- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
|
|
|
|
Mhe.Julius Laizer Kalanga
|
|
|
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe
|
|
HISTORIA YA WILAYA YA KARAGWE |
CHIMBUKO LA KARAGWE NA WATU WAKE (WANYAMBO)
|
Jina " Karagwe " kutokana na simulizi za wazee wetu mbali mbali na watafiti wa historia ya Karagwe kama ( Katoke 1975; 162) inaelezwa kwamba jina hili linatokana na kilima kinachopatikana Kusini Magharibi ya Makao makuu ya wilaya ya Karagwe ,kwenye kijiji cha Kandegesho ,kata ya Nyakakika ambacho mtawala (Omukama) wa kwanza alifanya kafara ya kwanza. Taarifa zilizopo mtawala huyo alijulikana kwa jina la Nono ya Malija kutoka ukoo wa Basiita. Na kwamba kumbukumbu hii ya "Karagwe ka Nono "inatokana na ukweli kuwa Nono alikuwa mtawala wa mwisho wa wenyeji asilia kabla ya kuondolewa madarakani na Omukama Ruhinda mtoto wa Wamara. Inasemekana kwamba Nono aliondolewa kwa ujanja bila ya misukosuko wala mapigano ya aina yoyote. Kwa kifupi hii ndio kumbukumbu yake na chimbuko la historia ya jina Karagwe.
MIPAKA YA WILAYA
|
Wilaya ya Karagwe ni kati ya Wilaya saba (7) za Mkoa wa Kagera. Wilaya inapakana na Wilaya ya Kyerwa upande wa Kaskazini, Nchi ya Rwanda upande wa Kusini Magharibi, Wilaya ya Ngara upande wa Kusini na Wilaya za Missenyi, Bukoba Vijijini na Muleba upande wa Mashariki.
JIOGRAFIA YA WILAYA
|
Wilaya ipo kilomita 115 kutoka Manispaa ya Bukoba –Makao makuu ya Mkoa wa Kagera. Wilaya inapatikana kati ya nyuzi 1o na 2o, 20' Kusini Latitudo 30o hadi 38,30 Mashariki Longitudo. Mwinuko wa ardhi kutoka usawa wa bahari ni mita 1,500 hadi mita 1,800. Hali ya hewa kwa ujumla ni joto la wastani wa degree 26oC. Mvua zinanyesha kwa wastani wa mm 1,040 hadi 1,200 kwa mwaka, kati ya mwezi Septemba na Januari na kati ya mwezi Machi na mwezi Mei.
ENEO LA WILAYA
|
Wilaya ya Karagwe ina eneo la kilomita za mraba 4,500 kati ya hizo kilomita za mraba 4,342 ni eneo la nchi kavu na kilomita za mraba 158 ni eneo la maji. Eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 153,540 na eneo linalolimwa ni Hekta 82,808.5 sawa na asilimia 53.9.
UTAWALA
|
Maeneo ya Utawala yamebadilika kutoka Tarafa 4, Kata 28, Vijiji 109 na Vitongoji 1,162 mwaka 2005 hadi Tarafa 5, Kata 23, Vijiji 77 na Vitongoji 629 mwaka 2014. Vitongoji 594 vipo katika Halmashauri ya Wilaya na vitongoji 35 vipo katika Mamlaka ya mji mdogo. Waheshimiwa Madiwani wa kuchaguliwa wapo 23 na Waheshimiwa Madiwani Wanawake Viti maalum 7.
IDADI YA WATU
|
Kulingana na Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ya Karagwe ilikuwa na jumla ya watu wapato 332, 020. Kati ya hao 163,864 (wanaume) na 168,156 (wanawake), ambapo ongezeko la watu ni asilimia 2.9 kwa mwaka.
Maoteo ya watu kwa mwaka 2015 ni kuwa Wilaya ilikuwa na watu 351,555. Kati ya hao, wanawake ni 178,050 na wanaume ni 173,505. Aidha idadi ya kaya nayo imeongezeka toka kaya 72,836 mwaka 2012 hadi kaya 76,425 mwaka 2015.
ORODHA YA WAKUU WA WILAYA YA KARAGWE TANGU MWAKA 1961 HADI SASA |
NA.
|
JINA KAMILI
|
MWAKA WA KUINGIA |
MWAKA WA KUTOKA |
22.
|
NDG. JULIUS LAIZER KALANGA |
2023
|
-
|
21.
|
NDG. JULIETH NKEMBANYI BINYURA |
2021
|
2023
|
20. |
NDG. GODFREY A. MHELUKA
|
2016 |
2021 |
19. |
NDG. DEODATUS L. KINAWILO
|
2015 |
2016 |
18. |
NDG. DARRY I. RWEGASIRA
|
2012 |
2015 |
17. |
NDG. ISSA S NJIKU (AG)
|
2011 |
2012 |
16. |
NDG. FABIAN I. MASSAWE
|
2009 |
2011 |
15. |
NDG. FRANK UHAHULA
|
2006 |
2009 |
14. |
NDG. DAVID J. DAUD
|
2004 |
2004 |
13. |
NDG. SANING’O OLE TELELE
|
2000 |
2004 |
12. |
NDG. PETER KANGWA
|
1999 |
2000 |
11. |
NDG. GERARD J. GHACHOCHA
|
1997 |
1999 |
10. |
NDG. JOSEPH E. NDITI
|
1994 |
1997 |
09. |
NDG. LUHOZYO E. SIWALE
|
1989 |
1994 |
08. |
NDG. MOHAMED CHIMSALA
|
1984 |
1989 |
07. |
NDG. RAPHAEL CHAYAKO
|
1980 |
1984 |
06. |
NDG. F.X. ITALA
|
1978 |
1980 |
05. |
NDG. RUHASI
|
1977 |
1978 |
04. |
NDG. THOMAS MSONGE
|
1973 |
1977 |
03. |
NDG. LOSA LIYEMBA
|
1969 |
1973 |
02. |
NDG.ENOS RYANGARO
|
1965 |
1969 |
01. |
NDG. PETER N. KAFANABO
|
1961 |
1963 |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.