- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
Mkoa wa Kagera unakadiriwa kuwa na ng’ombe wapatao 550,070 wanaofugwa ambapo ng’ombe wa asili ni 528,632 na ng’ombe wa maziwa ni 21,438. Mbuzi wafugwao ni 593,607 ambapo mbuzi wa asili ni 583,202 na mbuzi wa maziwa ni 10,405. Wanyama wengine ni kondoo 53,061 na nguruwe 44,402.
Mazao ya mifugo
a) Maziwa
Mkoa unakadiriwa kuwa na ngo’ombe wa maziwa 21,169 na kwa mwaka 2014/2015 mkoa umeweza kupata maziwa lita 43,915,266 ukilinganisha na lita 14,870,268 kwa mwaka 2013/2014 ambapo kuna ongezeko la lita 29,044,998. Ng’ombe hawa wana uwezo wa kuzalisha maziwa wastani wa lita 5.6 kwa ngo’mbe mmoja kwa siku. Uhamasishaji wa unywaji wa maziwa unaendelea vizuri kwani hivi sasa kumekua na maduka maalumu ya uuzaji wa maziwa tayari kwa kunywa (Milk Bars) ambayo yanachangia kufanikiwa kwa biashara ya maziwa.
b) Mayai
Ufugaji wa kuku wa mayai kwa mkoa wa kagera unaendelea kuimarika ambapo kwa mwaka 2014/2015 jumla ya mayai 10,783,016 yaliripotiwa kukusanywa na thamani yake ni Tsh 2,804,476,900. Asilimia kubwa ya mayai haya hukusanywa kutoka kwa kuku wa kienyeji. Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa wafugaji wa kuku ili waweze kuongeza uzalishaji wa mayai na pia kupambana na magonjwa mbalimbali yanayoadhiri ndege hawa na kusababisha vifo. Kwa sasa ugonjwa unaosababisha vifo vingi vya kuku ni ugonjwa wa mdondo wa kuku. Hivyo wafugaji wanahaswa kuchanja kuku dhidi ya ugonjwa huu kwa wakati.
c) Ngozi
Mkoa wa Kagera umeendelea kuimarisha zao la ngozi kwa kuhimiza utunzaji wa ngozi inapokua kwa mnyama hai hadi pale inapovunwa kwa ajili ya kuuzwa kama zao la ngozi. Kwa mwaka 2014/2015 mkoa umekusanya jumla ya Ngozi za Ngo’mbe 23,288 na za mbuzi pamoja na kondoo 17,464. Uwekezaji katika viwanda vya usindikaji ngozi ni mdogo na hivyo kusababisha dhamani ya ngozi kushuka, hivyo sekta hii inahimiza na kukaribisha wawekezaji kujikita katika soko la ngozi kwani likitiliwa mkazo litawafaidisha wafugaji na wafanyabiashara wa zao la ngozi pamoja na taifa kwa ujumla.
Mkoa wa Kagera unaongoza kwa kuwa na huria nyingi za Taifa ambapo zipo huria 5 kati ya 10 zinazomilikiwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa (National Ranching Company Ltd – NARCO). Huria hizo ni Missenyi, Kitengule, Kikulula, Mabale na Kagoma. Eneo lote la huria mkoani lina ukubwa wa hekta. 135,802. Katika harakati za kuongeza uzalishaji wa mifugo na kuongeza ufanisi katika matumizi ya huria hizi, serikali iligawanya ranchi hizi katika vitalu na kukodisha kwa wawekezaji wakubwa na wadogo asilimia kubwa wakiwa ni Watanzania. Hivi sasa wawekezaji waliokodisha vitalu hivyo wanakadiriwa kuwa na jumla ya ng,ombe 25,748, mbuzi 2,1262 na kondoo 1,269. Huria hizi zimeajiri wafanyakazi 302 ambao wengi wao ni wachungaji. Hata hivyo wawekezaji hawa wamewekeza katika ujenzi wa miundombinu kama vile nyumba za wafanyakazi, ofisi, uchimbaji wa mabwawa, kujenga uzio na pia uchimbaji wa visima vya maji. Pia baadhi ya wawekezaji hawa wamenunua usafiri wa kazi kama vile magari (pick up), pikipiki, baiskeli na matrekta. Pamoja na hayo yote bado kuna changamoto ya uvamizi wa wananchi kuanzisha makazi katika vitalu vilivyokodishwa kwa wawekezaji hawa na kuzuia uwekezaji kufanyika kwa haraka zaidi. Hata hivyo Mkoa unaendelea kutatua migogoro inayokwamisha maendeleo ya sekta ya mifugo ili wananchi wa Kagera waweze kufaidi matunda ya ranchi hizi.
Miundombinu na huduma za sekta ya mifugo
Miradi inayotekelezwa chini ya Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (District Agricultural Development Plans –DADPs) inasaidia kwa kiasi kikubwa katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya mifugo. Hivi sasa Mkoa una jumla ya majosho 63 kati ya 118 sawa na asilimia 53% ambayo yanafanya kazi na juhudi za kufanya ukarabati wa majosho mengine zinaendelea. Hali ya uogeshaji mifugo imeendelea kuimarika na hivyo kupunguza magonjwa yanayoenezwa na kupe.
Mkoa una jumla ya minada ya mifugo kumi na minne(14) ambapo ya Awali ni 10, la upili moja na Minada ya Mipakani mitatu (3).
Minada ya Awali inasimamiwa na Halmashauri za Wilaya na ni chanzo cha mapato ya Halmashauri. Minada ya Upili na Mipakani ni minada inayosimamiwa na Serikali Kuu. Pia kuna malambo kumi na saba, machinjio hamsini na tano (55) ambapo mkubwa ni mmoja uliopo katika Manispaa ya bukoba.
Miundombinu ya mifugo:
WILAYA
|
Majosho
|
Wataalamu wa mifugo.
|
|||||||
idadi
|
Yanayofanya kazi
|
Yasiyofanya kazi
|
Ofisi za uuguzi
|
Daktari wa mifugo
|
Maafisa mifugo
|
Maafisa ugani
|
Afisa ndorobo
|
Liv. Field Auxiliary
|
|
Ras Kagera
|
0
|
0
|
0
|
0
|
1
|
2
|
0
|
0
|
0
|
Muleba
|
27
|
24
|
3
|
1
|
1
|
0
|
21
|
1
|
1
|
Karagwe
|
17
|
1
|
16
|
1
|
0
|
2
|
18
|
1
|
1
|
Biharamulo
|
5
|
2
|
3
|
1
|
1
|
1
|
12
|
0
|
0
|
kyerwa
|
6
|
0
|
6
|
1
|
1
|
2
|
14
|
0
|
1
|
Bukoba manispaa
|
0
|
0
|
0
|
0
|
0
|
0
|
6
|
0
|
1
|
Bukoba vijijini
|
24
|
16
|
8
|
1
|
2
|
1
|
27
|
0
|
0
|
Misenyi
|
19
|
7
|
12
|
2
|
1
|
1
|
17
|
0
|
0
|
Ngara
|
20
|
13
|
7
|
1
|
1
|
0
|
14
|
2
|
2
|
Jumla
|
118
|
63
|
55
|
8
|
8
|
9
|
129
|
4
|
6
|
Huduma nyingine za Mifugo
WILAYA
|
Masoko ya mifugo
|
Malambo
|
machinjio
|
Mabanda ya ngozi
|
Maduka ya dawa
|
Kliniki za mifugo
|
Muleba
|
2
|
0
|
10
|
10
|
7
|
7
|
Karagwe
|
3
|
2
|
10
|
10
|
13
|
13
|
Biharamulo
|
2
|
8
|
10
|
3
|
3
|
3
|
kyerwa
|
1
|
0
|
3
|
3
|
3
|
3
|
Bukoba manispaa
|
0
|
0
|
1
|
1
|
2
|
4
|
Bukoba vijijini
|
1
|
3
|
7
|
2
|
4
|
12
|
Misenyi
|
2
|
4
|
5
|
6
|
4
|
6
|
Ngara
|
3
|
0
|
9
|
5
|
6
|
5
|
Jumla
|
14
|
17
|
55
|
40
|
42
|
53
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.