- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwendelezo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Kagera Mwaka 2018
Mwenge wa Uhuru waendelea na mbio zake Mkoani Kagera ambapo tayari Mwenge huo umekimbizwa katika Halmashauri tano za Muleba, Bukoba, Bukoba Manispaa, Missenyi na Kyerwa kati ya Halmashauri nane za Mkoa wa Kagera, aidha, tayari miradi 44 yenye thamani ya shilingi 6,309,492,560.70 imetembelewa, kukaguliwa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi.
Miradi hiyo 44 ni kati ya miradi 65 ya mkoa mzima wa Kagera itakayopitiwa na Mwenge Uhuru wa mwaka huu 2018. Thamani ya miradi hiyo 44 shilingi bilioni 6,309,492,560.70 ni kati ya shilingi bilioni 12,385,330,354 za miradi yote katika Mkoa kwenye Halmashauri za Wilaya.
Akito ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2018 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Charles F. Kabeho katika Halamashauri za Wilaya ambazo tayari zimepitiwa na Mwenge wa Uhuru aliwasistiza wananchi kuwekeza katika Elimu kwa watoto wao ili kuhakikisha watoto hao wanapata Elimu bora kwa manuaa ya taifa na mkoa wa Kagera hapo baadae.
“Serikali imetoa na inaendelea kutoa fedha nyingi kuhakikisha wanafunzi wa darasa la kwanza hadi kidato cha nne wanasoma bure, lakini Serikali kutoa fedha hizo hakujazuia majukumu ya wazazi katika kuhakikisha watoto wao wanapata Elimu bora” Alisisitiza Kiongozi wa Mbio za mwenge 2018 Charles Kabeho.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge aliongeza kuwa wazazi wanatakiwa kuhakikisha watoto wao wanapata chakula shuleni kulingana na Waraka wa Serikali unavyoelekeza. Pia Wazazi wanatakiwa kuwanunulia watoto wao sare za shule, kuwalipia nauli za kwenda shule na kuhakikisha watoto wana vifaa vyote vya shule kama madaftari na kalamu.
Katika Hatua nyingine Kiongozi wa Mbio za Mwenge aliwasisitiza wananchi wa mkoa wa Kagera kuachana na upikaji wa gongo na kusisitiza kuwa gongo ni mojawapo ya dawa za kulevya ambazo hazistahili kutumika katika jamii.
Pongezi, pia aliupongeza mkoa kwa kupambana na utoro wa wanafunzi shuleni kwamba mkoa huu unajithidi kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo yao shuleni lakini alisisitiza uongozi wa Mkoa kuongeza juhudi ili kufuta suala la utoro shuleni.
Mwenge wa Uhuru ulipokelewa Mkoani Kagera Aprili 8, 2018 na tayari umekimbizwa katika Halmashauri za Wilaya za Muleba, Bukoba, Bukoba Manispaa, Missenyi na Kyerwa. Aidha, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa katika Halmashur za Karagwe, Ngara na Biharamulo na utakabidhiwa Mkoa wa Kigoma tarehe 16 Aprili, 2018.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa