- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
MAENDELEO YA MICHEZO MKOA WA KAGERA
UTANGULIZI
Michezo ni kielelezo na utambulisho wa Utamaduni wa mtu, watu, jamii au Taifa; michezo ni chombo kinachokuza ustawi wa maendeleo ya jami,kujenga utimamu wa akili na mwili. Kutokana na umuhimu huo michezo na Utamaduni vimepitia katika hatua mbalimbali za mabadiliko yakiwemo ya kisayansi na kiteknolojia mfano watanzania wanashirikisha katika michezo ya jadi iikiwemo bao, kulenga shabaha na mishale. Baada ya ukoloni michezo michezo mipya ilitambulishwa ikiwemo mpira wa miguu, netiboli, ngumi, mpira wa meza na mpira wa mikono michezo hii ilienea Tanzania na duniani kote ikitambulika kama michezo ya ridhaa (Sports Ameuture) ambapo hivi leo michezo ni ajira na ni biashara duniani nzima.
HALI MAENDELEO YA MICHEZO MKOA WA KAGERA;
Mkoa una kiwanja kikuu cha mpira wa miguu cha kisasa cha Kaitaba kilichopo mjini (Artificial glasses play ground pitch) ambacho kilijengwa kwa ufadhili wa FIFA. Aidha, Mkoa una kiwanja dada cha Halmashauri ya Wilaya ya Muleba. Halmashauri za Wilaya zimetenga maeneo wazi “Open spaces and recreation” kwa ajili ya maendeleo ya michezo kwa lengo la ubuaji vipaji.
TAKWIMU ZA KIMAENDELEO TASNIA YA MICHEZO MKOA KAGERA
S/N
|
ENEO LA MAENDELEO
|
JUMLA |
||
1.
|
VYAMA
|
VILIVYOSAJILIWA
|
69 |
69 |
VISIVYO NA USAJILI
|
11 |
11 |
||
2.
|
WAAMUZI (REFEREES)
|
DARAJA LA IV
|
52 |
52 |
DARAJA III
|
61 |
61 |
||
DARAJA LA I
|
4 |
4 |
||
3.
|
MAKOCHA
|
DARAJA LA IV
|
48 |
48 |
DARAJA LA III
|
148 |
148 |
||
DARAJA LA I
|
2 |
2 |
||
4.
|
VILABU
|
DARAJA LA IV
|
82 |
82 |
DARAJA LA III
|
18 |
18 |
||
LIGI KUU I
|
1 |
1 |
||
5.
|
VIWANJA
|
VIKUU (STANDARDs)
|
2 |
2 |
VYA SHULE NA VYUO
|
826 |
826 |
||
MAFUNZO YA MUDA MREFU - DIPLOMA
|
6 |
6 |
||
MSINGI/SEKONDARI
|
505 |
505 |
USHIRIKI KATIKA MASHINDANO YANAYOANDALIWA NA VYAMA VYA MICHEZO NCHINI;-
Mkoa wa Kagera unashiriki kwenye ligi kuu ya soka (TPL) ambapo timu ya Kagera Sugar Football Club inashiriki ligi hiyo kwa mafanikio sanjari na timu za mpira wa wavu, netiboli na ngumu zimekuwa zikiuwakilisha mkoa vema. Aidha, kwa upande wa waamuzi mkoa unawakilishwa vema na Jonesia Rukyaa mwamuzi wa ligi kuu ya Tanzania ambaye anatambuliwa na TFF, CAF na FIFA.
MAENDELEO YA MICHEZO KATIKA TAASISI ZA SERIKALI;-
Katika mashindano ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Shule za Sekondari (UMISSETA) mkoa umekuwa ukifanya vizuri kwa kupeleka idadi kubwa ya wanamichezo wanaounda timu ya Mkoa na hatimaye kuchaguliwa katika timu za Taifa kwenye mashindano mbalimbali. Aidha, katika mwaka 2019 Mwanafunzi Kassim Ibrahim aliibuka kuwa mfungaji bora kwa Afrika mashariki kwenye mashindano ya shule za Sekondari yaliyofanyika mkoani Arusha.
MCHANGO WA MICHEZO KATIKA USTAWI WA JAMII, AFYA NA NGUVU KAZI YA TAIFA.
Ili kutoa mchango wenye tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla mkoa una programu ya kudumu ya mazoezi kwa afya kwa wananchi na watumishi wa umma ambayo hufanyika kila siku ya jumamosi yakihusisha mamlaka zote za Sekali za Mitaa, Taasisi, Idara na watu binafsi. Mazoezi yanalenga kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza (kisukari, shinikizo la Damu). Kutoa mafunzo ya namna bora ya kujikinga na magonjwa nyemelezi na ulaji sahihi na bora kwa wananchi ili hatimaye kupunguza vifo kwa wananchi na kuipunguzia gharama Serikali katika kutibu magonjwa yanayotibika kupitia mazoezi.
MIKAKATI YA KUINUA NA KUENDELEZA MICHEZO MKOA KAGERA MWAKA, 2020
Kuwepo kwa programu ya mafunzo ya michezo kwa walimu wa michezo mbalimbali.
Kuwepo kwa programu ya michezo kwa watumishi wa Serikali kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa kila mwisho wa mwaka
Kuanzisha vilabu vya mozezi mepesi (Jogging clubs, beach Clubs n.k)
Kuendelea kuwahamasisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kupeleka walimu wa michezo katika mafunzo ya muda mrefu na mfupi katika vyuo vya maendeleo ya michezo nchini.
Kuhamasisha taasisi na Idara za Serikali kushiriki katika michezo.
Kuandaa mabonanza yanayoshirikisha mikoa jirani na mikoa ya iliyopo katika nchi jirani
Kusudio la vituo vya michezo kwenye shule za msingi na sekondari
Ngoma za asili za kabila la Wahaya hazijasahaulika sana, vikundi mbalimbali vya ngoma kama vile Lugoloile, Zikolwe Engozi, Mikoni pamoja na Kikundi cha Muziki wa Dansi - KAKAU BENDI.
HALI YA MAENDELEO YA USTAWI WA UTAMADUNI KATIKA MKOA;
Mkoa una maeneo mbalimbali ya Makumbusho pamoja na Vivutio vya Utalii kwa ajili ya kuhifadhia mila na Utamaduni wa Mkoa huu pamoja na kusaidia ukuaji wa uchumi ambapo maeneo hayo ni yanavyooneka kwenye jedwali hapa chini;
TAKWIMU ZA VIVUTIO VYA UTALII KATIKA MKOA WA KAGERA;-
S/N
|
ENEO
|
SHUGHULI
|
MAHALI LILIPO
|
1.
|
Katuruka
|
Uhunzi na Ufuaji wa Vyuma
|
Bukoba (V)
|
2.
|
Bwanjai
|
Mapango na Maandishi ya Watu wa kale
|
Missenyi
|
3.
|
Kanazi
|
Jengo la Makumbusho
|
Bukoba (V)
|
4.
|
Radio Tower
|
Makumbusho ya Wajerumani
|
Ujirani mwema - Bukoba
|
5.
|
Germany Cemetries
|
Makaburi ya Wajerumani
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- Kagera
|
6.
|
Kiroyera Tours
|
Makumbusho pamoja na Utalii
|
Bukoba (M)
|
7.
|
Germany Building
|
Duka la Bishara
|
Bukoba (M)
|
8.
|
Nyumba ya Msonge
|
Makumbusho ya Watu wa Kale
|
Muleba
|
Mkoa una jumla ya vikundi vya sanaa na utamaduni thelathini na tatu (35) vikihusisha Muziki wa Asili “AKASIMBO” na “AMAYAGA’ pamoja na Bendi ya Muziki wa Dansi ya Kakau Bendi iliyopo Manispaa ya Bukoba pamoja na vikundi mbalimbali vya filamu na maigizo pamoja na vichekesho;-
HALI YA VIVUTIO VYA UTALII KATIKA MKOA;
Mkoa unavivutio mbalimbali vya Utalii kama inavyoonekana hapa chini
CHANGAMOTO ZA SEKTA YA UTAMADINI NA MICHEZO KATIKA MKOA
Jamii kuiga tamaduni za nje pamoja na kutofanya utalii kwenye vivutio kwa ajili ya kujifunza na kukuza uchumi wa Mkoa.
Vyama vya michezo kukosa udhamini wa programu na mashindano ya michezo mbalimbali.
Ukosefu wa Wataalamu wa mambo ya kale unaotokana na vifo na waliopo kutotembelea Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kutoa Ushauri wa namna ya uhifadhi mambo ya kale kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Wizi wa makusudi wa kazi za Wasanii unaotokana na kukuwa kwa kasi kwa Teknolojia ya Habari na mawasiliano duniani.
Uvamizi wa maeneo wazi ya viwanja vya Michezo na kutumika katika shughuli nyingine.
Vyama vya michezo kushindwa kujiendesha kutokana na ukosefu wa fedha
‘‘KAGERA, KAZI AMANI NA MAENDELEO“
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.