- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
UTANGULIZI
Mabadiliko ya Tabianchi.
Dunia imekuwa na mabadiliko makubwa ya tabianchi yanayosababisha uhaba wa mvua na hatimaye kuleta upungufu mkubwa wa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
Hali ya mabadiliko ya tabianchi imefanya majira ya mvua katika Mkoa wa Kagera kubadilika ambapo msimu wa mvua za vuli unaanza kunyesha mwezi Novemba badala ya mwezi Septemba wakati msimu mvua za masika unaanza kunyesha mwezi Aprili badala ya mwezi Februari hadi Juni.
Sera na Maelekezo ya Serikali.
Hali hii imefanya Serikali kuanzisha Sera ya umwagiliaji ya mwaka 2010 kwa lengo la kuinua Kilimo cha umwagiliaji.
Pamoja na sera ya Umwagiliaji yapo maelekezo mengine yanayosisitiza Kilimo kama vile:
Mpango wa Serikali wa Maendeleo wa Miaka Mitano kuanzia 2015 hadi 2020.
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 ambayo imesisitiza kilimo cha umwagiliaji kupitia Ibara Na. 21(m) na 22(c) i-vii.
Uongozi imara wa Sekretariet ya Mkoa wa Kagera unaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera (Mh. Mej. Jen.Mstaafu Salum M. Kijuu) pamoja na Katibu Tawala Mkoa (CP. Diwani Athuman) unaosimamia utekelezaji wa Sera,Miongozo na Maelekezo yote ya Serikali Kuu kuhusu sekta ya kilimo cha umwagiliaji.
Aina mbalimbali za Kilimo cha Umwagiliaji.
Umwagiliaji unaweza kufanywa kwa kutumia njia mbalimbali ambazo ni pamoja na:
1. Njia ya mafuriko(Surface Irrigation).
2. Njia ya mabomba(Sub surface Irrigation).
3. Njia ya Mtawanyo (Sprinkler Irrigation).
4. Njia ya matone(Drip Irrigation).
Ambapo kwa Mkoa wa Kagera umwagiliaji wa njia za mafuriko,mabomba na matone ufanywa na wakulima wadogowadogo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri za Wilaya ila umwagiliaji wa njia ya sprinkler unafanyika hasa katika mashamba makubwa ya Kiwanda cha Sukari Kagera(Kagera Sugar) kwani njia hiyo umwagiliaji ni nzuri hasa kwa mashamba makubwa kwa kuwa unamwagilia eneo kubwa kwa muda mfupi ingawaje inagharimu fedha nyingi katika kuendesha jenereta na mitambo mengine saidizi ya mfumo huo.
MIKAKATI INAYOTUMIKA.
Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya pamoja na wadau wengine wa maendeleo umejiwekea mikakati mbalimbali ya utekelezaji wa kilimo cha umwagiliaji.
Mikakati hiyo ni pamoja na:
Kuhamasisha umma na sekta binafsi katika Kilimo cha umwagiliaji.
Kuhakikisha kwamba mifumo ya umwagiliaji (Inayoanzishwa na itakayoanzishwa) inazingatia sheria na taratibu za nchi.
Kuhamasisha matumizi bora ya rasilimali maji katika mifumo ya Kilimo cha umwagiliaji.
Kuhakikisha kwamba Maendeleo ya Kilimo cha umwagiliaji yanazingatia masuala ya kiufundi, kiuchumi, kijamii na kimazingira.
Kuhakikisha kwamba rasilimali maji ya umwagiliaji yanatumika kikamilifu kwa kiwango cha juu kwa kuzingatia tija.
Kuhakikisha kwamba miundo ya maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji(Irrigation development models) inatumika kuzalisha mazao yenye tija kulingana na mahitaji ya soko.
Kuhuisha masuala mtambuka kama vile jinsia, ukimwi, mazingira, afya, ardhi na maji katika maendeleo ya Kilimo cha umwagiliaji.
Kuendelea kutekeleza Kilimo cha umwagiliaji kupitia programu ya maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP) kwa kuongeza eneo lenye miundo mbinu ya umwagiliaji kutoka hekta 19,831 za Desemba 2016 hadi hekta 50,000 ifikapo mwaka 2020. Sekta binafsi itashirikishwa katika uendelezaji na uwekezaji kwenye kilimo cha umwagiliaji.
Kuzihimiza Halmashauri kukamilisha kutunga sheria ndogo za umwagiliaji.
Kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji ya wakulima wadogo na wakati ili kuongeza uzalishaji na ufanisi wa matumizi ya maji.
Kujenga na kukarabati mabwawa ya kuvuna na kuhifadhi maji ya mvua na mito kwa ajili ya umwagiliaji kwa kila Halmashauri ya wilaya.
Kujenga uwezo wa Taasisi zinazohusika na umwagiliaji katika ngazi ya Halmashauri za wilaya na wakulima katika usimamizi na uendeshaji endelevu wa miradi ya umwagiliaji.
Wilaya
|
Eneo linalofaa kwa umwagiliaji(Ha)
|
Eneo linalotumika kwa umwagiliaji(Ha)
|
Asilimia ya matumizi(%)
|
Bukoba
|
10,300
|
497
|
4.8
|
Muleba
|
5,895
|
400
|
6.78
|
Missenyi
|
20,463
|
15,564
|
76.05
|
Ngara
|
5,000
|
3,200
|
64
|
Biharamulo
|
1300
|
50
|
3.8
|
Karagwe
|
3750
|
177.7
|
4.7
|
Kyerwa
|
250
|
50
|
20
|
JUMLA
|
43,918
|
19,831
|
45.15
|
MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Hapo juu ni takwimu za maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji pamoja maeneo yanayolimwa kwa sasa Mkoani Kagera hadi kufikia Desemba, 2016.
NB: Serikali Mkoani kagera inaendelea kufanya mwasiliano na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Ofisi ya Tume ya Umwagiliaji Kanda-Mwanza ili ifanyike National Irrigation Master Plan kwa ajili ya kubaini maeneo zaidi yanayofaa kwa Kilimo cha Umwagiliaji.
Pia Serikali ya Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI,Kituo cha Uwekezaji Tanzania pamoja na Wizara ya Maji na Umwagiliaji inaendelea na utaratibu wa kutangaza maeneo ya uwekezaji hasa yale yanayofaa kwa Kilimo cha umwagiliaji yakiwemo mabonde ya:Kyabalamba(500ha)-Bukoba,Katoro(515.2ha)-Bukoba,Kiijongo(961.2ha)-Bukoba,Kazinga(18ha)-Bukoba,Buterankuzi(221.6ha)-Bukoba,Kaibanja(654.4ha)-Bukoba,Ngarama(506.4ha)-Bukoba,Burigi(400ha)-Muleba, Nkenge(1300ha)-Missenyi,Bulembo(662.4ha)-Missenyi,Kabajuga(783.6ha)-Missenyi,Butulage(402.4ha)-Missenyi,Byeju(500ha)-Missenyi, Kajunguti(1000ha)-Missenyi, Buchurago(2000ha)-Missenyi, Kabingo(500ha)-Missenyi,Ngono(1300ha),Mpanyula(110ha)-Ngara, Rwinyana(40ha)-Ngara, Mubuhenge(86ha)-Ngara, Mugozi(120ha)-Ngara, Magamba(88ha)-Ngara,Mwiruzi(1000ha)-Ngara,Ngundusi(110ha)-Ngara,Muhongo(170ha)-Ngara,Ruvubu(300ha)-Ngara,Kagera(580ha)-Ngara,Mukafigiri(60ha)-Ngara,Murutabo(100ha)-Ngara,Nyarulama(110ha)-Ngara,Nzaza(150ha)-Ngara Bujuruga(300ha)-Karagwe, Nyakakika(100ha)-Karagwe na Kibogoyizi(375ha)-Karagwe, Mato(600ha)- Karagwe, Mkakajinja(500ha)-Karagwe, Nyakahita(450ha)-Karagwe, Bwelanyange(45ha)-Karagwe,Bukangara(570ha)-Karagwe na Mushabaiguru(210ha)-Karagwe.
MIRADI YA UMWAGILIAJI INAYOTEKELEZWA.
Serikali kupitia Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo nchini(ASDP) kwa kushirikisha wadau wa maendeleo kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB), World Vision Tanzania pamoja na Shirika la Maendeleo la Watu wa Japan (JICA) imeweza kutekeleza uanzishwaji wa Miradi ya Umwagiliaji katika maeneo mbalimbali ikiwa inamilikiwa na Serikali pamoja na wananchi wa maeneo husika kama ifuatavyo;-
Missenyi-Kyakakera (163ha/watu156), Karagwe-Mwisa (300ha/Watu 180), Ngara-Bigombo (110ha/Watu160), Biharamulo-Mwiluzi (120ha/Watu 200), Muleba-Kyamyorwa (500ha/Watu 300), Buyaga (80ha/Watu 150), Buhangaza (95ha/Watu 130) na Kyota (120ha/Watu 190)
NB: Mazao makubwa yanayolimwa katika maeneo ya miradi hiyo ni Mahindi, Mpunga,Mazao ya mizizi(Mihogo,Viazi vitamu,Viazi vikuu & Viazi Mviringo), Mazao ya mafuta(Alizeti & Ufuta) pamoja na Mbogamboga(Mchicha,Matango,Chainizi,Spinachi,Maboga,Vitunguu,Nyanya,pilipili,matikiti maji).
CHANGAMOTO
Zipo changamoto kadhaa zinazojitokeza katika utekelezaji wa mikakati ya kilimo cha umwagiliaji Mkoani kagera ikiwemo na:-
Bajeti ndogo ya uwekezaji katika kilimo cha umwagiliaji.
Uwezo na ushiriki mdogo wa taasisi binafsi katika maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji.
Ujuzi mdogo kwa wakulima kuhusu kilimo cha umwagiliaji.
Uwezo mdogo wa Halmashauri za wilaya katika uwekezaji na utekelezaji wa Kilimo cha umwagiliaji.
Utumiaji mdogo wa maji (insufficient water use) unaosababisha ukosefu wa tija katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji.
Ukosefu wa mifumo bora ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji.
Ukosefu wa vihifadhi bora vya maji (Water storage facilities) kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji.
Kukauka kwa vyanzo vya maji kunakosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Upungufu wa wataalamu wa umwagiliaji katika Halmashauri za wilaya.
MIKAKATI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO.
Katika kukabiliana na changamoto zilizopo, Serikali Mkoani Kagera imepanga kufanya yafuatayo ili kuendeleza kilimo cha umwagiliaji katika msimu wa mwaka 2016/17:-
Kuzishauri Halmashauri za Wilaya kutenga bajeti ya kutosha katika sekta ya umwagiliaji ili zisaidie katika zoezi la Tathimini na Ufuatiliaji wa shughuli za Umwagiliaji.
Kuhamasisha taasisi binafsi ili ziweze kushiriki vema katika kuendeleza sekta ya kilimo cha umwagiliaji.
Mfano: Kagera Tea Co. Ltd, KSL,MAYAWA,Igabiro Agric Institute n.k
Kuwawezesha wakulima mbinu mpya na bora zitakazosaidia kuendeleza kilimo cha umwagiliaji kupitia Wataalamu wa Ugani waliopo katika kila Kata na Vijiji.
Kuhamasisha matumizi bora na endelevu ya rasilimali maji kwaajili ya kufanikisha kilimo cha umwagiliaji kupitia Wataalamu wa Sekta ya Umwagiliaji waliopo katika Halmashauri za Wilaya pamoja na Tume ya Umwagiliaji ya Taifa.
Kuandaa mifumo bora, endelevu na yenye tija kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji.
Kuzihimiza Halmashauri kuandaa mipango bora na matumizi bora ya ardhi kwa sekta ya umwagiliaji.
Kusimamia ujenzi wa vihifadhi bora vya maji (Water storage facilities) vitakavyosaidia kuendeleza kilimo cha umwagiliaji.
Kuhamasisha na kuendeleza juhudi za utunzaji wa mazingira hasa maeneo yazungukayo miradi ya umwagiliaji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Climatical Change) kwa ushirikiano wa Baraza la Utunzaji wa Mazingira Tanzania.
Kuzishauri Halmashauri za wilaya ili zitenge bajeti za kuajiri wataalamu wa umwagiliaji kulingana na tange pamoja na ikama ya Halmashauri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa