- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora katika kusimamia maendeleo ya mkoa kupitia sera ya kila mwananchi kujikwamua kiuchumi kwa kuzalisha na kujiingizia kipato halali kupitia kazi anayoifanya atembelea na kukagua miradi ya maendeleo Visiwani Wilayani Muleba na kuongea na wavuvi kwa kuwaelimisha juu ya uvuvi wa kisasa wenye tija na kukuza uchumi.
Akifanya ziara ya siku mbili Machi 28 hadi 29, 2019 katika visiwa vinne vya Kimoyomoyo, Mulumo, Kassenyi, na Chakazimbwe katika Kata za Mazinga na Ikuza Prof. Kamuzora alikagua miradi ya maendeleo hasa ujenzi wa ghati katika visiwa hivyo na kushauri miradi hiyo isimamiwe vizuri na ujenzi uzingatie viwango vya ujenzi ili mara baada ya kukamilika ziweze kudumu zaidi ya miaka 100.
Pamoja na kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo pia Prof. Kamuzora alimtembelea Bw. Issa Jiwa Mjasiliamali anayechakata dagaa kwa kuowaongezea thamani na kuuza katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Pia Prof. Kamuzora alijionea wavuvi wengine wanavyochakata mazao ya samaki hasa uanikaji wa dagaa.
Katika mikutano yake na wananchi waishio visiwani Prof. Kamuzora mara baada ya kutembelea na kukaua miradi ya maendeleo aliwaelimisha wananchi hao kuzingatia ubora wa mazoa wanayoyazalisha hasa ubora wa samaki au dagaa wanapochakatwa kabla ya kufikishwa sokoni.
Prof. Kamuzola alikaripia vikali wavuvi wanaoanika dagaa chini kuwa hairusiwi kufanya hivyo kwani dagaa wakianikwa chini kwenye mchanga ubora wake unapungua katika masoko ya ndani api masoko ya nje ya nchi. Dagaa hao huwa na mchanga jambo ambalo huleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji.
“Hapa nchini Tanzania tuna tatizo kubwa la uharibifu baada ya mavuno (Post Harvest Loss) yaani unakuta mwananchi anahangaika kuzalisha bidhaa zake ili akauze sokoni lakini anashindwa kuziandaa bidhaa hizo katika hatua za mwisho wakati wakuzipeleka sokoni jambo ambalo linapelekea hasara kubwa kwa mhusika na wakati mwingine kusababisha madhara kwa watumiaji.” Alitahadharisha Prof. Kamzora
Prof. Kamzora aliwaagiza Maafisa Uvuvi na Maafisa Afya visiwani humo kuhakikisha wanatekeleza sheria ya uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 katika kusimamia masuala ya uvuvi na uchakataji wa mazao yake na kuchukua hatua kali kwa wale wote ambao wanaoendelea kukiuka sheria, taratibu na kanuni za uvuvi.
Pia Prof. Kamuzora akiongea na wananchi katika mikutano ya hadhara aliwaelimisha juu ya lishe hasa wazazi kuhakikisha wanapata elimu juu ya lishe ili kuondoa utapiamlo kwa watoto ambapo madhara ya utapiamlo ni makubwa katika makuzi ya watoto na madhara yake huonekana hata kama mtu akiwa mtu mzima.
Vilevile wananchi waishio visiwani walielimishwa kuhakikisha wanajiunga na bima ya afya iliyoboreshwa ili iweze kuwasaidia pale wanapokuwa wagonjwa au pale wanapokuwa wamepoteza uwezo wakufanya kazi kuvua samaki badala ya kurudishwa nyumbani nchi kavu badala yake wapatiwe matibabu au huduma ya afya hukohuko visiwani.
Katika hatua nyingine Prof. Kamuzora aliwapongeza wananchi katika visiwa alivyotembelea kwa kuchangia shilingi milioni 17 kwaajili ya ununuzi wa boti ya doria za ulinzi na kuwaomba kuendelea kuchangia ili boti hiyo yenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 29 iweze kununuliwa na kuanza kazi mara moja kuondoa maharamia wanaowasumbua wavuvi katika shughuli zao.
Mwisho Prof. Kamzora aliwaasa wavuvi kuachana na uvuvi haramu au kutumia zana haramu katika kuvua ambapo alichoma nyavu haramu katika kisia cha Chakazimbwe. Pia aliwasisitiza wananchi kuendelea kushirikiana na Halmashaur ya Wilaya ya Muleba kutekeleza miradi ya maendeleo kama kujenga shule na zahanati ili wapate huduma nzuri za kijamii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa