- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
LENGO LA KITENGO CHA TEHAMA
Kuwezesha utoaji wa ushauri wa kitaalam katika sekta za uchumi na uzalishaji kwenye Halmashauri
Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-
Kwa kuzingatia umuhimu wa TEHAMA na lengo la serikali la kuwa na serikali mtandao, Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa taasisi za serikali ambao unafanya vizuri katika eneo la TEHAMA.
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Mkoani Kagera ni ya kuridhisha kwa sasa.
Kampuni kongwe ya TTCL ndio inayotoa huduma za mawasiliano ya njia ya simu katika ofisi zote za serikali na mashirika Mkoani Kagera. Makampuni mengine ya simu za mkononi yametawanyika vizuri hadi katika baadhi ya vijiji na hivyo kufanya mawasiliano kuwa rahisi zaidi. Hali hiyo imewasaidia wakulima kujua bei halali ya soko la mjini kwa mazao yao na hivyo kuondoa adha ya kuibiwa na wafanyabiashara kwa kisingizio kuwa soko la bidhaa husika ni mbaya.
Mkoa una vituo viwili hadi sasa vinavyotoa huduma ya TEHAMA vijijini. Kituo kimoja kipo wilaya ya Bukoba vijijini katika kijiji cha Kibegwe kata ya Bugabo, na kingine kipo katika wilaya ya Ngara. Vituo hivyo vimekuwa vikitoa huduma nzuri kwa wanavijiji wa maeneo husika, ingawa vimekuwa havitoi huduma ipasavyo kutokana na mwamko duni wa wanavijiji katika matumizi ya TEHAMA.
Kutokana na mabadilko ya sera za habari na mawasiliano ambapo vituo binafsi vya radio vimeruhusiwa kuanzishwa, mkoa wa Kagera sasa una vituo vitano (5) vya radio. Vituo hivyo ni
Kasibante FM Redio iliyoko Bukoba
Radio Vision iliyoko Bukoba
Karagwe FM iliyoko Karagwe
Redio Fadeko iliyoko Karagwe
Radio Kwizera iliyoko Ngara
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imejenga miundombinu ya TEHAMA iliyo bora kwa ajili ya kuwa na serikali -mtandao .Aidha Ofisi nyingi hapa Mkoani hutumia teknolojia ya kompyuta katika kufanikisha shughuli za kila siku.
Hadi kufikia Septemba, 2013 mifumo mbalimbali ya kompyuta zaidi ya ishirini imefungwa katika Ofisi za serikali mkoani Kagera ili kurahisisha utendaji kazi wake. Ofisi moja ya mkuu wa wilaya ya Muleba imefungiwa miundombinu ya intaneti na hivyo kurahisisha mawasiliano kati ya Ofisi ya mkuu wa Mkoa na ofisi hizo. Aidha, mkoa unaendelea na juhudi za kuhakikisha kila Ofisi ya mkuu wa wilaya inafungiwa miundombinu ya intaneti ili kurahisisha mawasiliano.
Halmashauri za Ngara, Biharamulo, Kyerwa na Bukoba hazina miundombinu ya TEHAMA iliyo bora hadi sasa isipokuwa Manispaa ya Bukoba na halmashauri za Karagwe na Misenyi. Juhudi nyingi zinafanywa ili kujenga miundombinu hiyo kabla ya mwaka 2015 kwa lengo la kuharakisha lengo la serikali la kuwa na Serikali -Mtandao.
Huduma ya intaneti Mkoani Kagera hutolewa na makampuni mbalimbali. Kampuni kongwe ya TTCL ndiyo inayotoa huduma ya intaneti katika ofisi nyingi za serikali na mashirika. Aidha, makampuni ya simu za mikononi kama Vodacom, Tigo, Airtel na Zantel yanatoa huduma muhimu ya intaneti kupitia simu za mikononi na "moderm". Zipo pia baadhi ya ofisi ambazo hutumia makampuni mengine kwa ajili ya kupata intaneti. Makampuni hayo ni pamoja Simbanet ya jijini Dar es Salaam.
Mkongo wa Taifa ambao tayari umefika mkoani Kagera, umeweza kuongeza ufanisi wa huduma ya intaneti kwa kiwango kikubwa. Hadi sasa kampuni ya simu ya TTCL imeweza kutoa huduma bora zaidi za intaneti baada ya mkongo wa Taifa kuanza kufanya kazi hapa mkoani Kagera. Uwepo wa mkongo wa Taifa umepunguza gharama za intaneti katika ofisi za Serikali na pia umeongeza watumiaji wa intaneti katika Mkoa wa Kagera. Baadhi ya mabenki Mkoani Kagera, ofisi za TRA, Ofisi ya madini, NSSF zimeungwanishwa kwenye mkongo kupitia TTCL.
Hadi kufikia Septembal, 2013 ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera, Halmashauri za mkoa na manispaa ya Bukoba zimefungiwa mifumo ifuatayo;
Epicor--Mfumo huu hutumika katika kuandaa na kutoa malipo. Mfumo huu umesaidia sana na umepunguza hoja za ukaguzi kwa kiwango kikubwa. Mfumo huu umeunganishwa kwa kutumia mkongo wa Taifa.
SBAS--Huu ni mfumo kwa ajili ya kuandaa mipango ya serikali kuu.Bajeti ya Sekretariet ya Mkoa huandaliwa kwa kutumia mfumo huu.
PlanRep--Mfumo huu ni sawa na SBAS, tofauti ya mifumo hii miwili ni kuwa mfumo huu wa PlanRep hutumiwa na Halmashauri pamoja na Manispaa wakati wa kuandaa bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
CDR na CFR--Hii ni mifumo inayotumika kutolea taarifa za miradi ya maendeleo katika ngazi za Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
ETR--Huu ni mfumo unaotumika kutunza takwimu za wagonjwa wa kifua kikuu
LGHRIS-Mfumo huu unatumika katika kutunza taarifa za watumishi na unatumika katika ngazi ya mkoa na halmashauri.
Lawson-Huu ni mfumo unaotumika katika mishahara, kwa kutumia mfumo huu, serikali imeondoa tatizo la mishahara hewa, kuchelewa kwa stahili za watumishi n.k.
LGMD- Mfumo huu unatumika katika kukusanya na kutunza takwimu katika ngazi ya halmashauri. Takwimu hizi ndizo hutumika katika kuandaa mipango ya halmashauri.
MVC Database-Mfumo huu hutumika katika kutunza taarifa za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika ngazi ya halmashauri.
Aidha, ipo mifumo mingine ambayo si rahisi kuiweka hapa ambayo inapatikana katika baadhi ya halmashauri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.