- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kagera Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Vyafanya Mazoezi ya Pamoja Kuendelea Kujiimarisha Kuwalinda Raia na Mali Zao
Vyombo ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya pamoja ili kijiweka tayari na kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza jukumu moja kuu la kuwalinda raia na mali zao.
Mazoezi hayo yaliyofanyika katika Manispaa ya Bukoba Aprili 25, 2018 yameyashirikisha Majeshi ya Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto, Jeshi la Akiba na Jeshi la Wananchi Tanzania.
Akiongea na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Augustino Olomi mara baada ya kuhitimisha mazoezi hayo katika Viwanja vya Gymkhana alisema kuwa ni mazoezi ya kawaida kwa Majeshina kitaalam yanaitwa (Route Match)
“Mkoa wa Kagera tumekuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi haya kila Jumamosi ya kila wiki kwa kushirikiana na wananchi lakini leo wananchi wapo kwenye shughuli zao za uzalishaji, Majeshi kama unavyoyaona tumeshirikiana kufanya mazoezi ya pamoja kwani sote jukumu letu ni kulinda raia na malizao,” Alifafanua Kamanda Olomi
Aliongeza Kamanda Olomi kuwa Majeshi yakifanya mazoezi ya pamoja wanakuwa na utayari wa pamoja kupambana na vitendo ambavyo vinaweza kuhatarisha usalama wa raia na mali zao lakini pia na Askari katika mazoezi haya wanafahamiana kwa karibu jambo linaloleta ushirikiano mzuri katika kazi.
Aidha, Kamanda Olomi alitumia nafasi hiyo kuwatahadharisha wale wote wanaopanga kundamana au kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani siku ya maadhimisho ya Muungano tarehe 26 Aprili, 2018 kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera limejipanga vizuri kushughulika nao kikamilifu.
Kamanda Olomi alisisitiza kuwa mwananchi yeyote asidanganyike kwa kushawishiwa kuandamana na aliwataka wananchi hao kuendelea na shughuli zao za kawaida za baishara, kilimo au kutumia siku hiyo kupumzika kuliko kujihusisha kwenye vitendo ambavyo vinaweza kuwaletea matatizo.
Mazoezi ya pamoja ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera yalianzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kupitia katikati ya mji wa Bukoba kuelekea Kashai na yamehitimishwa katika Viwanja vya Gymkhana karibu na Bukoba Club.
Wito kwa wananchi wote hususani Manispaa ya Bukoba mnakaribishwa kila Jumamosi ya kila wiki kujumuika pamoja watumishi kufanya mazoezi ya pamoja kwaajili kuimarisha miili yetu, mazoezi hayo huanzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa saa 12:00 Asubuhi na kumalizikia katika viwanja vya Gymkhana saa 3:00 asubuhi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa