- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
UTANGULIZI
Vijana nchini Tanzania fasili yake ni vijana wa kike na wa kiume kuanzia umri wa miaka 15 hadi 35.(sera ya taifa ya maendeleo ya vijana toleo la Desemba 2007, uk. 13)
Sensa ya watu na makazi 2012
Takwimu za sensa ya taifa ya watu na makazi ya mwaka 2012 zinaonyesha kwamba idadi ya vijana nchini Tanzania ni 15,587,621 sawa na asilimia 34.7 ya watanzania wote. Miongoni mwao vijana wa kiume ni 7,314,116 sawa na asilimia 33.4 ya vijana wote nchini na wa kike ni 8,273,505 sawa na asilimia 35.9 ya vijana wote nchini
Kagera
Idadi ya vijana mkoani kagera hufikia 793,756 (me 381, 514 na ke 412,242) sawa na asilimia 5.09 ya vijana wote nchini. Vijana wanaoishi vijijini ni 696,397( me 335,766 na ke 360,631) na mijini ni 97,359( me 45,748 na ke 51,611).Idadi ya vijana wa kike waliofikia umri wa uzazi (reproductive women ) wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 ni 412,242 sawa na asilimia 3.78 ya wanawake wote wenye sifa hiyo wanaokadiriwa kufikia 10,905,117 nchini.
Shughuli za kiuchumi
Vijana mkoani Kagera hujishughulisha na ujasiriamali katika maeneo yafuatayo
Kilimo: kahawa,migomba,maharage,mahindi,maghimbi.
Uvuvi: Samaki wa aina mbalimbali kama sangara,dagaa,sato n.k
Ufugaji: Nyuki,ngombe,samaki,kuku n.k.
Usafirishaji: Pikipiki (bodaboda)
Biashara ndogondogo
ufundi: (seremela,ushonaji,kompyuta,uashi)
Asasi zinazotoa huduma kwa vijana
Kuna asasi mbalimbali zinazotoa huduma kwa vijana na hivyo basi kuchangia katika utekelezaji wa sera ya taifa ya maendeleo ya vijana. Baadhi ya Asasi hizo ni kama WOSCA, WAMATA, WORLD VISION, TUMAINI LETU, KADETEF, VIMAKA, HDT, GCNT ,CODISO, SAPO, REDESO, CADA, TWESA, CARITAS,FAIDERS,ACORD,BODESA, TAHEA,TRCS,SHIDEPHA,ISHI TADEPA na MUVIKA.
Asasi hizi kwa ujumla hujishughulisha na kutoa elimu ya Afya,kilimo,ujasiriamali,ufugaji na stadi za maisha kwa vijana.
Mwenge wa uhuru
Mbio za mwenge wa uhuru zinazoratibiwa na idara ya vijana pia imekuwa ni njia muhimu na maalum ya kuelimisha na kuhamasisha vijana na jamii kushirikiana na serikali kwa njia ya kujitolea ili kujiletea maendeleo.
Mwenge wa uhuru hukimbizwa na vijana katika kila mkoa, halmashauri za wilaya na manispaa kote nchini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.