- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
CPA Robert Lubimbi
Mkuu wa Kitengo
Lengo kuu la Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani katika Sekretarieti ya Mkoa wa Kagera ni kutoa ushauri kwa Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa juu ya matumizi sahihi ya rasilimali fedha kama imefuata sheria, kanuni na miongozo ya matumizi ya fedha za umma.
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kinahusika katika kukagua mifumo mbalimbali iliyowekwa ili kutumika kutunza rasilimali mbalimbali za Serikali kama inatumika ipasavyo na kufuatwa katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali kulingana na mifumo hiyo.
Pia Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kinahusika katika usimamizi wa thamani ya fedha (Value for Money) katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na kusimamiwa na Sekretarieti ya Mkoa wa Kagera. Kitengo kinakagua na kuhakiki mradi kama unaendana na thamani halisi ya kiwango cha fedha kilichotumika.
Katika Sekretarieti ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kina mtumishi mmoja anayefanya kazi ya Ukaguzi wa ndani Katika Sekretarieti ya Mkoa wa Kagera, pia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera pamoja na Ofisi za Wakuu wa Wilaya saba za Mkoa wa Kagera.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa