- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezungumza na wananchi wa Kata ya Kamachumu na Kata ya Nshamba, Wilaya ya Muleba na kuwaelezea juu ya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo sekta ya afya, elimu, maji, barabara, kilimo, ufugaji zinazotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Akizungumza na wananchi hao ameeleza kuwa ziara zinazofanywa na Viongozi ni kwaajili ya kupita kukagua miradi ya maendeleo kuona kama fedha zinazoletwa zimefika na zimetekeleza miradi kwa viwango na ubora.
“Kazi kubwa imefanywa na Serikali kwa miongozo iliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili na nusu mambo mengi ya maendeleo yamefanywa,” ameeleza Mhe. Majaliwa
Akielezea sekta ya elimu amesema kuwa Mkoa wa Kagera ina msingi mzuri wa kielimu hivyo Serikali inachokifanya ni kuongeza miundombinu na kuboresha miundombinu iliyochakaa. Huku akiwataka watoto wote wa Kitanzania waende shule na kukemea vitendo vya watu wanaowakatisha masomo wanafunzi wa kike hali inayowapelekea watoto hao kuzimwa kwa ndoto zao.
Aidha, amewataka watumishi kuwa waadilifu, wazalendo kwa Nchi na kukemea vitendo vya wizi kwenye fedha za Serikali kwani Serikali inahitaji fedha zaidi ili kujenga miradi ya maendeleo ikiwemo mabweni ili watoto wa kike wasome shule za bweni na kufikia malengo yao.
Akieleza juu ya sekta ya afya, ameeleza kuwa kila mwezi Halmashauri ya Wilaya ya Muleba hupokea kiasi cha Tsh. milioni 70 kwa ajili ya kununua dawa hivyo hakuna uhaba wa madawa hospitalini.
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Mhe. Charles Mwijage na Mbunge wa Muleba Kusini Mhe. Dkt. Oscar Kikoyo kwa niaba ya wananchi wameishukuru Serikali kwa kuwaletea fedha kutekeleza miradi ya maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa