- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Hadi kufikia tarehe 31 Julai, 2018 Mkoa wa Kagera unao jumla ya Maafisa Ushirika 15 wanaotekeleza shughuli za sekta ya Ushirika. Idadi ya watumishi hawa ni ndogo ukilinganisha na Idadi ya Vyama 689 vya Ushirika vilivopo kwani Afisa 1 anapaswa kuhudumia Vyama 7-10 hivyo kupelekea kuwepo na upungufu wa Maafisa Ushirika 55.
2. IDADI YA VYAMA VYA USHIRIKA
Mkoa unavyo Vyama vya Ushirika 689 kwa mchanganuo ufuatao:-
S/N |
Aina ya Vyama |
Idadi ya vyama |
Idadi ya Wanachama |
1. |
AMCOS (Vyama vya Ushirika wa Mazao Kahawa, Pamba, Tumbaku na Chai) |
249 |
105,430 |
2. |
SACCOS-(Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo) |
336 |
59,489 |
3. |
Madini (Vyama vya Ushirika wa wachimba madini) |
2 |
388 |
4. |
Uvuvi(Vyama vya Ushirika wa Wavuvi) |
14 |
366 |
5. |
Wafugaji (vyama vya Ushirika wa Wafugaji) |
33 |
1098 |
6. |
Nyumba (Vyama vya Ushirika wa Nyumba) |
5 |
149 |
7. |
Vyama vya Ushirika wa Walaji |
4 |
157 |
8. |
Vyama vya Ushirika wa Wasafirishaji |
1 |
201 |
9. |
Vyama vya Ushirika wa aina nyingine |
42 |
1,222 |
10. |
Vyama Vikuu vinavyojihusisha na ukusanyaji wa kahawa |
2 |
Vyama 222 |
11. |
Vyama Vikuu vya ushirika wa Akiba na Mikopo |
1 |
Vyama 29 |
Jumla |
689 |
168,751 |
Vyama vya Ushirika Mkoani Kagera vinazo mali mbalimbali zinazomilikiwa na vyama hivyo. Mali hizo ni Viwanda vya kukoboa kahawa 2, Mashamba ya miti, Shule, za Sekondari, Maghala 134, Mizani 318, Kasiki 258, Nyumba za biashara kama vile hotel nyumba za kupangisha, Magari, Pikipiki, majengo ya ofisi na samani zake.
4. KILIMO CHA PAMBA MSIMU WA 2018/2019
Pamba katika Mkoa wa Kagera inalimwa katika Wilaya ya Muleba Msimu wa Pamba ulifunguliw arasmi mnamo tarehe 1 Mei, 2018 lakini kwa Mkoa wa Kagera ukusanyaji wa Pamba kutoka kwa wakulima ulianza tarehe 18 Juni, 2018 katika Wilaya ya biharamulo na tarehe 6 Julai, 2018 katika Wilaya ya Muleba. Makampuni yanayonunua Pamba ya wakulima ni Kahama Cotton Company Ltd na Kahama Oil Mill Ltd. Hadi sasa jumla ya kilo 1,278,070 zimeshanunuliwa na kulipwa na kampuni hizo.
5. KILIMO CHA TUMBAKU MSIMU2018/2019
Kwa Mkoa wa Kagera ni Wilaya ya Biharamulo pekee ndiyo inayolima tumbaku. Msimu wa tumbaku kwa mwaka 2018/2019 ulianza tarehe 19 Juni, 2018 ambapo jumla ya kilo 156,487 zenye thamani ya Tshs. 629,451,262 zimeishakusanywa na kulipwa na msimu huu sasa umeishafungwa.
5.1 Takwimu za Wakulima na Uzalishaji
Ili kufikia malengo hayo, Viongozi wote pamoja na watendaji katika Mkoa wa Kagera wamekuwa wakisimamia na kufuatilia hatua mbalimbali za utekelezaji wa mpango kazi huo ambao uliozinduliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Meja (Mst) Salum.M.Kijuu tarehe 29 Januari, 2018.
Ili kuhakikisha maelekezo ya Serikali yanatekelezwa kwa ufanisi mkubwa, Mkoa wa Kagera uliandaa Mpango Kazi ambao unalenga katika kutekeleza maelekezo hayo na pia kuendeleza zao la kahawa ili kuongeza tija ya uzalishaji na hatimaye kumnufaisha zaidi mkulima. Mpango Kazi huo umegusa mambo makuu sita ambayo ni:-
5.2 Mkakati wa Mkoa katika kutekeleza Maelekezo ya Serikali
Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa Mikoa inayolima zao la kahawa aina ya robusta kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na kahawa aina ya Arabika. Hii ni kutokana na tofauti ya kijiografia kati ya Wilaya moja na nyingine. Hata hivyo Mkoa wa Kagera unazalisha kahawa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na Mikoa mingine ambapo karibu 50% ya kahawa yote nchini huzalishwa katika Mkoa wa Kagera. Serikali kupitia kwa heshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, mnamo tarehe 14 Januari, 2018 ilitoa maelekezo ya mfumo wa masoko ya kahawa kupitia mnada na kuwaondoa wanunuzi binafsi kununua kahawa kutoka kwa wakulima moja kwa moja na kuelekeza kuwa kahawa itakusanywa na vyama vya ushirika. Hivyo, wanunuzi wote binafsi wanapaswa kwenda mnadani Moshi kwa ajili ya ununuzi wa kahawa. .
6.0 KILIMO CHA KAHAWA MSIMU WA 2018/2019
Wakulima hao wana idadi ya miche aina ya robusta 49,438,699, miche ya arabika 1,239,549, ambayo imepandwa kwenye eneo la hekta 48,630.8. Makadirio ya mavuno ya kahawa kwa msimu wa 2017/2018 ni jumla ya tani 81,994 za kahawa ya maganda mbazo zinakadiriwa kufikisha tani 40,996.7 za kahawa safi. Aidha, Kahawa yote itakayovunwa inatarajiwa kukusanywa kupitia vyama vya ushirika vya msingi vilivyopo katika maeneo yanayolima zao la kahawa kama yalivyo maelekezo ya Serikali.
Kutokana na takwimu za wakulima zilizokusanywa hadi kufikia mwezi Mei, 2018, Mkoa wa Kagera unahitaji miche bora ya kahawa aina ya robusta 6,779,858, miche ya arabika 291,335; mbolea ya kupandia (DAP) tani 1,974.5; mbolea ya kukuzia (N.P.K) tani 2,560.6; misumeno 107,826 na mikasi 100,787 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za shamba. Vilevile Mkoa unahitaji lita 112,052 za viauatilifu. Aidha mbolea na viuatilifu vinatakiwa kufika mkoani mwezi Julai na Desemba kila mwaka ili kuwahi misimu ya mvua inayoanza kati ya mwezi Agosti na Septemba kwa mvua za vuli na mwishoni mwa Februari kwa mvua za masika.
6.2.3 Takwimu za Maafisa Ugani
Mkoa wa Kagera una jumla ya Halmshauri 8, kata 192, na vijiji/Mitaa 732 ambapo zaidi ya 80% ya vijiji vyote vinazalisha zao la kahawa. Mkoa wa Kagera una jumla Maafisa Ugani 468 ambapo kata zenye maafisa ugani ni 184 sawa na 94% ya kata zote, vijiji vyenye maafisa ugani ni 260 sawa na 35.4% ya vijiji vyote. Jumla ya kata 8 na vijiji 472 havina mafisa ugani kabisa. Kati ya maafisa ugani 468, Maafisa ugani 73 sawa na 15.6% tu ndio walibainika kuwa na usafiri wa pikipiki kwa ajili ya kuwasaidia katika shughuli zao za kusimamia kilimo, Aidha maafisa ugani 100 tu sawa na 21.4% walikuwa na vifaa saidizi kama vile misumeno, vifaa vya kujikinga pamoja na mikasi.
Kwa kuzingatia takwimu hizi Halmashauri zote zimeelekezwa kuweka mkakati wa kuhakikisha kuwa maafisa ugani wanapatiwa vitendea kazi na pia kuweka mpango wa mafunzo maalum kwa ajili ya kuwapatia mafunzo wale ambao hawana uelewa mzuri kuhusu zao la kahawa kwa kushirikiana na Kituo cha Utafiti wa kahawa TaCRI- maruku.
Hadi kufikia juni, 2018 jumla ya vyama vikuu vya ushirika viwili (2) na vyama vya ushirika vya msingi vipatavyo 232 vinavyojihusisha na zao la kahawa vilikuwa vimesajiliwa katika Mkoa wa Kagera. Aidha, Jumla ya mashine za kukoboa kahawa (hullers) 134, mizani 318, maghala 520 na kasiki 258 vimebainika kuwepo katika baadhi ya vyama vya ushirika.
6.2.4.1 Makusanyo na usafirshaji wa kahawa msimu wa 2018/19
Hadi kufikia tarehe 3 Agosti, 2018 KDCU Ltd ilikuwa imekusanya jumla ya kilo 11,222,660 za kahawa za maganda na KCU (1990) Ltd ilikuwa imekusanya jumla ya kilo 3,014,448 za kahawa za maganda. Aidha, jumla ya kilo 1,078,525 ya kahawa hai (organic coffee) zilizokobolewa zimekwishakusanywa na KCU (1990) Ltd. Kahawa hizi zinalo soko maalumu nje ya nchi.
Hadi tarehe 03 Agosti, 2018 KCU (1990) Ltd haijalipa malipo ya awali kwa wakulima kiasi cha Tshs. 3,072,591,752/= na KDCU Ltd bado wanadaiwa na wakulima kiasi cha Tshs.4,500,000,000/=. Mpango uliopo wa kuyalipa madeni haya ni kutumia maombi mapya ya mkopo toka TADB na fedha ya malipo ya kahawa inayokuwa inauzwa mnadani ili itumike kurudi kwenye mzunguko wa kuwalipa wakulima.
NB: Kwa minada ya tarehe 12/07/2018, 19/07/2018 na 26/07/2018 bei za kahawa mnadani Moshi zilikuwa chini hali iliyopelekea KCU (1990) Ltd kwa kutumia Kitengo chake cha Mauzo ya Nje (Export Unit) kilichopo Moshi waliamua kuzichukua kahawa hizo kiasi cha Kg 515,473 ili kuzitafutia soko nje ya nchi lenye bei kubwa zaidi ya ile iliyotolewa mnadani kwa siku hizo. Aidha Bodi ya kahawa inapaswa kuleta fedha za mauzo ya kahawa iliyouzwa mnadani kwenye vyama ili fedha hizo ziweze kutumika kwenye mzunguko wa kuwalipa wakulima.
Jina la Chama Kikuu |
Tarehe ya mnada |
Kahawa iliyopelekwa mnadani |
Kiasi cha kilichouzwa |
Thamani ya kahawa iliyouzwa |
Wastani wa bei |
Mnunuzi |
KCU (1990) Ltd
|
12/07/2018
|
119493 |
119493 |
554,412,586.02 |
439.71 |
KCU-Export officer
|
19/07/2018
|
347,790 |
59,950 |
313,171,250.63 |
5223.88 |
KCU
|
|
26/07/2018
|
370,890 |
238,640 |
663,975,337.5 |
2782.33 |
OLAM, KCU, TAYLOR
WINCH, SHERIF DEWJI
|
|
02/08/2018
|
251,960 |
236,140 |
822,001,796.61 |
3481.00 |
KCU, AMIR AMZA, TAYLO WINCH
|
|
Jumla
|
|
1,090,133 |
654,223 |
2,353,560,970.7 |
|
N/A
|
KDCU Ltd
|
19/07/2018
|
360,000
|
288,000 |
898,801,722 |
3120.84
|
COTACOF,EBERO NA DTQ
|
26/07/2018
|
360,000
|
414,000 |
1,370,260,325.70 |
3309.81 |
COTACOF & IBERO
|
|
02/08/2018
|
360,000
|
378,000 |
986,569,398.90
|
2609.97
|
AMRI H,DTQ, TWT
|
|
Jumla
|
|
1,080,000 |
1,080,000 |
2,269,062,048 |
|
|
Tangu msimu ulipotangazwa mwezi Mei, 2018 tayari Vyama Vikuu vya Ushirika vya KCU (1990) Ltd na KDCU Ltd vimeshauza kahawa katika minada minne (4) ya kahawa iliyokwishafanyika Mjini Moshi kuanzia tarehe 12/07/2018, 19/07/2018, 26/07/2018 na 02/08/2018. Mchanguo wa mauzo wa mauzo hayo ni kama ifuatavyo:-
6.2.4.3 Mauzo ya kahawa mnadani
Hadi kufikia tarehe 03 Agosti, 2018 KDCU Ltd ilikuwa imekoboa jumla ya kilo 5,000,000 kwa kutumia viwanda binafsi vilivyopo kwenye maeneo yao (KADERES, ASU, Karagwe Marketing na Amri Amir) pamoja na kiwanda kinachomilikiwa na chama kilichoko Kamahungu. Aidha KCU Ltd ilikuwa imeshakoboa jumla ya kilo 2,229,000 za kahawa maganda kwa kutumia kiwanda chake cha BUKOP Ltd kilichopo Manispaa ya Bukoba.
Hadi kufikia tarehe 3 Agosti, 2018 jumla ya wakulima 64,300 wa KDCU walikuwa wamekwishasajiliwa katika Mfumo wa Mpya wa Malipo kupitia Akaunti za Benki ya CRDB Bank na NMB. Kwa upande wa KCU wakulima 43,000 walikuwa wamekwishasajiliwa katika Mfumo wa Mpya wa malipo kupitia Akaunti za Benki ya CRDB Bank kufikia tarehe 3 Agosti, 2018.
6.2.4.6 Mapokezi ya fedha na Malipo ya awali kwa wakulima
Kwa upande wa KCU (1990) Ltd mikopo ulioidhinishwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ni Tshs. 8,000,000,000.00 na kiasi kilichopokelewa hadi kufikia tarehe 3 Julai, 2018 ni 7,883,456,303.00 ambapo Tshs. 4,455,307,836.84 zimetumika kulipa deni la CRDB. Kiasi cha Tshs. 173,278,607.16 zimetumika kufanya maandlizi ya msimu, Kiasi cha Tshs. 40,590,000.00 zimetumika kulipia ada ya mkopo wa TADB na kiasi cha Tshs. 3,256,747,048.00 zimetumika kukusanyia kahawa ikiwa ni malipo ya awali ya wakulima ya Tshs.1, 000.00 kwa kilo ya kahawa ya maganda.
Mikopo ulioidhinishwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa KDCU ni Tshs. 11,760,000,000.00 na kiasi kilichopokelewa hadi kufikia tarehe 3 Agosti, 2018 ni 11,760,000,000.00 ambapo Tshs. 3, 223,295,565.31 zimetumika kulipa deni la CRDB. Kiasi cha Tshs. 1, 000,000,000.00 zimetumika kufanya maandlizi ya msimu ikiwa ni pamoja na kulipia ada ya mkopo TADB na kiasi cha Tshs. 7,237,904,210.00 zimetumika kukusanyia kahawa ikiwa ni malipo ya awali ya wakulima ambayo ni Tshs.1,000/= kwa kilo ya kahawa ya maganda.
Katika Wilaya ya Ngara kuna Chama cha Ushirika kinachoitwa Ngara Farmers Cooperative Society Ltd kinachojihusisha na ukusanyaji wa kahawa ya wakulima wa Wilaya ya Ngara. Chama kama ilivyo kwa KCU (1990) Ltd na KDCU Ltd nacho kimepata mkopo wa Tshs 1.2 bil kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa ajili ya kukusanyia kahawa kutoka kwa wakulima. Maandalizi ya msimu yamekamilika ingawa ni kwa kuchelewa na tayari zoezi la ukusanyaji wa kahawa linaendelea vizuri na malipo ya awali kwa wakulima yanafanyika. Kahawa zote zitakazokusanywa na Ngara Farmers zitakobolewa katika kiwanda cha Arab Globe.
Mahitaji ya miche bora ya kahawa kwa Mkoa wa Kagera ni miche ya arabika 291,335 na miche ya robusta 6,779,858 Aidha, chanzo kikuu cha miche bora ya kahawa ni kutoka Kituo cha Utafiti wa kahawa TaCRI ambao pia hushirikiana na Halmashauri za Wilaya katika kuanzisha vitalu vya miche karibu na maeneo ya wakulima wa kahawa. Hata hivyo idadi ya miche inayopatikana kwenye vitalu vilivyopo ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na mahitaji halisi ya miche kwa Mkoa. Tuna amini Bodi ya kahawa ambao wanadhamana ya kuwezesha upatikanaji wa miche ya kahawa watashirikiana na TaCRI ili waweze kuongeza uzalishaji kwani uwezo upo changamoto ni uwezeshaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa