- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
EWURA Yawaelimisha Wafanyabiashara wa Mafuta Kagera Ili Kutoa Huduma Bora kwa Walaji
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yatoa elimu kwa watoa huduma ya Mafuta (Wafanyabiashara ya mafuta) Mkoani Kagera lengo kuu likiwa ni kuwaelimsha jinsi ya kutoa huduma zao kwa walaji (Watumiaji wa Mafuta) na kufuata sheria na kanuni katika kufanya biashara zao.
Akitoa mada juu ya Sheria na Kanuni katika udhibiti wa sekta ya Petroli nchini Mhandisi Godwini Samwel Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA alisema kuwa Mamlaka inatoa elimu kwa Wafanyabiashara nchi nzima ili wazielewe sheria na kanuni za kuendesha biashara za mafuta ili Mamlaka isiwatoze faini kwa kukiuka sheria na kanuni kumbe hawakuelimishwa awali na Mamlaka hiyo.
Aidha, Mhandisi Samweli alisema kuwa Mamlaka inatoa elimu kwa wafanyabiashara wa mafuta wazijue vizuri Sheria na kanuni za kuendesha biashara hiyo ili kumlinda mlaji ambaye ni mtumiaji wa mafuta naye apate mafuta yenye viwango kwa bei sahihi na katika mazingira yanayokidhi viwango vya kutolea huduma hiyo.
Katika semina hiyo wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera walitoa changamoto zao katika kuendesha biashara za mafuta ikiwa ni pamoja na EWURA na Mamlaka nyingine kuchelewesha taratibu za utoaji wa vibali vya kuanzisha vituo vya mafuta ambapo vibali hivyo huchukua muda mrefu zaidi ya mwaka tangu mwombaji aombe kupata leseni.
Akitoa majawabu ya changamoto hiyo Mhandisi Samweli alisema kuwa tayari Mamlaka (WEWURA) wamekaa na wadau wengine kama NEMC wanaohusika na usimamizi wa mazingira na kuwekeana mkakati wa kuhakikisha utoaji wa vibali unakwenda haraka ili kutowakwamisha wafanyabiashara , mfano kwasasa (EWURA) wanashughulikia leseni kwa siku 45 tu kama mwombaji atakuwa ametimiza vigezo vyote.
Wafanya biashara walioshiriki katika semina hiyo waliishukuru Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuwapa elimu juu ya sheria na kanuni za kuendesha biashara zao hasa uanzishwaji wa vituo vya mafuta kwani walikuwa wanapata changamoto hasa maeneo ya kuweka vituo vya mafuta kwani kabla ya semina walifikiri kuwa vituo havitakiwi kuwekwa karibu na makazi ya wananchi.
Pongezi hizo zilitolwa baada ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godwini Samwel kutoa ufafanuzi kuwa hakuna sheria inayozuia kituo cha mafuta kujengwa karibu na makazi ya wananchi ispokuwa taratibu zote za usalama zikifuatwa. Pili alisema kuwa Vituo vya mafuta vinajengwa ili kuwahudumia wananchi kwahiyo ni bora vikawa karibu na wananchi ambao wanategemea kupata huduma hiyo.
Akifunga Semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera Oktoba 9, 2017 Afisa Biashara wa Mkoa wa Kagera Bw. Isaya tendega alitoa wito kwa wafanyabiashara wa Kagera kuhudhuria semina kama hizo zinzpoitishwa na kusisitiza kuwa zina manufaa makubwa katika uendsha ji wa biashara ya mafuta na zinawapunguzia faini wafanyabiashra zisizokuwa za lazima.
Aidha, Bw. Tendega aliwashauri wafanyabiashara waliohudhuria wanaporudi makazini kwao wawaelimishe waenzao kwa kuwapatia makabrasha waliopewa katika semina hiyo ili wayasome na kuzijua Sheria na kanuni za uendeshaji wa biashara za mafuta ili mkoa uwe na wafanyabiasha walio rasmi na kuondokana na biashara zisizorasmi.
Hadi sasa Mkoa wa Kagera una wafanyabiashara au wauzaji wa mafuta ambao ni rasmi wenye vituo 48 na wauzaji wasio rasmi 72. Jumla ya wafanya biashara ya mafuta yaani wauzaji ambao ni rasmi na wasiokuwa rami jumla ni 120.
Kati ya wadau waliopongezwa kwa kufuata sheria, Kanuni na taratibu za kuanziasha na kutoa huduma za biashara ya mafuta Mkoani Kagera ni Bw. Remigius Patrick (Maarufu kama Dk Remy) mwenye kituo cha Smart Oil Kibeta Manispaa ya Bukoba wafanyabiashara wameaswa kuiga mfano wake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa