- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkoa wa Kagera waadhimisha siku ya Malaria Duniani kwa kuhamasisha wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kushiriki katika kupunguza kiwango kikubwa cha ugonjwa wa Malaria hasa kwa watoto wa Shule za Msingi kwa kuzingatia usafi na kuharibu mazalia ya mbu na kuzingatia kanuni za afya.
Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliyekuwa mgeni rasmi na kuwakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Missenyi Bw. Abdalla Mayombo aliwasisitiza wananchi woe wa Mkoa wa Kagera kusafisha mazingira yaliyo karibu na makazi yao kama vile vichaka na madimbwi ili kuua mazalia ya umbu.
Pia katika hotuba hiyo Mkuu wa mkoa aliwasisitiza wananchi kushirikiana na wadau ambao wanausaidia mkoa katka mapambano ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa kuruhusu nyumba zao kunyunyiziwa dawa ya ukoko , kuhakikisha wanapokea vyandarua ambavyo vinagawiwa katika vituo vya afya.
Kwa utafiti wa kitaifa wa maambukizi ya malaria uliofanyika mwaka 2015/2016 kwa watoto wenye umri chini miaka mitano mkoa wa Kagera maambukizi yalikuwa asilimia 41% , asilimia hiyo ilipanda sana ukilinganisha na utafiti uliofanyika mwaka 2010/2011 maambukizi yalikuwa ni asilimia 8.5%
Aidha, kwa mwaka 2016 utafiti wa vimelea vya Malaria kitaifa kwa watoto wa Shule za Msingi ulionesha kuwa Mkoa wa Kagera ulikuwa na asilimia 30.2% na Wilaya ya Missenyi ilikuwa na aasilimia 69% ambapo kiwango hicho kilikuwa juu ya kiwango cha taifa na mkoa kwa ujumla.
Akisistiza katika hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw. Abdalla Mayombo alisema kwa umoja na kushirikiana na wadau mbalimbali kiwango hicho cha vimelea kinatakiwa kushushwa ili kukomesha maambukizi ya malaria katika Mkoa wa Kagera .
Kaulimbiu ya Siku ya malaria mwaka huu 2017 ambayo huadhimishwa kila mwaka Aprili 25 inasema, “Shiriki kutokomeza ugonjwa wa Malaria kwa manufaa ya jamii” Aidha wadau mbalimbali wanaoshirikiana na Mkoa wa Kagera katika kutokomeza Malaria ni ABT Associates, John Hopkins University, na Shirika la Redcross Tanzania.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa