- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ukijani wa Mkoa wa Kagera Sasa Waelekezwa Katika Matunda Kuboresha Afya za Wananchi na Kulisha Viwanda
Mkoa wa Kagera waadhimisha kilele cha wiki ya upandaji miti Wilayani Karagwe kwa kupanda miche zaidi ya 600 ya miti ya matunda aina mbalimbali ili kuboresha afya za wananchi wa Kagera na kuondokana na matatizo ya utapiamlo na udumavu hasa watoto wadogo.
Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka alisema katika hotuba yake kuwa wananchi wa mkoa wa Kagaera wana tatizo la kutokula matunda wakati kilimo cha matunda kinakubali katika ardhi ya Kagera.
Mkuu wa Mkoa alisistiza juu ya Kampeini yak e aliyoizindua mwezi Janauari 26, 2018 ya kupanda miti ya matunda kwa wingi ili kuhamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kula matunda mara kwa mara ili kumaliza tatizo la udumavu pamoja na utapiamlo magonjwa yanayosababishwa na kutokula matunda kwa wingi.
Mkuu wa Mkoa Kijuu alisisitiza tena kila kaya kuhakikisha inapanda angalau miche mitano ya matunda kuzunguka katika nyumba yao na Halmashauri za Wilaya kuhakikisha zinaanzisha vitalu vya matunda ili kurahisisha upatikanaji wa miche hiyo ya matunda kwa wananchi.
Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa inasema “Tanzania ya Kijani Inawezekana, Panda Miti kwa Manufaa ya Viwanda” katika kufanikisha kaulimbiu hiyo mkoa wa Kagera umekuwa ukipanda miti kwa wingi ili kulinda mazingira na mwaka wa fedha 2016/17 ulifanikiwa kupanda jumla ya miti milioni 14 na miti milioni 12 ilifanikiwa kuota na kukua.
Aidha kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 mkoa chini ya kampeini ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera unaendelea kuhamasisha wananchi kupanda zaidi miti ya matunda kuliko miti ya mbao ili kuboresha afya ambapo kila Halmashauri imeagizwa kupanda miti hasa ya matunda na kufikia lengo la miche milioni moja na nusu.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Kayanga Mkuu wa Wilaya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Kagera alijumuika na wananchi, wanafunzi pamoja na walimu na wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kupanda miche ya miti ya matunda katika viwanja vya Shule hiyo na maeneo yanayozunguka Shule ya Msingi Kayanga.
Bw. Isaya Tendega Kaimu Katibu Tawala Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji kwaniaba ya Katibu Tawala wa Mkoa aliwasisitiza walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi kayangia kuitunza miche hiyo ya matunda ili ikue ili wanafunzi na walimu waweze kunufaika na matunda yatakayopatikana kutokana na miti hiyo.
Katika hatua nyingine Bw. Tendega aliwashukuru wadau mbalimbali katika Mkoa wa Kagera wanaounga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira kwa kutoa miche ya matunda na miti katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera . Wadau hao ni pamoja na Tanzania Agricultural Modernization Association, Kanisa Katoliki, Vi Agroforestry, KKKT Dayosisi ya Karagwe na wengineo.
Mwaka huu maadhimisho ya wiki ya upandaji miti kitaifa ilifanyika Mkoani Shinyanga Wilayani Kishapu na Mkoa wa Kagera uliadhimisha kilele hicho Wilayani Karagwe na huadhimishwa kila mwaka Aprili Mosi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa