- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkoa wa Kagera Utoa Huduma zifuatazo Katika Sekta ya Elimu:
ELIMU MKOANI KAGERA KWA KIPINDI CHA MIAKA MINNE 2021 HADI 2024
Kwa upande wa sekta ya elimu kwa kipindi cha miaka minne Mkoa umepokea jumla ya shilingi Bilioni 115.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu na uendeshaji wa Elimu msingi bila malipo. Miradi ya Ujenzi na ukarabati kama ifuatavyo:
Kutokana na mapokezi ya fedha kwa ajili ya kujenga/kukarabati miundombinu ya elimu, Mkoa umepata mafanikio yafuatayo:
a) Kuongezeka kwa idadi ya Shule za Msingi za Serikali kutoka shule 933 novemba 2020 hadi 976 Septemba 2024 ikiwa ni ongezeko la shule 43 sawa na asilimia 46.09
b) Kuongezeka kwa idadi ya Shule za Sekondari kutoka shule 203 novemba, 2020 hadi 245 Septemba, 2024 sawa na ongezeko la shule 42 sawa na asilimia 20.69
c) Kuongezeka kwa vyumba vya madarasa katika shule za msingi za Serikali kutoka vyumba 1606 novemba,2020 na hadi 7610 Septemba, 2024 ikiwa ni ongezeko la vyumba 6,004 sawa na asilimia 373.84
d) Kuongezeka kwa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari za Serikali kutoka vyumba 3322 novemba, 2020 hadi 4340 Septemba, 2024 ikiwa ni ongezeko la vyumba 1018 sawa na asilimia 30.64
e) Kuwepo kwa mwitikio mkubwa wa wazazi katika kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule. Kwa mwaka 2024 uandikishaji wa wanafunzi darasa la kwanza ulivuka lengo hadi kufikia asilimia 107.55
f) Kuongezeka kwa idadi ya walimu katika shule za msingi kutoka walimu 8199 novemba, 2020 hadi 9475 Septemba, 2024 ikiwa ni ongezeko la walimu 1276 sawa na asilimia 15.56
g) Kuongezeka kwa idadi ya walimu katika shule za sekondari kutoka walimu 2384 novemba 2020 hadi 2790 Septemba, 2024 ikiwa ni ongezeko la walimu 406 sawa na asilimia 17.03
Maalum cha Mkoa wa Kagera.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa