- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kupeleka vitendea kazi na vifaa tiba kituo cha afya Kakunyu ndani ya siku tano ili kianze kutoa huduma
Akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua mradi huo uliogharimu Tsh. milioni 610 kwa fedha za mapato ya ndani na Serikali kuu, unaotarajiwa kuhudumia wakazi wapatao elfu 26 ameeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kila baada ya miezi mitatu inapokea fedha Tsh. milioni 135 kwa ajili ya kununua dawa, hivyo fedha zipo.Halmashauri ikamilishe taratibu za ununuzi wa madawa na vifaa tiba huduma ianze kutolewa
"Nawapa siku 5, jengo hili la mapokezi na magonjwa ya kawaida lianze kazi. Nikimaliza ziara leo mlete samani, vitendea kazi, madaktari tayari wapo hapa, fedha za madawa zipo hivyo wananchi waanze kupata huduma," ameeleza Mhe. Majaliwa
Ameendelea kueleza kuwa Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi kwa Wilaya ya Missenyi ndani ya miaka miwili shule, barabara, zahanati na vituo vya afya vimejengwa. Umeme unaendelea kusambazwa katika vijiji vyote na miradi ya maji imetekelezwa kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alidhamiria kumtua mama ndoo kichwani.
Amesisitiza juu ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji kwa kuwataka Serikali za Vijiji na kamati za mazingira kusimamia na kuchukua hatua kwa watu wanaoharibu mazingira na vyanzo vya maji ili Nchi iendelee kupata mvua na maji ya kutosha ya matumizi ya majumbani, kilimo na mifugo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Festo Dugange amemshukuru Waziri Mkuu kwa kufika na kutembelea kituo hicho cha afya huku akieleza kuwa kwa Wilaya ya Missenyi, Rais Dkt. Samia ametoa fedha Tsh. bilioni 4.8 kwa sekta ya afya na kati ya hizo hospitali ya kisasa ya Wilaya imejengwa.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Florent Kyombo ameeleza kwa miaka miwili shule ya sekondari kubwa ambayo ilikuwa hitaji kubwa la wananchi imejengwa, miradi ya maji na kituo cha afya kimejengwa, vijiji vya Bugango na Kakunyu nguzo za umeme zinajengwa kuwaunganishia umeme wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa