- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
Upatikanaji wa Huduma ya Maji
Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama imeongezeka kutoka a 53% mwaka 2015 hadi kufikia 70% mwaka 2024. Kwa upande wa mjini, hali ya upatikanaji wa maji uko kati ya 82% hadi 95% inatofautiana kati ya mji mmoja na mwingine.
Miundombinu ya Maji
Kwa kipindi cha miaka minne (2020 hadi 2024) Serikali imetoa Tsh. 69,370,644,767.82 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji. Kwa upande wa vijijini, jumla ya vijiji 560 kati ya vijiji 651 vinayosimamiwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) vina miradi ya maji ya bomba inayohudumia wakazi wapatao 1,844,097 kati ya 2,634,423 sawa na 70. 00% ya wakazi wote wa Mkoa wa Kagera wanoishi maeneo ya vijijini. Pia jumla ya vijiji 91 bado havijajengewa miradi ya maji ya bomba. Katika mwaka wa fedha 2023/24 Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi katika vijiji 48. Kukamilika kwa miradi katika vijiji hivyo kutapelekea Mkoa kubakiwa na vijiji 43 ambavyo vitakua havina miradi ya maji ambavyo vimewekwa katika mpango wa mwaka wa fedha 2024/2025 kuchimbiwa visima vya maji. Aidha, juhudi mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa za kukarabati na kuboresha miradi chakavu.
Mpango wa utekelezaji wa Miradi ya Maji kwa mwaka wa fedha 2024/25
Mamlaka katika bajeti yake ya mwaka 2024/25 imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ya maji katika mkoa wa kagera yenye thamani ya TZS 19,731,806,440.71 miradi hiyo itatekelezwa kadri ya upatikanaji wa fedha kutoka Serikali Kuu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.