- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Hali ya hewa ya Mkoa wa Kagera kwa ujumla ni ya joto la wastani wa 26.02 sentigredi. Mvua zinanyesha kwa wastani wa milimita 600 – 2,000 kwa mwaka kati ya mwezi Septemba na Januari na kati ya mwezi Machi na Mei. Mvua hizi ndizo zinazowezesha kuwepo kwa uoto wa asili wa kuvutia katika maeneo mengi ya Mkoa. Kwa miaka ya kawaida Mkoa hupata mvua za uhakika za vuli na masika ambazo ni muhimu kwa shughuli za kilimo na ufugajiA
Mkoa wa Kagera umegawanyika katika kanda tano (5) za kilimo kuzingatia mwinuko wa maeneo hayo kutoka usawa wa bahari na kiwango cha unyeshaji wa mvua.
Ukanda huu unajumuisha maeneo ya Mashariki ya Wilaya za Bukoba na Muleba yanayo ambaa kando kando ya Ziwa Victoria na uko katika mwinuko wa mita 1,300 mpaka 1,500 kutoka usawa wa bahari. Mvua katika ukanda huu zinanyesha kwa wastani wa milimita 800 - 1,750 kwa mwaka. Shughuli kuu za kiuchumi katika eneo hili ni kilimo cha ndizi, maharagwe, mahindi, kahawa, uvuvi na ufugaji. Eneo la ukanda huu ni asilimia 17 ya eneo la mkoa.
Huu ni ukanda wa juu ulioko kwenye mwinuko wa mita 1,400 mpaka 1,800 kutoka usawa wa bahari. Ukanda huu unajumuisha maeneo ya juu ya Wilaya ya Karagwe, Kyerwa na Ngara na mvua zinanyesha kwa wastani wa milimita 800 - 1,000 kwa mwaka. Mazao yanayolimwa kwenye ukanda huu ni migomba, maharagwe, mahindi, kahawa n.k. Eneo la ukanda huu ni asilimia 19 ya eneo la Mkoa.
Ukanda huu uko katika mwinuko wa mita 1,000 kutoka usawa wa bahari na unajumuisha Wilaya ya Biharamulo. Mvua zinanyesha kwa wastani wa milimita 750 - 800 kwa mwaka. Shughuli kuu za kiuchumi ni uzalishaji wa mazao ya mahindi, mihogo, mpunga, mtama, karanga, tumbaku na pamba. Eneo la ukanda huu ni asilimia 27 ya eneo la Mkoa.
Ukanda huu upo kwenye mwinuko wa mita 1,000 kutoka usawa wa bahari na unajumuisha maeneo ya Mashariki ya Wilaya ya Karagwe, Wilaya ya Missenyi na maeneo ya Magharibi ya Wilaya ya Bukoba. Mvua za ukanda huu zinanyesha kwa wastani wa milimita 800 - 1,000 kwa mwaka. Shughuli kuu za kiuchumi ni kilimo cha mazao ya mahindi, maharagwe, miwa na ufugaji. Eneo la ukanda huu ni asilimia 10 ya eneo lote la Mkoa.
Ukanda huu unajumuisha maeneo ya Kaskazini ya Wilaya ya Karagwe na Missenyi na uko kwenye mwinuko wa mita 1,000 kutoka usawa wa bahari ukanda huu unapata mvua za wastani wa milimita 750 - 800 kwa mwaka. Sehemu kubwa ya ukanda huu ni misitu ya hifadhi na mapori ya akiba. Eneo la ukanda huu ni asilimia 27 ya eneo lote la Mkoa.
Mahitaji ya chakula kwa mkoa wa Kagera ni tani 842,936 (wanga tani 771,239 protein tani 71,697) kwa mwaka. Kwa miaka minne mfululizo uzalishaji wa mazao ya chakula ulikuwa kati ya tani 3,000,000 hadi tani 3,359,276. Hivyo kumekuwa na utoshelevu wa zaidi ya 255% - 300% ambapo ziada inauzwa nje ya mkoa na nje ya nchi.
Uzalishaji katika zao la kahawa kwa miaka minne ni tani 387,464.64 kuanzia msimu wa mwaka 2020/21 hadi msimu wa mwaka 2023/2024 aidha bei imeongezeka kutoka wastani wa Tsh. 1100 hadi kufikia Tsh. 6153 eongezeko la bei 82%.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa