- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
|
Serikali Mkoani Kagera imeendelea kutoa kipaumbele katika huduma za afya zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha afya zao. Serikali ya Mkoa inatambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi wake kwani afya bora ni raslimali muhimu kwa maendeleo. Maendeleo ya Mkoa wetu wa Kagera yataletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali.
Katika kuhakikisha kuwa wananchi wa Kagera wana afya bora, Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa huduma za afya kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo. Sera ya Taifa ambayo imeendelea kutumika katika kuelekeza utoaji wa huduma za afya mkoani Kagera ilipitishwa mwaka 1990. Tangu sera hiyo ilipopitishwa, yamekuwepo mabadiliko mbalimbali ya Kiuchumi na Kijamii, mabadiliko ya Sayansi na Technolojia na kuongezeka kwamagonjwa. Yametokea pia, maelekezo mbalimbali ya Serikali. |
Mabadiliko na maelekezo yote haya yanatoa changamoto mpya katika utoaji wa huduma za afya na yamechangia kwa pamoja kuifanya sera iliyopitishwa mwaka 1990 kutokidhi mahitaji na matarajio ya sasa na ya miaka ijayo.
|
Mfumo na utaratibu wa utoaji huduma unaotumika hivi sasa umebadilika kutokana na mabadiliko yaliyotokea, ikilinganishwa na mfumo uliokuwa unatumika kwa maelekezo ya Sera ya 1990. Mwaka 1996 marekebisho ya sera yalipitishwa kwa lengo la kuanzisha mfumo mpya wa utoaji na uendeshaji wa Huduma za Afya katika ngazi ya Wilaya. Katika marekebisho haya, ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa afya ulitambuliwa na kupewa msukumo, pia yalikasimu usimamizi wa utekelezaji katika mamlaka za Serikali za Mitaa na hivyo kuongeza ushiriki wa wananchi katika kusimamia na kumiliki raslimali za afya.
Mabadiliko haya yamelazimu kufanyia mapitio Sera ya mwaka 1990, na yamezingatia Sera na mikakati mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Sera na mikakati hiyo ni pamoja na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA).
Sera ya afya ya mwaka 1990 iliyopitiwa mwaka 2007, imeweka bayana dira, makusudio, maelekezo ya Serikali katika mfumo wa matamko, mabadiliko ya kiuchumi na kijamii, matokeo ya tafiti na majaribio na uzoefu katika utoaji wa huduma. Aidha, utayarishaji wa sera hii umekuwa shirikishi kwa Wizara kuwashirikisha wadau mbalimbali wanaotoa na kutumia huduma za afya katika kupitia Sera ya 1990.
Jukumu la wadau wote wa Sekta ya Afya ni kusoma, kuielewa na kutafsiri matamko yaliyomo katika sera hii wakati wa kupanga, kutoa na kutathmini Huduma za Afya nchini.
Wizara inatoa shukrani kwa wadau wote walioshiriki kutoa maoni yao na hivyo kukamilisha Sera hii. Nina imani kuwa wadau katika ngazi zote watashiriki kikamilifu katika kutekeleza Sera hii kwa lengo la kuboresha huduma za afya kote nchini.
LENGO LA HUDUMA ZA AFYA MKOANI KAGERA |
Lengo la Huduma za Afya Mkoani Kagera ni kuwezesha utoaji wa Afya ya Kinga, Tiba, Maendeleo ya Afya na Ustawi wa Jamii kwenye Mkoa. Aidha, Mkoa unafanya kazi ya kuratibu na kushauri juu utekelezaji wa Sera ya Afya kwenye Mkoa kamailivyofafanuliwa hapo juu.
Pili ni kufuatilia na kusimamia watoa huduma za afya zinazotolewa na Serikali na Sekta binafsi ambapo Mkoa wa Kagera unatoa Huduma za Afya katika Vituo vya kutolea Huduma 291. Zahanati zikiwa 246, Vituo vya Afya 31, na Hospitali 14. Tatu, ni kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utoaji wa Huduma za Afya kwa Wananchi. Nne, ni Kutoa msaada wa kitaalam kipindi cha milipuko ya magonjwa. Mwisho ni kutoa ushauri wa kitaalam katika mipango ya kukabiliana na Ugonjwa wa UKIMWI kwenye Mkoa.
|
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa