- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri Mkuu Mstaafu Aagiza Chuo Kikuu Huria Tanzania Kuanzisha Kozi Fupi Kwa Watumishi Ili Kuendana na Sera ya Viwanda
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania aagiza chuo hicho kuandaa kozi fupi kwa kada mbalimbali ili kuwawezesha watumishi wa umma kuendana na utekelezaji wa Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Serikali ya Viwanda.
Waziri Mkuu Mstaafu Pinda aliyasema Hayo alipofanya ziara Mkaoni Kagera Februari 23, 2018 ili kukagua miundombinu na maendeleo ya Chuo Kikuu Huria Tanzania Tawi la Kagera ambapo alipongeza juhudi za zinazoendelea kuchukuliwa kukiendeleza chuo hicho Tawi la Kagera.
Akiongea na wanafunzi, watumishi , uongozi wa chuo hicho na uongozi wa Mkoa wa Kagera katika viwanja vya Chuo Kikuu Huria Tawi la kagera Migera Manispaa ya Bukoba Waziri mkuu Mstaafu Pinda alisema chuo hicho ni Chuo cha wananchi na kinawafuata wananchi badala ya wananchi kukifuata chuo.
“Chuo hiki ni chuo cha wananchi kwani hakimlazimishi mwananchi kuacha familia yake au mtumishi kuacha majukumu yake ya kazi kwenda kusoma mbali bali mwananchi yeyote atasoma mahali popote alipo kwan i Chuo chetu kina matawi kila Mkoa na kwa sasa kila Wilaya.” Alifafanua Mhe, Pinda.
Mhe. Pinda alisema pia kuwa tayari amemwagiza Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Elphazi Bisanda na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Profesa Rwekaza Mkandara kuhakikisha wanaangalia uwezekano wa kuandaa kozi fupi kwa watumishi wa umma kama Watendaji wa kata juu ya kusimamia sera ya viwanda pia kozi hizo zitawafanya watumishi waendane na wakati wa Sayansi na Teknolojia.
Mhe. Pinda alitoa mfano wa Nchi ya Korea Kusini kuwa Vyuo Vikuu Huria nchini humo vilisaidia sana katika kuwanoa watumishi ambao baadae walikuja kutoa mchango mkubwa katika mapinduzi ya kiuchumi na nchi hiyo kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika Sayansi na Teknolojia .
Katika Kuhitimisha Mhe. Pinda alimwomba Mkuu wa Mkoa Kagera kuhakikisha watumishi wa umma wanaruhusiwa kutumia fursa ya chuo hicho kujiendeleza kielimu, pili aliwaomba wanafunzi wa chuo hichio kusoma kwa bidii ili kupambana na ushindani wa vyuo vingine na ikiwezekana wasome kwa muda muafaka kama vyuo vingine pia mfano badala ya kusoma shahada ya kwaza kwa zaidi ya miaka mitatu iwe mitatu tu.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Huria Tanzania Prof. Elphazi Bisanda alisema kuwa Mkoa wa Kagera una mwitikio mzuri wa wanafunzi wanaojiandikisha kusoma katika chuo hicho. Ambapo alihaidi kuwa matawi zaidi yatazidi kufunguliwa ili chuo kiwafutae wananchi. Tawi jipya linalotarajiwa kufunguliwa ni Katika Wilaya ya Biharamulo.
Prof. Bisanda alihaidi kuwa uongozi unaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya Chuo Kikuu Huria Tawi la Kagera ili miundombinu hiyo iwe na hadhi ya chuo Kikuu. “ Tunaendelea kuboresha miundombinu ya hapa kadri tunavyopata fedha na nina uhakika kuwa tutaweza kufika tunapopataka. Alifafanua Prof, Bisanda
Naye mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu akimshukuru Mhe. Pinda kwa kuja Kagera kutembelea Chuo Kiku Huria Tawi la Kagera alisema Mkoa wa Kagera ni wa tatu kutoka mwisho kwa umasikini lakini kwa sasa kuna juhudi kubwa zinafanyika ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujiendeleza ili kuutoa Mkoa kwenye nafasi hiyo ya tatu toka mwisho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa