- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Hatimaye Mkoa wa Kagera wazindua rasmi vitambulisho vya taifa kwa watumishi 22,771 ambao ni sawa na asilimia 98% ya watumishi wote wa mkoa walioandikishwa na NIDA kama awamu ya kwanza ya utangulizi ili kuandaa uandikishaji kwa wananchi wote wa mkoa wa Kagera.
Akitoa taarifa Afisa Msajili wa NIDA mkoa wa Kagera Bw. Hassan M.Godigudi alisema kuwa katika Mkoa wa Kagera una jumla ya watumishi 23,190 ambapo kati ya hao waliosajiliwa ni 22,771 sawa na asilimia 98% jambo ambalo ni mafanikio makubwa ya uandikishaji.
Aidha, Bw. Hassan alisema dhumuni kuu kuanza usajili wa vitambulisho vya Taifa kwa watumishi wa umma ulilenga watumishi hao kuwa mabalozi wazuri na waelimishaji wa wananchi juu ya kujisajili kupata vitambulisho vya taifa ambapo watakaoruhusiwa kujisajili ni raia wa Tanzania tu na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Pia Bw. Hassan alisema kuwa kitambulisho cha Taifa kuna faida nyingi kwa mwananchi yeyote katika kutatua masuala mbalimbali kama kupata mikopo katika taasisi mbalimbali za kifedha pia na kuwa na utambulisho halali na wa kudumu sehemu mbalimbali za ndani ya nchi na nje ya nchi.
Vilevile Bw. Hassan aliomba vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Mkoa wa Kagera chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Kagera kuhakikisha wanasimamia uandikishaji wa wananchi amabao ni raia wa Tanzania tu ili kuepuka uandikishaji watu ambao sio raia wa Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. kijuu akizindua vitambulisho hivyo vya taifa kwa Mkoa wa Kagera aliwapongeza NIDA kusajili watumishi wa umma kwa asilimia 98% na kusema kuwa jambo hilo ni mafanikio makubwa aidha, alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo wakati ukifika.
Mhe. Kijuu alisema kuwa kwasababu Mkoa wa Kagera upo mpakani na nchi nyingine atahakikisha kuwa vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama vinasimamia kwa karibu sana zoezi la uandikishaji ili kuepukana na kuandikishaji na utoaji wa vitambulisho vya Taifa kwa watu wasiokuwa raia wa Tanzania au wale ambao hawajafikisha umri wa miaka 18 na kuendelea.
Mkuu wa Mkoa Kijuu pia alisema kuwa uzinduzi huo siyo kwamba ndiyo mwisho wa utoaji wa vitambuklisho vya taifa bali ndio mwanzo wa uandikishaji wa wananchi kupata vitambulisho vya taifa. Pia alitoa wito kwa wananchi kuwa wazalendo wakati wa uandikishaji kujitokeza na kuwabaini wasio raia. Uzinduzi huo ulifanyika Aprili 5, 2017 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa