• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Agriculture

Katika msimu wa kilimo 2016/2017 Mkoa ulijiwekea lengo la kulima na kutunza jumla ya hekta 650,706 za mazao mbalimbali ya chakula zilizotarajiwa kuzalisha jumla ya tani 2,218,990  za ndizi, tani 413,049  za nafaka, tani 154,995 za mikunde na tani 1,166,268 za mazao ya mizizi.

Aidha, Mkoa ulilenga kulima na kupanda jumla ya hekta 62,079  za mazao mbalimbali ya biashara zilizokadiriwa kuzalisha tani 82,674 za kahawa maganda ,tani 337 za tumbaku, tani 1160 za pamba mbegu  na tani 4543 za majani mabichi  ya chai.

Hadi kufikia Juni, 2017 Mkoa ulikuwa umelima na kutunza jumla ya hekta 600,632 za mazao mbalimballi ya chakula na kuzalisha jumla ya tani 1,420,445 za ndizi, tani 115,200 za nafaka ambapo kati ya tani hizo zao la mahindi limechangia uzalishaji wa tani 109,440, tani 61,748  za  mikunde na tani  758,00 za mazao ya mizizi hata hivyo katika Mkoa wa Kagera kuna baadhi ya maeneo ya Wilaya uvunaji na uzalishaji wa mazao ya mizizi huwa ni endelevu kwa msimu wote wa mwaka

Mazao ya biashara, Mkoa umelima na kutunza  jumla ya hekta 50,581 za mazao mbalimbali ya biashara na  kuzalisha  tani 28,050 kahawa safi, tani 200 za tumbaku, tani 900 za pamba mbegu na  tani 1,500 za majani mabichi ya chai.

Katika mazao ya kipaumbele kitaifa Mkoa wa Kagera unazaliza mazao ya kahawa, chai, pamba na tumbaku. Kwa umuhimu wa mazao hayo uzalishaji ni kama ifuatavyo:

Mkoa wa Kagera ni moja ya Mikoa inayozalisha kwa wingi zao la kahawa hapa nchini ambapo wastani wa uzalishaji wa kahawa ya maganda kwa mwaka ni tani 50,000. Kutokana na takwimu za uzalishaji kahawa kitaifa, Mkoa wa Kagera unaongoza katika uzalishaji wa kahawa.

Zao la pili la biashara linalozalishwa Mkoani Kagera ni Chai inayolimwa katika Wilaya za Bukoba na Muleba. Wastani wa uzalishaji wa zao la chai kwa mwaka ni tani 1,000 hadi 1,500 kwenye eneo la hekta 1,132.

Zao la tatu ni pamba ambayo huzalishwa katika Wilaya za Biharamulo na Muleba. Wastani wa uzalishaji kwa mwaka ni tani 900 ambazo huzalishwa kwenye eneo la hekta 2,000. Idadi ya wakulima wanaojihusisha na kilimo cha pamba Mkoani Kagera ni takribani 5,700.

Zao la nne kwa umuhimu katika Mkoa wa Kagera ni Tumbaku ambayo huzalishwa katika wilaya ya Biharamulo kwenye eneo la hekta 237 na wastani wa mavuno kwa mwaka ni tani 230.

Mazao mengine ya biashara yanayolimwa Mkoani Kagera ni pamoja na vanilla na miwa. Wastani wa uzalishaji wa zao la vanilla ni tani 45 kwenye eneo la hekta 50 ambapo wakulima wanaojiuhusisha na kilimo cha vanilla ni takribani 6,000 wengi wao wakiwa chini ya usimamizi wa MAYAWA (Maendeleo ya Wakulima).

Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la kahawa iliyopitishwa na Kikao cha Wadau Mkoani ni kama ifuatvyo:-

  1. Kuongeza tija ya uzalishaji wa kahawa kutoka kilo 500 kwa hekta hadi kilo 2,000 kwa hekta za kahawa maganda kwa kuimarisha huduma za ugani, kuongeza na kuimarisha matumizi ya miche bora na pembejeo za kilimo na Kuimarisha udhibiti wa magendo ya kahawa.
  2. Kuongeza maeneo ya uzalishaji wa kahawa na kufufua mashamba yaliyokanda kwa muda mrefu.
  3. Kuimarisha uwezo wa vyama vya ushirika na usimamizi wa vyama vya ushirika ili viwe na uwezo wa kukusanya kahawa za wakulima na kuzitafutia soko la uhakika.
  4. Kuimarisha ushirikiano baina ya wakulima na sekta binafsi hususani wenye viwanda vya kahawa ili waweze kusaidia kutoa huduma muhimu kwa wakulima.

Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la chai:

  1. Kuhamasisha wananchi kuongeza uzalishaji wa chai kwa kufufua mashamba yaliyokanda.
  2. Kuimarisha utendaji wa kiwanda cha chai Kagera ili kiwe na uwezo wa kuwalipa wakulima kwa wakati kwa kutafuta mbia mwenye mtaji wa kutosha.
  3. Kuimarisha huduma za ugani katika kilimo cha chai.
  4. Kuimarisha bei ya majani ya chai ili kuvutia wakulima kuzalisha chai kwa wingi.
  5. Kuhakikisha chai inayozalishwa inaongezewa thamani ili mkulima aweze kupata bei ya soko tofauti na bei zinazopangwa na wadau kwa sasa.

Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la pamba:

  1. Kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za zao la pamba hususani mbegu, mbolea viuadudu na viuatilifu.
  2. Kuimarisha huduma za ugani kwa kuwajengea uwezo wataalamu wa kilimo ili waweze kutoa elimu sahihi kwa wakulima kupitia mashamba darasa.
  3. Kuhamasisha wakulima kujiunga katika vikundi na vyama vya msingi vya mazao ili iwe rahisi kufikiwa na huduma za mikopo na huduma nyingine za ugani.
  4. Kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi wa zao la pamba kupitia viongozi wa ngazi zote.

Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la tumbaku:

  1. Kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za zao la pamba hususani mbegu, mbolea viuadudu na viuatilifu kwa wakati.
  2. Kuimarisha huduma za ugani kwa kuwajengea uwezo wataalamu wa kilimo ili waweze kutoa elimu sahihi kwa wakulima kupitia mashamba darasa.
  3. Kuhamasisha wakulima kujiunga katika vikundi na vyama vya msingi vya mazao ili iwe rahisi kufikiwa na huduma za mikopo na huduma nyingine za ugani.
  4. Kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi wa zao la tumbaku kupitia viongozi wa ngazi zote.

 

 Hali ya Chakula

Mahitaji ya Chakula

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Mkoa wa Kagera una idadi ya wakazi wapatao 2,458,023 na wastani wa ongezeko la asilimia 3.1 linalopelekea idadi ya watu kufikia 2,762,818 hadi Desemba, 2016. Kwa uwiano wa mahitaji ya mtu mmoja kwa siku ambayo ni gramu ya utomwili na gram 650 za vyakula vya wanga, Mkoa wa Kagera unahitaji tani 655,479 ya vyakula vya wanga na tani 65,547 ya vyakula vya utomwili kwa mwaka.

 

Uhakika wa Chakula katika Mkoa wa Kagera

Hadi mwishoni mwa mwezi Juni, 2017 Wilaya zote zinazozalisha ndizi zilikuwa zimezalisha zaidi asilimia 64 ya lengo, sawa na tani 1,420,445 za ndizi ambazo ndiyo chakula kikuu kwa wananchi walio wengi katika Mkoa wa Kagera, hivyo kiasi hicho pamoja na mazao mengine yaliyozalishwa kipindi hicho kilitosheleza mahitaji kwa kipindi husika na hatukuwa na ziada ya kutosheleza kuuza maeneo mengine. Aidha Mazao mengine ya chakula kama vile Mihogo, Viazi na Magimbi yameendelea kuzalishwa katika kiwango cha wastani.

Upatikanaji wa Pembejeo bora za kilimo za Ruzuku

Wakulima wameweza kutumia pembejeo bora kama vile mbolea, dawa pamoja na mbegu bora zikiwemo za ruzuku na ambazo si za ruzuku.  Mkoa ulipokea pembejeo za ruzuku msimu wa mwaka 2016/2017 za aina mbili ambazo ni mbegu ya mahindi Kilogram 50,000 na mbole ya kukuzia Kilogram 100,000. Mbolea hizi zilishasambazwa katika Halmashauri tano zilizopo kwenye mpango wa ruzuku. Halmashuri hizo ni Biharamulo (Kg 10,000 mbegu na Kg 20,000 mbolea), Ngara (Kg 10,000 Mbegu na Kg 15,000 mbolea), Karagwe (Kg 12,500 mbegu na Kg 25,000 Mbolea), Missenyi (Kg 10,000 mbegu na Kg 20,000 Mbolea) na Kyerwa (Kg 7,500 Mbegu na Kg 20,000 mbolea).

Hatua Zinazochukuliwa na Mkoa Kuimarisha Sekta ya Kilimo

  1. Mkoa umeendelea Kuhimiza kilimo cha mazao yanayostahimili ukame na kukomaa kwa muda mfupi.
  2. Kwa kushirikiana na kituo cha Utafiti wa Kilimo Maruku Mkoa unaendelea kuzalisha na kusambaza mbegu kinzani za magonjwa ya kahawa na mihogo.
  3. Kuhamasisha usindikaji wa mazao mbalimbali ya kilimo.
  4. Maafisa ugani na watendaji wengine ngazi za vijiji na kata wamehimizwa kwenda mara kwa mara kutoa elimu kwa wakulima.
  5. Kuwahamasisha wakulima kujiunga katika vikundi/ vyama vya msingi vya mazao (AMCOS) na  vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) ili waweze kupata mtaji.

Katika kuendeleza Sekta ya kilimo, Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri imekuwa ikibuni Mipango mbalimbali ya Kisera na Kimkakati mfano maonesho ya kilimo (Nanenane) Kimkoa, Lengo likiwa ni kubadilisha kilimo kutoka kilimo cha mazoea na kukifanya kiwe kilimo cha kibiashara na endelevu kutokana na teknolojia mbalimbali wanazozipata kupitia maonesho hayo.


Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.