- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
SEKTA YA KILIMO |
Utekelezaji wa Malengo ya Kilimo Msimuwa Mwaka 2017/2018 |
Katika msimu wa kilimo 2017/2018 Mkoa ulijiwekea lengo la kulima na kutunza jumla ya hekta 679,393 za mazao mbalimbali ya chakula zilizotarajiwa kuzalisha jumla ya tani 2,592,695 za ndizi, tani 360,729 za nafaka, tani 170,053 za mikunde na tani 1,042,326 za mazao ya mizizi.
Aidha, Mkoa ulilenga kulima na kutunza eneo la hekta 92,081.5 za mazao mbalimbali ya biashara linalotarajiwa kuzalisha, tani 81,994 za kahawa maganda, tani 4,488.9 za pamba mbegu, tani 383 za tumbaku, tani 3,645 za majani mabichi ya chai.
Hadi kufikia Mwezi Juni, 2018 Mkoa ulikuwa umelima na kutunza jumla ya hekta 673,974 za mazao mbalimbali ya chakula na kuzalisha jumla ya tani 2,379,901 za ndizi, tani 285,595 za nafaka, kati ya tani hizi, zao la mahindi limechangia uzalishaji wa tani 243,287, tani 122,406 za mikunde, aidha, zaidi ya tani 1,095,347 za mizizi zimezalishwa kati ya tani hizi, zao la mhogo limechangia uzalishaji wa tani 818,742.
Hata hivyo, uzalishaji wa mazao ya mizizi katika Mkoa wa Kagera kwenye Halmashauri zake ni endelevu kwa msimu wote wa Vuli (Septemba –Desemba) na Masika (Machi –Mei).
Mazao ya biashara, Mkoa umelima na kutunza jumla ya hekta 129,151 za mazao mbalimbali ya biashara na kuzalisha tani 156.5 za tumbaku, tani 2,249.983 za majani mabichi ya chai, zao la kahawa na pamba bado yanaendelea kuvunwa.
Katika mazao ya kipaumbele kitaifa Mkoa wa Kagera unazalisha mazao ya kahawa, chai, pamba na tumbaku.
Mkoa wa Kagera ni moja ya Mikoa inayozalisha kwa wingi zao la kahawa hapa nchini ambapo wastani wa uzalishaji wa kahawa ya maganda kwa mwaka ni tani 50,000. Kutokana na takwimu za uzalishaji kahawa kitaifa, Mkoa wa Kagera unaongoza katika uzalishaji wa kahawa.
Zao la pili la biashara linalozalishwa Mkoani Kagera ni Chai inayolimwa katika Wilaya za Bukoba na Muleba. Wastani wa uzalishaji wa zao la chai kwa mwaka ni tani 1,000 hadi 1,500 kwenye eneo la hekta 1,132.
Zao la tatu ni pamba ambayo huzalishwa katika Wilaya za Biharamulo na Muleba. Wastani wa uzalishaji kwa mwaka ni tani 900 ambazo huzalishwa kwenye eneo la hekta 2,000. Idadi ya wakulima wanaojihusisha na kilimo cha pamba Mkoani Kagera ni takribani 5,700.
Zao la nne kwa umuhimu katika Mkoa wa Kagera ni Tumbaku ambayo huzalishwa katika wilaya ya Biharamulo kwenye eneo la hekta 237 na wastani wa mavuno kwa mwaka ni tani 230.
Mazao mengine ya biashara yanayolimwa Mkoani Kagera ni pamoja na vanilla na miwa. Wastani wa uzalishaji wa zao la vanilla ni tani 45 kwenye eneo la hekta 50 ambapo wakulima wanaojiuhusisha na kilimo cha vanilla ni takribani 6,000 wengi wao wakiwa chini ya usimamizi wa MAYAWA (Maendeleo ya Wakulima).
Mikakati ya Mkoa ya Kuendeleza zao la Kahawa Iliyopitishwa na Kikao cha Wadau Mkoani ni Kama Ifuatvyo:- |
Kuongeza tija ya uzalishaji wa kahawa kutoka kilo 500 kwa hekta hadi kilo 2,000 kwa hekta za kahawa maganda kwa kuimarisha huduma za ugani, kuongeza na kuimarisha matumizi ya miche bora na pembejeo za kilimo na Kuimarisha udhibiti wa magendo ya kahawa.
Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la chai: |
Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la pamba: |
Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la tumbaku: |
HALI YA CHAKULA |
Mahitaji ya Chakula |
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Mkoa wa Kagera ulikuwa na Idadi ya wakazi wapatao 2,458,023. Ongezeko la watu kwa mwaka limepanda hadi kufikia wastani wa asilimia 3.2 kutoka wastani wa 3.1 mwaka 2002. Makadirio ya mwaka 2017 Mkoa wa Kagera una idadi ya watu 2,879,231. Kwa uwiano wa mahitaji ya mtu mmoja kwa siku ambayo ni gramu 65 ya utomwili na gram 650 za vyakula vya wanga, Mkoa wa Kagera unahitaji tani 655,479 ya vyakula vya wanga na tani 65,547 ya vyakula vya utomwili kwa mwaka.
Uhakika wa Chakula Katika Mkoa wa Kagera |
Hadi mwishoni mwa mwezi Juni, 2018 Wilaya zote zinazozalisha ndizi zilikuwa zimezalisha asilimia 92 ya lengo, sawa na tani 2,379,901 za ndizi ambazo ndiyo chakula kikuu kwa wananchi walio wengi katika Mkoa wa Kagera, hivyo kiasi hicho kinatosheleza mahitaji kwa kipindi husika na hata kuweza kuuzwa katika Mikoa ya jirani na nchi jirani.
Ugavi wa mazao mbalimbali kama ya nafaka, mizizi na mikunde ni mzuri kwenye masoko ya vijijini na mjini kwa mwaka 2017/2018 na bei za mazao hayo zimekuwa za wastani, mfano wastani wa kilo moja ya mahindi kwasasa ni Tsh 350-550/= na ndizi mbichi kwa kilo tsh 500-1000/=. Vyakula aina ya mizizi (muhogo, na viazi) vinaendelea kuvunwa na kuimarisha hali ya upatikanaji wa chakula katika ngazi ya Kaya.
Hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa ili kuimarisha usalama wa chakula katika Mkoa wa Kagera. Hatua hizo ni pamoja na Kuhamasisha matumizi ya maghala ya kuhifadhia chakula, kuendelea kutoa elimu ya hifadhi ya vyakula kwa kutumia mifuko ya PICs, kuhamasisha wakulima kupanda mazao ya muda mfupi ikiwa ni pamoja na kusisitiza Matumizi ya mbolea na mbegu bora na za muda mfupi ambazo zinastahimili mvua chache na magonjwa kwa kushirikiana na Kituo cha utafiti Maruku. Kuwahamasisha wakulima kujiunga katika vikundi/ vyama vya msingi vya mazao (AMCOS) na vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) ili waweze kupata mtaji.
Aidha, Katika kuendeleza Sekta ya kilimo, Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri imekuwa ikibuni Mipango mbalimbali ya Kisera na Kimkakati mfano Maonesho ya kilimo (Nanenane) Kimkoa, Lengo likiwa ni kubadilisha kilimo kutoka kilimo cha mazoea na kukifanya kiwe kilimo cha kibiashara na endelevu kutokana na teknolojia sahihi na mbalimbali wanazozipata kupitia maonesho hayo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.