- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Fursa za Uwekezaji Katika Kilimo
Katika kujenga uchumi wa viwanda na kuelekea uchumi wa Kati ifikapo 2025, Mkoa wa Kagera unatangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika sekta za Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Maliasili, Huduma za Fedha na Mitaji, Utalii n.k. Miongoni mwa fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani Kagera ambazo zikitumiwa vizuri zinaweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi ni kupitia kilimo na viwanda.
Mkoa wa Kagera unayo fursa ya kupakana karibu na nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kagera Geographical Strategic Location) zikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi na nchi ya Kenya kwa upande wa Ziwa Victoria, Jumuiya yenye zaidi ya watu 150 milioni inatoa fursa ya masoko ya mazao na bidhaa zitakazozalishwa Kagera.
Hali ya hewa ya Mkoa wa Kagera pamoja na upatikanaji wa mvua kwa misimu miwili kwa mwaka inaruhusu kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara kama vile kilimo cha kahawa, miwa, chai, vanilla, alizeti, mpunga, mahindi, maharage, ndizi, viazi, mihogo, mbogamboga, maua n.k
Fursa Katika Kilimo; Kutokana na uwepo wa ardhi ya kilimo yenye rutuba mazao mbalimbali yanaweza kustawi katika Mkoa wa Kagera mfano kilimo cha mpunga, mahindi, maharage na mbogamboga katika Bonde la Mto Kagera, Mto Ngono na Bonde la Nkenge. Aidha, kilimo cha parachichi, vanilla, muhogo, kahawa, chai na zao jipya la chia. Vanilla inayozalishwa Kagera imethibitika kuwa na ubora wa juu duniani kuliko nchi yoyote kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha venille content, hivyo ipo fursa kubwa ya kuongeza uzalishaji wa vanilla Kagera tofauti na ilivyo sasa.
Kutokana na viwanda vyote vilivyopo Mkoani Kagera kuzalisha chini ya kiwango (under capacity), ipo fursa ya kuongeza na kukuza uzalishaji wa mazao kama chai, kahawa, miwa, alizeti n.k ili kupata malighafi ya viwanda hivyo viweze kufikia optimal capacity utilization.
Ujenzi wa soko la kimataifa katika mpaka wa Mutukula na ukamilishaji wa masoko ya kimkakati ya mpakani ya Murongo, Nkwenda na Kabanga utatoa fursa ya masoko kwa mazao na bidhaa zinazozalishwa katika Mkoa wa Kagera. Eneo la Mutukula lipo tayari, limepimwa, hati ipo na linamilikiwa na Halmashauri.
Fursa ya Kilimo cha Umwagiliaji: Mkoa wa Kagera unayo fursa ya kilimo cha umwagiliaji mazao ya mpunga, mahindi, maharage, mbogamboga na matunda katika eneo lenye takribani hekta 19,000 kwenye skimu za umwagiliaji za Kyota, Buyaga, Buhangaza, Kyamyorwa, Burigi, Muhutwe, Kyakakera, bonde la Nkenge na Mto Kagera pamoja na skimu ya Mwisa Wilayani Karagwe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa