- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
|
Katika kipindi cha kuanzia 2020 hadi Juni 2024, Mkoa wa Kagera umepokea jumla ya Shilingi Bilioni 54.4 kutoka vyanzo mbalilmbali kwa ajili ya Ujenzi, Ukarabati wa Miundombinu ya huduma za afya na ununuzi wa vifaa tiba. Ifuatayo ni miradi ya ujenzi iliyotekelezwa:
|
|
Ujenzi wa Hospitali za Wilaya
Ujenzi wa Hospitali za Wilaya Katika Halmashauri za Wilaya za Karagwe, Bukoba, Kyerwa, Ngara, Missenyi na Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba zimekamilika na zinatoa huduma. Aidha, ujenzi wa hospitali za Wilaya za Muleba na Biharamulo zipo hatua mbalimbali za ujenzi.
Vituo vya Afya:
Ujenzi wa vituo vya afya vipya 24 umekamilika katika Halmashauri za Karagwe, Bukoba, Kyerwa, Ngara, Missenyi, Muleba, Biharamulo na Manispaa ya Bukoba umekamilika na vyote vinatoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera
Zahanati
Ujenzi wa zahanati mpya 40 katika Halmashauri za Karagwe, Bukoba, Kyerwa, Ngara, Missenyi, Muleba, Biharamulo na Manispaa ya Bukoba umekamilika na vyote vinatoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera. Aidha, kukamilika kwa vituo hivi kumeimasha utoa wa huduma za afya ikiwa ni pamoja na huduma ya upasuaji kwa akina mama wajawazito wanaohitaji huduma hiyo.
Mkakati wa Mkoa kukabiliana na magojwa ya mlipuko
Mkoa una mikakati ya kukabiliana magojwa ya mlipuko hasa ukizingatia Mkoa wetu upo mpakani. Kwa kipindi cha miaka minne Mkoa umejenga vituo kumi na mbili (12) (isolation wards) ya kuwahudumia wagonjwa wanaohisiwa kuwa na magonjwa hayo wakati uchunguzi ukufanyika. Adha, Mkoa umetoa mafunzo maalumu kwa watumishi 155 wa afya kwa ajili ya kutoa huduma pindi magonjwa ya mlipuko yanapotokea.
Mafanikio mengine ya Huduma za Afya ndani ya Mkoa kwa Kipindi miaka minne yaani kuanzaia 2020 hadi 2024 ni kama ifuatavyo.
LENGO LA HUDUMA ZA AFYA MKOANI KAGERA |
Lengo la Huduma za Afya Mkoani Kagera ni kuwezesha utoaji wa Afya ya Kinga, Tiba, Maendeleo ya Afya na Ustawi wa Jamii kwenye Mkoa. Aidha, Mkoa unafanya kazi ya kuratibu na kushauri juu utekelezaji wa Sera ya Afya kwenye Mkoa
|
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa