• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Historia

HISTORIA YA MKOA WA KAGERA




CHIMBUKO AU ASILI YA MKOA WA KAGERA

Kabla ya Uhuru na hadi kufikia mwaka 1961, eneo la sasa la Mkoa wa Kagera, lilikuwa ni moja ya maeneo yaliyounda Jimbo lililoitwa “Lake Province”. Jimbo hili lilijumuisha Wilaya za Bukoba, Musoma, Shinyanga na Tabora. Baada ya uhuru mwaka 1962 mkoa ulibadilishwa jina na kuitwa ‘West Lake Region’ (Ziwa Magharibi) na kujumuisha Wilaya 4 za Ngara, Biharamuro, Karagwe na Bukoba. Jina hili (Ziwa Magharibi) lilidumu katika kipindi cha ukoloni na baada ya uhuru mwaka 1961 mpaka mwaka 1979 baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda (Vita ya Kagera).

Mkoa ulipata jina la Kagera kutokana na Mto Kagera zamani ukijulikana kama “Akagera” ambao hutiririsha maji yake kutoka Rwanda kupitia Kaskazini na kumwaga maji yake katika ziwa Victoria

UKUBWA WA MKOA NA MAHALI ULIPO

Mkoa wa Kagera unapatikana Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Tanzania. Makao Makuu ya Mkoa yapo katika mji wa Bukoba umbali wa kilometa 1500 kutoka Dar es Salaam, Mkoa huu unapakana na nchi ya Uganda kwa Kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa Magharibi,Mikoa ya Geita na Kigoma,  kwa upande wa Kusini. Pia Mkoa wa Kagera unapakana na  Ziwa Victoria kwa upande wa Mashariki ambapo kwa ndani ya Ziwa hilo mkoa unapakana na Mikoa ya Geita, Mwanza na Mara. Vile vile Mkoa wa Kagera uko Kusini mwa Ikweta kati ya Latitude 1 “00” na 2”45”. Mashariki mwa ‘Greenwich' katika Longitudi 30”25” na 32”40”

Mkoa wa Kagera una jumla ya eneo la Kilomita za mraba 35,686 kati ya hizo Kilomita za Mraba 25,513 ni eneo la nchi kavu ambalo ni sawa na asilimia 73 ya eneo lote la Mkoa na kilomita za mraba 10,173 ni eneo la maji sawa na asilimia 27. Mkoa una visiwa vikubwa katika Ziwa Victoria ambavyo ni Bumbire, Iroba, Kelebe, Goziba, Ikuuza na Mhutwe na visiwa vingine vidogo jumla vikiwa 27 vinavyokaliwa na watu na jumla ya visiwa 21 vidogo vidogo visivyokaliwa na watu.  Ukiacha mbali Wilaya ya Biharamulo ambayo ni tambarare, sehemu kubwa ya mkoa ni yenye milima na vilima vilivyogawanywa na mabonde yenye matingatinga. Upande wa magharibi wa mkoa mito mingi inamwaga maji yale katika Mto Kagera ambao nao humwaga maji yake katika Ziwa Victoria. 

Mwinuko wa nchi (altitude) ni kati ya mita 1,100 na 1,800 juu ya usawa wa Bahari. Mchanganuo wa kilomita za mraba kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo: - Halmashauri ya Wilaya Biharamulo (5,627 km2), Halmashauri ya Wilaya Bukoba (5,071 km2), Bukoba Manispaa (80km2), Halmashauri ya Wilaya Karagwe (4,630 km2), Halmashauri ya Wilaya Kyerwa (3,086 km2), Halmashauri ya Wilaya Missenyi (2,709 km2), Halmashauri ya Wilaya Muleba (10,739 km2), na Halmashauri ya Wilaya Ngara (3,744 km2).

MUUNDO WA KIUTAWALA

Kiutawala Mkoa wa Kagera umegawanyika katika Wilaya Saba (7) ambazo ni Biharamulo, Bukoba, Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Ngara. Mkoa una Halmashauri za wilaya 7 na ya Manispaa moja (1), Tarafa 27, Kata 192, Vijiji vilivyosajiliwa 662, Mitaa 66 na Vitongoji 3,728. Aidha, Mkoa una Majimbo tisa (9) ya uchaguzi.

IDADI YA WATU

Mkoa wa Kagera una jumla ya watu 2,989,299 wanawake 1,530,019 na Wanaume 1,459,280  (sensa ya Mwaka 2022) Mkoa una jumla ya kaya 702,412, wastani wa watu katika  kaya ni 4.3  na katika mkoa kila kilometa ya mraba 1 ya nchi kavu ina wastani wa watu 117. Aidha, Pato la Mkoa wa Kagera ni Shilingi milioni 4,352,005 ambapo pato la mwananchi mmoja mmoja ni Shilingi 1,445,861 (NBS Tanzania 2022) kwa mwaka.

WATU WA MKOA WA KAGERA

Kabla na baada ya kuja kwa wakoloni Mkoa wa Kagera ulikuwa na utawala wa Kimila (Chiefdoms) uliogawanyika katika himaya 8. Himaya hizo ni pamoja na Kyamutwara, Kihanja (Kanazi), Kiziba, Ihangiro, Bugabo, Karagwe, Biharamulo (Rusubi) na Maruku (Bukara).

Baadhi ya Watemi waliotawala himaya hizo ni pamoja na Emmanuel Rukamba (Kyamtwara), Rumanyika (Karagwe), Kasusura (Biharamulo), Lugomola (Bukara), Rutinwa (Kiziba), Kayo za (Bugabo), Kahigi (Kihanja) na Nyarubamba (Ihangiro). Kila mtemi alikuwa na walinzi wake walioitwa Warugaruga.

Makabila yanayopatikana hivi sasa katika mkoa wa Kagera ni pamoja na Wahaya ambao wanapatikana zaidi katika wilaya za Bukoba, Muleba na Missenyi. Makabila mengine ni Wanyambo, wanaopatikana katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa, Wasubi katika wilaya ya Biharamulo, Wahangaza wanaopatikana katika Wilaya ya Ngara. Pia kuna Waha, Wazinza and Warongo.

Baada ya kuja kwa wazungu waliongeza ulimaji wa kahawa kama zao la biashara lililowasaidia kujiongezea kipato. Wakazi wa asili ya Kagera ni wabantu na wengi wao wanaasili ya Bunyoro. Wanaongea lugha sawa na ile ya Wanyoro, Wanyankole, Watoro na Wakiga. Busubi na Bugufi wana lugha na desturi sawa na Watusi, Wahutu na Waha. Lakini makabila hayo ni ya Wabantu wa Ziwa (Interlacustrine Bantu) na yanafanana mila na desturi.

Makundi hayo yaligawanyika katiya wachungaji (Bahima) ambao walitawala na wakulima (Bairu) ambao walitawaliwa na mara nyingi kudharauliwa. Bahima (Balangira) walikuwa na koo chache zipatazo 20 na walitawaliwa na Wahinda, Wabito na Wankango Bairu walikuwa na koo kama 130 zenye mashina 24 ambayo kiasili walikuwa Bairu lakini kwa kuoa katika Bahima au kufanya kazi kwa Watemi walipandishwa hadhi na kuwa Bahima (Batware). Kila ukoo uliitwa jina la Baba mwanzilishi wake na kina ukoo ulikuwa na kitu walichokatazwa kula (Omuziro) na mnyama walioshirikishwa nae (Ekyerumono).

HALI YA HEWA

Hali ya hewa ya Mkoa wa Kagera kwa ujumla ni ya joto la wastani wa 26.02 sentigredi. Mvua zinanyesha kwa wastani wa milimita 800-1,100 kwa mwaka kati ya mwezi Septemba na Januari na kati ya mwezi Machi na Mei. Mvua hizi ndizo zinazowezesha kuwepo kwauoto wa asili wa kuvutia katika maeneo mengi ya mkoa. Kwa miaka ya kawaida mkoa hupata mvua za uhakika za vuli na masika ambazo ni muhium kwa shughuli za kilimo na ufugaji.

SHUGHULI ZA KIUCHUMI

Uchumi wa wenyeji wa mkoa wa Kagera ulijikita katika mashamba ya migomba na kahawa. Chakula chao kikuu ni ndizi katika aina zake mbalimbali. Katika mashamba yao hulima mazao mengine kufuatana na msimu. Mazao hayo ni pamoja na maharage, mihogo, mahindi na mboga.

ORODHA YA WAKUU WA MKOA WA KAGERA TANGU UHURU MWAKA 1961 HADI SASA

NA.
PICHA
JINA KAMILI

MWAKA WA KUINGIA

MWAKA WA KUTOKA

26.
 Hajjat Fatma Abubakar Mwassa
2023
-

25.

 Bw. Albert John Chalamila
2022
2023
24.


 Maj.Gen.Charles M. Mbuge

2021

2022

23.


 Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti

2018
2021


22.



 Maj. Gen.(Mst) Salum M. Kijuu


2016


2018


21.



 Bw. John V.K. Mongella


2014 


2016


20.



 Col. (Mst) Fabian I. Massawe           


2011


2014


19.



 Bw. Mohammed A. Babu         


2009


2011


18.



 Col. Enos Mfuru


2006


2009


17.




 Gen. T. N. Kiwelu


1999



2006


16.



 Bw. Mohammed A. Babu


1996


1999


15.



 Bw. Philip J. Mangula


1993


1996


14.

 

 
 Capt. A. M. Kiwanuka       

      


1991


1993


13.


 
 Bw. Paul Kimiti                       


1989


1991


12.



 Bw. Horace Kolimba


1987


1989


11.

 


 
 Lt. Col. Nsa Kaisi                     

1981

1987


10.



 Capt. Peter  Kafanabo            


1978


1981


09.

 



 
 Bw. Mohamed Kisoki

1977

1978


08.



 Col. T. A. SIMBA


1975


1977

07.

 


  Brig. M. M. Marwa

1974

1975


06.



 Maj. Gen. Twalipo


1972


1974


05.

 


 
BW. L. N. Sijaona



1970

1972

04.

 


 BW. P. C. Semshanga

1967

1970

03.

 


 Bw. P. C. Walwa

1966

1967

02.

 


 BW. Osward Marwa       

1964

1966


01.


 
Bw. Samwel N. Lwangisa


1961


1964

 

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa