- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa ameeleza kuwa kupitia TARURA, Mkoa wa Kagera unahudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya kilometa 8,369 huku akisisitiza matokeo bora katika utekelezaji wa miradi ya hiyo na ushirikishwaji wa wananchi ili kujua vipaumbele vyao kabla ya utekelezaji wa miradi
Amesema hayo katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika leo, tarehe 10, Juni, 2023 katika ukumbi wa ofisi yake na kueleza kuwa watendaji wa Serikali wapo kwaajili ya kusimamia watu hivyo ni vema kutekeleza na kutatua changamoto za wananchi ili kuwaondolea kero wananchi. Huku akisihi kuzingatia ubora na viwango stahiki vya utekelezaji wa miradi hiyo.
“Tunataka ubora,tunafanya hii miradi tunawaachia wananchi, sisi leo tupo Kagera kesho tutakuwa mahali pengine, hawa tunaowaacha huku na miradi iliyo chini ya viwango wanabaki kutaabika. Tusikubali uzembe wetu ututafune,” ameeleza Mhe. Mwassa
Ameendelea kueleza kuwa kila miradi inayotekelezwa vifaa kama vifusi, kokoto vitapimwa kwa vipimo vya maabara. Na kuongeza kuwa kupandisha hadhi barabara kuna ambatana na faida na changamoto. Barabara ikishasajiliwa ndipo inapata uhalali wa kuingizwa kwenye bajeti na kupangiwa fedha kwa ajili ya matengenezo mbalimbali.
Ambapo changamoto yake lazima ikidhi vigezo kama upana na urefu hivyo kupelekea kuchukua ardhi za watu binafsi au taasisi katika eneo husika.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Ndg. Toba Nguvila amewasihi watumishi wakiwemo wataalam wa TARURA na TANROAD kutoa elimu kwa wananchi kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi hiyo ili kuondoa changamoto zikiwemo za madai ya fidia pale mradi unapoanza kutekelezwa
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali Wilson Sakulo ameeleza kuwa barabara ni fursa wananchi wanapopelekewa barabara ni fursa ya maendeleo hivyo ni vema kupitia vikao vya Waheshimiwa Madiwani elimu itolewe ili watu wafahamu juu ya fursa hiyo.Na kusisitiza juu ya barabara za ulinzi kwa kutoa mfano katika Wilaya ya Missenyi, barabara ya kutoka Kakunyu kwenda jiwe namba 27 ili kufika eneo la namba 27 mpaka wa Tanzania na Uganda unapita Nchi ya Uganda,hivyo kuwasihi TANROAD kutekeleza barabara hiyo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa