- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
CPA Pius Lazaro Mwakimenya
Mhasibu Mkuu wa Mkoa
MAJUKUMU YA KITENGO CHA FEDHA NA UHASIBU NA JINSI KINAVYOTEKELEZA MAJUKUMU YAKE
Kitengo cha Fedha na Uhasibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kinatekeleza Majukumu Makuu matano. Majukumu hayo matano yameainishwa na kufafanuliwa jinsi yanavyotekelezwa na Wataalam waliopo kwenye Kitengo cha Uhasibu na Fedha kama ifuatavyo:
Usimamizi wa Fedha:
Katika Usimamizi wa Fedha kitengo cha Fedha na Uhasibu kinawajibika kuandaa na kuidhinisha malipo mbalimba ya shughuli za kila siku za uendeshaji wa ofisi pamoja na shughuli za kutoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera. Aidha, kitengo hiki kinawajibika katika kuandaa na kuidhinisha malipo ya Mishahara ya Watumishi, kuwezesha makato mbalimbali yanayokubalika kisheria kutoka kwenye mishahara ya watumishi na kuyawasilisha kwenye mamlaka zinazohusika na makato hayo. Pia kutunza orodha na nyaraka za Watumishi wanaolipwa mishahara kwa ajili ya kumbukumbu za baadae.
Kuwezesha Malipo:
Katika Kitengo cha Fedha na Uhasibu tunawezesha malipo mbalimbali ya fedha kwa njia za kisasa ambazo ni za mtandao (yaani malipo yanafanyika kwa njia ya intaneti) ili kuondoa urasmu wa kuchelewesha malipo na kupelekea kukwamisha shughuli mbalimbali za Serikali, au kukwamisha malipo mbalimbali ya watumishi na malipo ya watoa huduma wanaotoa huduma mbalimbali katika Serikali. Pia Kitengo kinawajibika kutunza daftari la hesabu kwa ajili ya kumbukumbu za kimahesabu, Kupeleka benki fedha taslimu na hundi benki.
Hesabu za Mwisho wa Mwaka:
Kitengo cha Fedha na Uhasibu kinawajibika kutayarisha Makadirio ya Bajeti na kudhibiti matumizi ya fedha pia kuandaa taarifa ya matumizi ya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali. Kuandaa taarifa ya hesabu za mwisho wa mwaka na kuziwasilisha kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Aidha, Kujibu hoja zote za ukaguzi na maoni ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pale anapokuwa amefanya ukaguzi wa fedha katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Ukusanyaji Mapato:
Kitengo cha Fedha na Uhasibu pia kinawajibika katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Serikali kwa mujibu wa sheria na miongozo kwa baadhi ya mali za Serikali zinazosimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera na mali hizo ni nyumba zinazomilikiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.
Ukaguzi wa Awali:
Kitengo cha Fedha na Uhasibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kinatekekeleza majukumu yake kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na na miongozo ya fedha ambapo kabla ya malipo hufanyika uhakiki wa nyaraka za malipo kuona kama nyaraka hizo zimezingatia taratibu za malipo ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa. Aidha, kuhakikisha malipo yanayofanyika hayavuki bajeti ya kasma husika.
“Kagera: Kazi, Amani na Maendeleo”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.