- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jeneral Marco E. Gaguti na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa, wakiongoza timu za Vijana wa Bodaboda JPM Bodaboda Kagera 2020 na timu ya Bodaboda kutoka mkoani Mtwara wafanya ziara ya kutembelea na kujionea miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkoa wa Dar es salaam.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Desemba 13, 2020 Wakuu hao wa Mikoa na vijana waendesha Bodaboda walitembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR na jengo la abiria la Tanzanite, Mradi wa Mabasi ya mwendokasi, Ujenzi wa stendi mpya ya Mabasi ya Mbezi Luis, Daraja la Juu Ubungo na Mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi namba mbili.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa alisema waliamua kuwaleta vijana waendesha Bodaboda kwenye ziara hiyo ili waweze kujionea Mambo mazuri na makubwa yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ili wawe mabalozi wazuri kwa wenzao.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jeneral Marco E. Gaguti aliipongeza Serikali kwa kazi kubwa na nzuri iliyofanyika katika utekelezaji wa miradi yenye lengo la kutatua kero kwa wananchi.
Aidha, Brigedia Jenerali Gaguti amesema mbali na ziara hiyo timu ya vijana wake JPM Bodaboda Kagera 2020 awali Desemba 12, 2020 walifanya shindano la Mpira wa miguu kati ya Timu ya Bodaboda Mtwara kwa lengo la kujenga uzalendo kwa kundi hilo la vijana na kuwafanya kuwa mabalozi wazuri wa shughuli za Serikali.
Vile vile Wakuu hao wa Mikoa ya Kagera na Mtwara walisema kuwa wanatamani kuona mikoa yote Tanzania inawaunganisha vijana wa kundi hilo la Bodaboda ili washiriki kikamilifu katika sshughuli za ulinzi na usalama pia kupata elimu ya usalama barabarani, huduma ya kwanza katika shughuli zao na kuwezeshwa kwa mafunzo ya ujasiliamali katika vikundi ili kupata mikopo ya kuzalisha na kupata kipato nje ya kazi yao ya Bodaboda.
(Habari hii ni kwa Msaada wa Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa