulima na kuzipeleka katika mnada zikauzwe kwa bei ya soko la Dunia. Kwa kuwa Kagera mlizoea kulipwa fedha za awali Serikali inasimamia kwa karibu ili Vyama vya Ushirika vipate fedha za kuwalipa wakulima malipo ya awali ambayo yatakuwa madogo  kama asilimia 20 tu ili baada ya kahawa kununuliwa mkulima apate kiasi kikubwa cha malipo.,” Alifafanua Waziri Dkt. Tizeba.

Pia alifafanua kuwa mkulima atasubiri fedha yake ya malipo ya pili kwa muda usiozidi wiki mbili na kikomo cha muda huo ni mwezi mmoja tu na si vinginevyo.

Changamoto Kubwa Sita Alizozitatua Dkt. Tizeba Kuhusu Mfumo Mpya Utakaotumika Kununua Kahawa ya Wakulima Msimu wa Mwaka Huu 2018.

Kwanza; Vyama vya Ushirika Mkoani Kagera namna ya kupata fedha ya kukusanyia Kahawa za Wakulima na kuzipeleka mnadani kwenye soko la dunia. Waziri  akijibu changamoto hiyo Dkt. Tizeba alisema kuwa tayari Serikali inavisimamia vyama vya KCU 1990 LTD, KDCU LTD na NGARA FARMERS kupata fedha kwa ajili ya malipo ya awali ya wakulima na mwanzoni mwa Mwezi Mei  2018 Vyama vyote vitakuwa na fedha ya kutosha kukusanyia kahawa ya wakulima.

Pili; Namna gani viwanda vyote vya binafsi na vya Vyama vya Ushirika vitakoboa kahawa. Katika Kikao hicho cha wadau iliamuliwa kuwa Vyama vya Ushirika vilivyoruhusiwa kukusanya kahawa ya wakulima vitoe tenda katika viwanda vilivyopo maeneo husika vikoboe kahawa ili kuiwahisha mnadani. Aidha, viwanda vitavyotumika kukoboa kahawa hiyo ni vile ambavyo vina viwango na si vile vinavyokata kahawa na mwisho kuonekana haina ubora.

Tatu; Dhana ya Vyama vya Ushirika kununua kahawa ya Wakulima. Pamoja na Waziri Dkt. Tizeba kulitolea ufafanuzi jambo hilo lakini pia Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bw. Tito Haule alitoa ufafanuzi kuwa Vyama vya Ushirika havitakiwi kufanya biashara kwa wananchama wake bali jukumu lake ni kukusanya kahawa kwa wakulima na kuzipeleka mnadani katika soko la dunia ili mkulima apate bei iliyo nzuri.

Nne; Bei elekezi iliyotangazwa na Chama Kikuu cha Ushirika Kagera Co operative Union 1990 LTD (KDCU 1990 LTD) katika mkutano wake Mkuu kwa wakulima. Waziri Dkt. Tizeba alifafanua kuwa chama hicho hakikutakiwa kutangaza bei elekezi kwasababu hakitanunua kahawa ya wakulima bali jukumu lake ni kukusanya kahawa ya wakulima. Aidha, wakulima watalipwa fedha ya awali ambayo itakuwa kidogo ili mara baada ya kahawa kupata bei halisi mkulima alipwe fedha nyingi na kumnufaisha.

Tano; Namna bora ya kudhibiti utorashaji wa kahawa maarufu  ‘Obutura’. Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo alikikumbusha kikao kuwa Mkuu wa Mkoa tayari alishatoa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya kuhakikisha hakuna kahawa inauzwa kwa njia za Magendo au Obutura.

Agizo, Katika hatua nyingine mara baada ya kusikiliza malalamiko ya wadau kutoka Wilaya ya Karagwe kuhusu baadhi ya vyama ambavyo vilisajiliwa na vinavyoendesha ununuzi wa kahawa holela Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba alimuagiza Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Tanzania kuvifutia usajili vyama hivyo mara moja tangu tarehe 26.04.2018 Vyama hivyo ni Nguvumali, Nkwenda Amcoss na Mavuno na kuagiza kuwa viache mara moja kujishughulisha na masuala ya kununua kahawa.

Sita; Gharama za uendedeshaji wa Vyama vya Ushirika Mkoani Kagera. Katika Mkoa wa Kagera wakulima walikuwa hawapati malipo ya pili takribani miaka mitano iliyopita kutokana na Vyama vya Ushirika kuwa na gharama kubwa za uendeshaji jambo ambalo lilipelekea Serikali kuanzisha mfumo mpya wa Vyama hivyo kukusanya kahawa za wakuli na si kununua kwasababu fedha ya wakulima ilikuwa inaenda kwenye gharama za uedeshaji wa Vyama.

Katika kulishughulikia suala hilo Dkt. Tizeba alimagiza Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Tanzania kuhakikisha analeta mara moja wataalamu wa hesabu kuzikagua gharama za uendeshaji wa Vyama hivyo na kuhakikisha zinakuwa gharama halisi na ndogo ili zisimuumize mkulima kwa kukatwa fedha yake ili msimu ukianza kila kitu kiwe katika mpangilio mzuri.

Katika hatua nyingine Waziri wa Kilimo Dkt. Tizeba alikitembelea kiwanda cha Kahawa cha AMIAMZA kilichopo Kibuye Manispaa ya Bukoba  na kuongea na mmiliki wa Kiwanda hicho Bw. Amir Amza ambaye alimuomba Waziri Dkt. Tizeba kuona uwezekano wa kuondoa Ushuru wa Halmashauri (Cess)  ili kahawa ya kiwanda hicho iweze kushindana katika soko la dunia.

Akilitolea ufafanuzi  suala hilo Waziri alisema kuwa Serikali inaishi kwa kutegemea kodi kujenga miundombinu kama barabara kwahiyo kodi hizo haziwezi kufutwa isipokuwa Serikali ilipunguza kiwango cha cha Kodi hiyo ya Halmashauri kutoka asilimia 5 hadi asilimia 3.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa