- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MAENDELEO YA JAMII
Lengo kuu la sekta ya Maendeleo ya Jamii ni kuchukua hatua zinazowawezesha watu kutambua uwezo walio nao wa kubaini matatizo na uwezo wao wa kutumia raslimali zilizopo kujitatulia matatizo hayo, kujipatia na kujiongezea kipato na kujiletea maisha bora zaidi na hivyo kujiletea maendeleo, na kuweka mazingira muafaka yatakayo wawezesha wanawake na wanaume kutekeleza majukumu yao katika jamii kwa kuzingatia mahitaji ya kijinsia. Aidha lengo jingine ni kuongeza ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika shughuli za maendeleo, hatimaye kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.
Kazi zinazotekelezwa na sekta ya Maendeleo ya Jamii katika mkoa wa Kagera ni pamoja na:-
• Kujenga uelewa wa wananchi ili aweze kushiriki shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo yao kwa njia ya kujitegemea na kuwasaidia kupanga mipango inayotekelezeka.
• Kuhamasisha wananchi kujiunga katika vikundi vya kijamii na SACCOS ili kuanzisha na kutekeleza shughuli za uzalishaji mali zenye kuchangia kuinua hali zao za maisha, pamoja na utoaji wa mikopo ya kiuchmi kwa wananwake kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii wa wanawake.
• Kushirikisha jamii katika mapambano dhidi ya janga la UKIMWI na kutoa msaada kwa watoto yatima.
• Kusaidia jamii jinsi ya kuondokana na mila potofu zinazochangia kuzorotesha maendeleo ya wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa