- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Wilayani Muleba imeanzia Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), kilichopo Kijiji cha Bushagara, Kata ya Kamachumu kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho kitakachogharimu kiasi cha Tsh. milioni 903.
Akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi,
ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta fedha ili vijana wapate nafasi ya kujifunza ufundi katika fani wanazotamani. Na Chuo hicho kinachukua vijana wa ngazi zote kuanzia darasa la saba mpaka Chuo Kikuu kwani wapo vijana wanahitimu Chuo kikuu lakini hawawezi kujenga, kushona hivyo wakaja hapa kwaajili ya kupata mafunzo ya ujuzi.
“Wazazi wa eneo hili na Wilaya hii hakikisheni vijana wetu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa majengo yanayojengwa na kwakuwa Mkurugenzi Mkuu amesema anapanua wigo wa Chuo kuwa na kozi takribani 200 ni nafasi nzuri ya kuwaleta vijana ili wapate ujuzi,” ameeleza Mhe. Majaliwa
Amewatoa wasiwasi vijana kuwa Serikali imetoa maelekezo kwa kila Halmashauri kuhakikisha wanatenga bajeti kila mwaka ili kuwezesha wanafunzi wanaohitimu kuwa na mtaji wa kuanza shughuli waliyosomea. Aliyejifunza cherehani Halmashauri itenge bajeti kwa ajili ya kutoa cherehani na kuwaanzishia mitaji ili waanzishe maeneo yao ya kushona.
CPA Anthony Kasore, Kaimu Mkurugenzi Mkuu VETA ameeleza kuwa mnamo mwaka 2019, Serikali ilianzisha mpango wa kuhakikisha kila Wilaya inakuwa na chuo cha kuongeza ujuzi katika maeneo ya Wilaya. Serikali ilitenga fedha na kutoa takribani Tsh. bilion 4.9 kwa ajili ya kutengeneza na kukarabati majengo ya taasisi mbalimbali ambayo yalikuwepo ili kuyabadilisha na kuwa vyuo vya ufundi stadi.
Majengo yanayojengwa ni bweni la wavulana, bweni la Wasichana, bwalo la chakula, karakana ya umeme na uchomeleaji, nyumba ya Mkuu wa Chuo na jiko la kupikia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa