- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
1.0 UTANGULIZI |
Mkoa wa Kagera unapatikana Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Tanzania ambapo unapakana na nchi ya Uganda kwa upande wa Kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa Magharibi mkoa wa Kigoma na Mwanza kwa upande wa Kusini na Ziwa Victoria kwa upande wa Mashariki. Mkoa huu una jumla ya Halmashauri za Wilaya 8 ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Muleba, Kyerwa, Biharamulo, Ngara, Missenyi na Karagwe.
Sekta ya Uvuvi ni moja ya Sekta muhimu katika kuwapatia Wananchi wengi wa Mkoa wa Kagera ajira, kipato, lishe bora na hivyo kuchangia katika kumuondolea mwananchi umaskini. Shughuli za Uvuvi katika Mkoa hufanyika katika Ziwa Victoria, mto Kagera, Ngono, Ruvuvu na Mabwawa. Maeneo mengine ya Uvuvi ni katika Maziwa madogo madogo ya Burigi, Rwakajunju, Kamakala, Ikimba, Rushwa, Melula, Katwe, Luko, Karenge, Mitoma, Kaburi, Kitete, Kabindi, Ngoma na Rumanyika. Samaki wanaovuliwa katika Ziwa Victoria ni Sangara (Nile perch), Dagaa, Sato jamii ya Nile tilapia (O. niloticus, variabilis, Oesculentus na leucostictus), Kambale (Clarius gariepinus) na furu (Haplochromis).
Mkoa katika kuendeleza Sekta ya Uvuvi unasimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na mikakati mbalimbali ya Sekta ya Uvuvi ikiwa ni pamoja na kudhibiti Uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira, kuendeleza ufugaji bora wa samaki, kudhibiti utoroshaji wa mazao ya samaki kwenda nchi jirani, kutoa elimu juu ya madhara ya Uvuvi haramu na VVU/UKIMWI, kusimamia masoko na mialo ya samaki, kuhakiki viwango vya ubora na usalama wa mazao ya Uvuvi na kusajili mitumbwi ili kudhibiti mapato na uhalifu n.k.
Taarifa hii inaelezea muendelezo wa utekelezaji wa shughuli za Uvuvi, ambapo kwa kipindi cha Mwaka wa fedha 2017/2018 kuanzia Mwezi Julai 2017 hadi Agosti, 2018, Sekta ya Uvuvi Mkoa wa Kagera imechukua na inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kisheria katika kulinda raslimali za Uvuvi kwa ajili ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
2.0 Dira, Dhamira na Malengo ya Mkoa Kuendeleza Sekta ya Uvuvi |
Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya Sekta ya Uvuvi umedhamiria kulinda raslimali za Uvuvi kwa kufanya Uvuvi endelevu unaozingatia Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003.
Dhamira ya Mkoa ni kuwajibika ipasavyo katika kulinda raslimali ya Uvuvi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa jamii.
Kukuza uhifadhi, maendeleo na usimamizi endelevu wa raslimali za Uvuvi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Katika kufanikisha utekelezaji wa dira na mwelekeo wa Mkoa kuendeleza Sekta ya Uvuvi, malengo 15 yamependekezwa kama ifuatavyo:-
3.0 Hali ya Sekta ya Uvuvi Mkoa wa Kagera |
Tangu enzi za Uhuru, shughuli za Uvuvi zimekuwa miongoni mwa vyanzo muhimu vya mapato na lishe kwa wakazi wengi wa Mkoa wa Kagera. Shughuli za Uvuvi hufanyika kwa kiasi kikubwa katika Ziwa Victoria, mito na maziwa madogo madogo 15 (Satellite lakes). Shughuli hizi zinalenga kwa kiasi kikubwa kwenye Uvuvi wa Sangala wanaovuliwa kwa wingi na wenye Soko kubwa ndani na nje ya nchi. Samaki huyu ameleta faida kubwa kwa upande wa “pato la taifa” na wananchi ambapo amewafanya kuwa matajiri. Samaki wengine (Endermic Species) wanaovuliwa katika Ziwa Victoria kama vile Sato, Nembe, Gogogo, Ningu, Soga, Dagaa, Furu, Kamongo, Ngege, Mumi, Mbofu, Kuyu nk. Samaki hawa walivuliwa kwa kutumia nyavu za inchi 2½ hadi inchi 3.
Kutokana na Sensa ya Uvuvi ya mwaka 2014idadi ya wavuvi katika Mkoa wa Kagera imeongezeka kutoka wavuvi 9,616mwaka 2000 hadi wavuvi 23,740mwaka 2018. Sambamba na hilo idadi ya mitumbwi nayo imeongezeka kutoka mitumbwi 3,395mwaka 2000hadi mitumbwi 7,338 mwaka 2018.Pia idadi ya nyavu za sangala imeongezeka kutoka nyavu 51,068 mwaka 2000 hadi nyavu 98,389 mwaka 2018.
Jedwali lifuatalo linaonyesha idadi ya Wavuvi, Mitumbwi na Nyavu kimkoa
MWAKA
|
IDADI YA WAVUVI
|
IDADI YA MITUMBWI
|
IDADI YA NYAVU (SANGALA)
|
IDADI YA NYAVU DAGAA
|
IDADI YA MIGONZO
|
2000
|
9.616
|
57,068
|
453
|
||
2016
|
24,122
|
7,321
|
100,288
|
1,836
|
1,492,174
|
2018
|
23,740
|
7,338
|
98,389
|
1,027
|
1,638,955
|
Kutokana na kuongezeka kwa nguvu ya Uvuvi (fishing effort) idadi ya samaki ziwani imekuwa ikipungua kila mara. Kwa mujibu wa sensa ya Uvuvi ya Mwaka 2014 na 2015, sangala walipungua kutoka tani 651,353 mwaka 2014 hadi tani 621,254 mwaka 2015. Wakati huo dagaa waliongezeka kwa asilimia 9% kutoka tani 698,736 Mwaka 2014 hadi tani 859,931 Mwaka 2015. Kiasi hiki cha dagaa kimekuwa kikiongezeka tangu mwaka 2007. Asilimia kubwa ya samaki hawa wanaishi mwambao wa pwani ya Ziwa.
Jedwali lifuatalo linaonyesha idadi ya dagaa na sangala waliomo ziwani.
|
Septemba 2011
|
Septemba 2014
|
Novemba 2015
|
||||
Stratum
|
Eneo (km2)
|
Dagaa (t/km2)
|
Sangala (t/km2)
|
Dagaa (t/km2)
|
Sangala (t/km2)
|
Dagaa (t/km2)
|
Sangala (t/km2)
|
Deep
|
6,166
|
63,510 |
136,269 |
78,925 |
53,583 |
198,947 |
54,137 |
Coastal
|
5,786
|
135,971 |
114,563 |
133,657 |
182,085 |
197,207 |
172,113 |
Inshore
|
2,003
|
51,677 |
53,480 |
45,268 |
49,053 |
61,013 |
43,398 |
SG
|
2,909
|
48,289 |
45,090 |
49,744 |
39,388 |
92,617 |
40,747 |
Deep
|
6,251
|
56,884 |
51,258 |
180,654 |
80,013 |
163,253 |
126,056 |
Coastal
|
6,601
|
53,468 |
40,266 |
151,823 |
179,217 |
78,943 |
128,011 |
Inshore
|
3,181
|
33,401 |
27,675 |
50,578 |
61,139 |
57,882 |
52,319 |
EP
|
2,022
|
14,558 |
3,033 |
8,088 |
6,875 |
10,071 |
4,472 |
JUMLA
|
476,068 |
471,634 |
698,736 |
651,353 |
859,931 |
621,254 |
4.0 Fursa Zilizopo Mkoa Wa Kagera Katika Sekta Ya Uvuvi |
Mkoa wa Kagera una eneo la maji lenye ukubwa wa kilomita za mraba 10,655 sawa na asilimia 27, jiografia nzuri, maeneo chepechepe yenye udongo unaotunza maji na vyanzo vingi vya maji (water bodies) kama vile mto Kagera, Mto ngono, mto Ruvuvu, mto Kanoni, Ziwa Victoria na maziwa mengine madogo madogo 15. Mkoa huu wa Kagera unasifika na kuwa Mkoa wa kwanza nchini Tanzania na wa pekee wenye maziwa madogo madogo (Satellite Lake) mengi yanayofikia 15 kama yafuatayo.
Ziwa Burigi Ziwa Burigi linapakana na Wilaya tatu ambazo ni Muleba, Karagwe na Biharamulo Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina samaki wengi aina ya Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haprochromis), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.
Ziwa Rwakajunju Ziwa Rwakajunju linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina ukubwa wa km2 27.72. Baadhi ya samaki waliomo ni pamoja na Furu (Haprochromis), Sato (Oreochromis esculentus na Variabilis), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.
Ziwa Kamakala Ziwa kamakala linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili linasifika kwa kuwa na samaki wengi aina Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haprochromis), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.
Ziwa Ikimba Ziwa Ikimba linalinapatikana Wilaya ya Bukoba Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina ukubwa wa km2 38.09. Baadhi ya samaki waliomo ni pamoja na Furu (Haplochromines), Sato (Oreochromis esculentus), Kamongo (Protopterus catastoma) na Kambale (Clarius gariepinus). Ziwa hili linapatikana Bukoba Vijijini Mkoa wa Kagera. Baadhi ya changamoto zilizopo Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.
Ziwa Rushwa Ziwa Rushwa linapatikana Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina ukubwa wa km2 10.08. Baadhi ya samaki waliomo ni pamoja na Sato (Oreochromis esculentus, leocosticus, niloticus, variabilis na Tilapia zilii), Kamongo (Protopterus aethhiopicus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.
Ziwa Melula Ziwa Melule liko Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina ukubwa wa km2 15.21. Samaki waliomo ni pamoja na Sato (Oreochromis esculentus na niloticus), Furu (Haplochromines) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.
Ziwa Katwe Ziwa katwe linapatikana Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina ukubwa wa km2 2.23. Ziwa hili lina aina 6 za samaki ambao ni pamoja na Sato (Oreochromis leocostictus), Furu (Haprochromines), Kamongo (Protopterus aethiopicus), Kambale (Clarius gariepinus), (Momyrus) na Gogogo (S.afrofischeri). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.
Ziwa Luko Ziwa Luko linapatikana Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina samaki wengi aina nyingi ya Sato (Oreochromis esculentus), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.
Ziwa Kalenge Ziwa Karenge linapatikana Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Ziwa lina aina 9 za samaki ambao ni Sato (O.leocostictus, niloticus na variabilis), Furu (Haplochromines), B.profundus na B.sadleri, Kambale (Clarius gariepinus na C.alluaudi) na Gogogo (S.afrofischeri). Ziwa hili linakumbwa na changamoto ya Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumu na magugu maji.
Ziwa Mitoma Ziwa Mitoma linapatikana Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Kuna aina 5 za samaki ambao ni (B.sadleri), Kambale (Clarius gariepinus), Furu (Haplochromines), Kamongo (Protopterus aethiopicus) na Gogogo (Synodontis afrofischeri).
Ziwa Kaburi Ziwa Kaburi linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili linasifika kuwa na samaki wengi aina Sato (Oreochromis esculentus), Kamongo (Protopterus aethiopicus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zilinazopo ni Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na kilimo na magugu maji.
Ziwa Kitete, Ziwa Kitete linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili linasifika kwa kuwa na samaki wengi aina Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haplochromines), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Ziwa hili Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.
Ziwa Kabindi Ziwa Kabindi linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili linasifika kwa kuwa na samaki wengi aina Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haplochromines), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Ziwa hili Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.
Ziwa Ngoma Ziwa Ngoma linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili linasifika kwa kuwa na samaki wengi aina Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haplochromines), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.
Ziwa Rumanyika Ziwa Rumanyika linapatikana katika hifadhi ya rumanyika Wilaya ya Kyerwa. Ziwa hili linasifika kwa kuwa na samaki aina Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haplochromines), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus).
5.0 SERA, SHERIA, KANUNI NA MIKAKATI YA SEKTA YA UVUVI |
5.1 SERA YA UVUVI YA MWAKA 1997 ILIYOBORESHWA MWAKA 2015 |
Sera ya Taifa ya Uvuvi ni chombo cha usimamizi ambacho kina himiza uvunaji, matumizi na biashara endelevu ya raslimali za uvuvi kwa ajili ya kuwapatia wananchi chakula, kipato, ajira na fedha za kigeni na ulinzi thabiti wa viumbe hai wa majini na mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo pamoja na kuhakikisha kuwa kunakuwepo na mafanikio/ufanisi. Lengo kuu la Sera ya Taifa ya Uvuvi ni kukuza uhifadhi, maendeleo na usimamizi endelevu wa raslimali za uvuvi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Pia Sera hii ina malengo ya kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Kupunguza umaskini nchini (MKUKUTA II).
5.2 SHERIA YA UVUVI NAMBA 22 YA MWAKA 2003
Sheria ya Uvuvi ni chombo kinachotumika katika kusimamia utekelezaji wa Sera ya Uvuvi. Dhumuni la Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 ni kuleta maendeleo endelevu, kulinda, kuhifadhi, kuendeleza ufugaji wa viumbe hai kwenye maji, kudhibiti ubora wa samaki na mazao yake, mimea ya majini na mazao yake na masuala mengine yanayofanana na hayo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Sheria ya Uvuvi Sehemu ya Tano (V) inasisitiza usimamizi na Udhibiti wa Shughuli za Uvuvi. Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003 inalenga Uvuvi endelevu unaozingatia taratibu pamoja na kuvua samaki kwa kutumia zana halali zinazoruhusiwa kisheria. Baadhi ya zana haramu za Uvuvi zisizoruhusiwi kisheria ni:-
6.0 UTEKELEZAJI WA SERA NA SHERIA YA UVUVI |
Mkoa wa Kagera umeendelea kusimamia na kutekeleza Sera ya Taifa ya Uvuvi ya Mwaka 1997, Mikakati na Sheria ya Uvuvi na. 22 ya Mwaka 2003.
Sekta ya Uvuvi ni moja ya Sekta muhimu kwa maendeleo ya wananchi wa Mkoa wa Kagera kiuchumi na kijamii.
Sekta ya Uvuvi inachangia kwa kiasi kikubwa katika kutoa ajira ambapo jumla ya wananchi26,830 wameajiriwa au kujiajiri kutokana na Shughuli za Uvuvi Mkoani Kagera. Kati ya hao waliajiriwa kwenye Viwanda vya samaki ni 462, ajira kwa wavuvi ni 23,740, wafugaji samaki ni 665 na wauzaji wa samaki ni 1,787. Kutokana na ajira hizi wananchi wameweza kujipatia kipato, fedha za kujikimu na kuboresha makazi na kuchangia maendeleo.
Jedwali Na. 3: Uchangiaji wa Sekta ya Uvuvi katika Ajira
Na
|
Wilaya
|
Ajira Kwa Viwanda
|
Ajira kwa Wavuvi
|
Ajira Kwa Wafugaji samaki
|
Ajira Kwa Wauzaji wa samaki
|
Jumla
|
1
|
Bukoba (M)
|
350 |
928 |
29 |
123 |
1,430 |
2
|
Bukoba (W)
|
112 |
3,475 |
61 |
241 |
3,889 |
3
|
Muleba
|
0 |
18,491 |
98 |
602 |
19,191 |
4
|
Karagwe
|
0 |
340 |
165 |
120 |
625 |
5
|
Missenyi
|
0 |
82 |
103 |
308 |
755 |
6
|
Kyerwa
|
0 |
424 |
40 |
305 |
769 |
7
|
Ngara
|
0 |
0 |
120 |
12 |
122 |
8
|
Biharamulo
|
0 |
0 |
49 |
76 |
49 |
|
Jumla
|
462 |
23,740 |
665 |
1,787 |
26,830 |
Sekta ya Uvuvi inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua hali ya uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Serikali kutokana na kodi mbalimbali. Kwa kipindi cha Mwaka wa fedha 2017/2018 kuanzia Mwezi Julai 2017 hadi Juni 30, 2018 jumla ya tani 4,651.8 za samaki zilivuliwa katika Ziwa Victoria ambazo zilikuwa na thamani ya Tshs Bilioni 27.75, maziwa madogo madogo (Satellite Lakes) na kwenye mabwawa ya kufugia Samaki yaliyopo Mkoani Kagera. Samaki hao wanatumika kama kitoweo na hivyo kusaidia kuboresha afya na wengine kuuzwa kwa ajili ya kujipatia kipato. Baadhi ya Samaki wameuzwa humu ndani ya Mkoa wetu wa Kagera na zingine kusafirishwa kwenda nchi za nje hivyo kusaidia kuliingizia Taifa fedha za kigeni.
Jedwali Na. 04: Uchangiaji wa Sekta ya Uvuvi katika Uchumi
Na |
Halmashauri ya Wilaya |
Samaki Waliovunwa Ziwa Victoria na Maziwa Madogo madogo
|
Samaki waliovunwa kwenye mabwawa ya Samaki |
||
Uzito (Kg) |
Thamani (Tshs)
|
Uzito (Kg) |
Thamani (Tshs) |
||
1 |
Bukoba MC
|
593,490 |
3,264,195,000 |
0 |
0 |
2 |
Bukoba DC
|
967,246 |
6,314,147,600 |
383 |
3,255,500 |
3 |
Muleba DC
|
2,908,856.8 |
17,470,742,400 |
420 |
2,100,000 |
4 |
Karagwe DC
|
82,689 |
330,756,000 |
170 |
850,000 |
5 |
Missenyi DC
|
47,609 |
285,654,000 |
25 |
75,000 |
6 |
Kyerwa DC
|
51,998 |
83,196,800 |
520 |
2,600,000 |
7 |
Ngara DC
|
0 |
0 |
200 |
1,000,000 |
8 |
Biharamulo
|
0 |
0 |
0 |
0 |
|
JUMLA
|
4,651,888.8 |
27,748,691,800 |
1,718 |
9,880,500 |
N.B: Chanzo cha taarifa ni wavuvi, wafanya biashara na wafugaji wa samaki
Katika kuendeleza ufugaji bora wa samaki Mkoani Kagera, wananchi wamehamasishwa kuchimba mabwawa hususani ufugaji wa samaki kibiashara, kutoa miongozo ya mabwawa ya mfano, kuzalisha, kusambaza vifaranga na kutoa mafunzo kwa wafugaji wa samaki.Kutokana na hamasa, elimu pamoja na juhudi za wafugaji samaki, jumla ya mabwawa 619 yamechimbwa mkoani Kagera kwa Mwaka 2017/2018 kutoka mabwawa 202 Mwaka 2008/2009 sawa na ongezeko la mabwawa 407.
Pia Vikundi 21 vimehamasishwa ufugaji bora wa samaki aina ya Sato na Kambale ambapo baadhi yao ni Kikundi cha Bugabo fish Pond, Ujamaa group, Chavuma sauti ya watu, Umoja ni nguvu, Fish pond development group (FPDG), Tujunangane Group na Jiunge, Wazee group n.k.
Jedwali Na. 5: Takwimu za Mabwawa ya Ufugaji wa Samaki Mkoani Kagera
WILAYA
|
Idadi ya Mabwawa Mkoa wa Kagera Kuanzia Mwaka 2008 – 2018
|
||||||||
2008/2009 |
2010/2011 |
2011/2012 |
2012/2013 |
2013/2014 |
2014/2015 |
2015/2016
|
2016/2017 |
2017/2018
|
|
Bukoba (M)
|
33 |
33 |
35 |
61 |
71 |
72 |
80 |
77 |
39 |
Missenyi
|
13 |
13 |
24 |
41 |
45 |
61 |
64 |
61 |
61 |
Muleba
|
41 |
41 |
48 |
87 |
121 |
121 |
144 |
180 |
221 |
Bukoba (W)
|
32 |
32 |
36 |
50 |
56 |
44 |
71 |
48 |
51 |
Kyerwa
|
0 |
0 |
0 |
39 |
42 |
42 |
50 |
52 |
53 |
Karagwe
|
49 |
49 |
57 |
55 |
58 |
67 |
71 |
73 |
73 |
Ngara
|
25 |
25 |
30 |
35 |
39 |
43 |
55 |
55 |
79 |
Biharamulo
|
0 |
0 |
7 |
19 |
21 |
21 |
32 |
38 |
42 |
Chato
|
9 |
4 |
6 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
Jumla
|
202 |
197 |
238 |
387 |
453 |
471 |
567 |
584 |
619 |
Vyombo vinavyotumika kwa shughuli za Uvuvi katika Ziwa Victoria na maziwa madogo madogo (Satellite lakes) yaliyopo Mkoa wa Kagera ni mitumbwi ya injini na mitumbwi midogo ya kasia.Kwa kipindi cha Mwaka wa Fedha 2017/2018 kuanzia Mwezi Julai 2017 hadi Juni 30, 2018 jumla ya mitumbwi ya kuvua samaki ni 7,338ambapokati ya hiyo, mitumbwi 3,415 ya kasia na mitumbwi 2,763 ya injini imesajiliwa na kulipia mapato sawa na asilimia 84.2 ya mitumbwi yote ya kuvua samaki.Zoezi la usajili wa mitumbwi linaendelea ili kuhakikisha kwamba mitumbwi yote imesajiliwa, kupewa namba za usajili na kulipia mapato ya Serikali.
Jedwali Na. 6: Takwimu za Mitumbwi ya kuvua Samaki Mkoa wa Kagera
Na |
H/WILAYA
|
Jumla ya Mitumbwi yote ya Kuvua Samaki |
Mitumbwi iliyosajiliwa na kulipia Mapato |
Mitumbwi ambayo haijasajiliwa |
||
Mitumbwi ya Kasia |
Mitumbwi ya Injini |
Mitumbwi ya Kasia |
Mitumbwi ya Injini |
|||
1 |
Bukoba (M)
|
417 |
79 |
236 |
69 |
33 |
2 |
Bukoba (W)
|
835 |
304 |
642 |
59 |
67 |
3 |
Muleba
|
5,554 |
2,725 |
1,854 |
696 |
49 |
4 |
Karagwe
|
196 |
147 |
5 |
44 |
0 |
5 |
Missenyi
|
62 |
25 |
26 |
11 |
0 |
6 |
Kyerwa
|
274 |
135 |
0 |
139 |
0 |
7
|
Ngara
|
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
8
|
Biharamulo
|
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
|
JUMLA
|
7,338 |
3,415 |
2,763 |
1,018 |
149 |
N.B: Wilaya za Biharamulo na Ngara hazipakani na Ziwa hivyo hakuna shughuli za Uvuvi ziwani bali ufugaji wa samaki kwenye mabwawa.
Halmashauri zote zenye shughuli za Uvuvi zimedhibiti uingiaji katika shughuli za Uvuvi kwa kuzingatia ukusanyaji wa mapato, usajili na kutoa leseni kwa vyombo vya Uvuvi na wavuvi kama vile mitumbwi, nyavu, wauzaji wa samaki na mazao ya Uvuvi. Kwa Mwaka 2017/2018 jumla ya Tshs bilioni 1.86 zimekusanywa kutokana na shughuli za Uvuvi zaidi ya bilioni 1.34 zilizo kusanywa mwaka jana 2016/2017 sawa na Ongezeko la Tshs milioni 519.
Jedwali Na7: Ukusanyaji wa mapato kuanzia Mwaka 2014 – 2018.
Na |
WILAYA
|
Mapato ya Uvuvi yaliyokusanywa Kuanzia Mwaka 2014 – 2018 |
|||
2014/2015
|
2015/2016
|
2016/2017
|
2017/2018
|
||
1 |
Bukoba (M)
|
51,367,000 |
51,140,745 |
77,710,022 |
110,800,864 |
2 |
Bukoba (W)
|
141,293,200 |
175,909,000 |
189,591,800 |
240,075,650 |
3 |
Muleba
|
690,078,200 |
793,266,270 |
1,014,915,156 |
1,462,390,802 |
4 |
Karagwe
|
3,283,000 |
1,745,000 |
29,679,600 |
5,844,600 |
5 |
Missenyi
|
2,716,500 |
5,536,000 |
9,917,500 |
13,506,700 |
6 |
Kyerwa
|
2,885,000 |
14,889,100 |
19,443,200 |
17,969,300 |
7 |
Biharamulo
|
0 |
0 |
0 |
350,000 |
8 |
Ngara
|
0 |
0 |
0 |
9,655,500 |
JUMLA KUU
|
891,622,900 |
1,042,486,115 |
1,341,257,278 |
1,860,593,416 |
N.B: Wilaya za Biharamulo na Ngara hazipakani na Ziwa Victoria hivyo hakuna shughuli za Uvuvi ziwani bali ufugaji wa samaki kwenye mabwawa.
Shughuli ya kudhibiti Uvuvi haramu ni mkakati endelevu katika Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kulinda raslimali ya mazao ya Uvuvi kutokana na Sera ya Uvuvi ya Mwaka 2015 na Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003. Shughuli hii imekuwa ikifanyika kwa kushirikisha taasisi mbalimbali kama vile Uvuvi, Polisi, Mahakama, TAKUKURU pamoja na Idara ya Uhamiaji kwa kufanya doria dhidi ya Uvuvi haramu katika mialo na nchi kavu.Piautekelezaji wa mikakati ya kazi hii ulifanyika kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile kutafuta taarifa za uhalifu, kuweka watoa taarifa za siri (informer) kwa maeneo mbalimbali pamoja taarifa kutoka kwa maafisa Uvuvi Wilaya na wananchi ambao wanachukia suala la Uvuvi haramu.
Katika kudhibiti matumizi ya zana haramu za Uvuvi Mkoani Kagera jumla ya doria 131 zimefanyika kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2017 hadi Juni, 2018 na hivyo kuwezesha kukamatwa zana haramu za Uvuvi ambazo ni kokoro za sangala 462, nyavu ndogo za dagaa 221, nyavu za timba 4,189, nyavu za makila ()5,300, katuli 17, Ndoano 820, mitumbwi 235 na samaki wachanga wenye uzito wa Kg 16,615 ambazo kwa ujumla zilikuwa na thamani ya Tshs Bilioni 7,249,054,500 kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali namba 4. Pia watuhumiwa 126 walikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria ambapo wengine wamehukumiwa na wengine kesi zao bado zinaendelea.
Aidha watendaji wote wa Vijiji na Mitaa wameandikiwa barua zenye maagizo yanayolenga kudhibiti vitendo vyote vya matumizi ya zana haramu za Uvuvi kuanzia ngazi ya Vijiji/Mitaa na kuhakikisha kuwa wavuvi haramu wanasalimsha zana zao haramu za Uvuvi kwa hiari. Zoezi hili linaenda vizuri ambapo hadi kufikia mwezi Juni 30, 2018 wavuvi 62 wamesalimisha zana haramu za Uvuvi walizokuwa wakizitumia kwa shughuli za Uvuvi na wengine waliokaidi walikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Pia vikundi vyote vya usimamizi wa raslimali za Uvuvi (BMU) vimeagizwa kutekeleza Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003 katika mialo.
N.B: Wilaya za Biharamulo na Ngara hazipakani na Ziwa Victoria hivyo hakuna shughuli za Uvuvi ziwani bali ufugaji wa samaki kwenye mabwawa.
Jedwali Na 5: Ukusanyaji wa mapato kwa kipindi cha Mwezi Juni 2016 – Julai, 2017.
MAKUSANYO YA MAPATO KWA ROBO YA TATU YA MWAKA WA FEDHA 2016/2017 (TSHS)
|
||||||||
Na
|
WILAYA
|
Malengo kwa mwaka (a)
|
Ada za Leseni/
Vibali (b) |
Tozo za Faini (c)
|
Maduhuli (d)
|
Makusanyo Mengine (e)
|
Jumla (f=b+c+d+e)
|
%
(f/a) |
1
|
Bukoba (M)
|
55,472,800 |
21,068,000 |
0 |
13,252,430 |
43,389,092 |
77,710,022 |
140.1 |
2
|
Bukoba (W)
|
273,250,000 |
33,317,000 |
2,760,000 |
151,208,800 |
0 |
189,591,800 |
69.38 |
3
|
Muleba
|
1,024,200,000 |
499,943,676 |
1,158,500
|
0 |
513,812,980
|
1,014,915,156
|
99.09 |
4
|
Karagwe
|
3,480,000 |
6,320,000 |
300,000 |
23,059,600 |
0 |
29,679,600 |
852.8 |
5
|
Missenyi
|
5,616,000 |
6,219,000 |
0 |
0 |
3,698,500 |
9,917,500 |
176.5 |
6
|
Kyerwa
|
2,500,000 |
16,392,200 |
3,051,000 |
0 |
0 |
19,443,200 |
777.1 |
JUMLA KUU
|
1,364,518,800
|
583,259,876 |
7,269,500 |
187,520,830 |
560,900,572 |
1,341,257,278 |
98.13 |
N.B: Wilaya za Biharamulo na Ngara hazipakani na Ziwa Victoria hivyo hakuna shughuli za Uvuvi ziwani bali ufugaji wa samaki kwenye mabwawa.
Shughuli ya kudhibiti Uvuvi haramu ni mkakati endelevu katika Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kulinda raslimali ya mazao ya Uvuvi kutokana na Sera ya Uvuvi ya Mwaka 2015 na Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003. Shughuli hii imekuwa ikifanyika kwa kushirikisha taasisi mbalimbali kama vile Uvuvi, Polisi, Mahakama, TAKUKURU pamoja na Idara ya Uhamiaji kwa kufanya doria dhidi ya Uvuvi haramu katika mialo na nchi kavu. Pia utekelezaji wa mikakati ya kazi hii ulifanyika kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile kutafuta taarifa za uhalifu, kuweka watoa taarifa za siri (informer) kwa maeneo mbalimbali pamoja taarifa kutoka kwa maafisa Uvuvi Wilaya na wananchi ambao wanachukia suala la Uvuvi haramu.
Katika kudhibiti matumizi ya zana haramu za Uvuvi Mkoani Kagera jumla ya doria 65 zimefanyika kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2016 hadi Juni, 2017 na hivyo kuwezesha kukamatwa zana haramu za Uvuvi ambazo ni kokoro za sangala 422, nyavu ndogo za dagaa 57, nyavu za timba 3,231, nyavu za makila 14,141, katuli 16, Ndoano 712 mitumbwi 133 na samaki wachanga wenye uzito wa kg 3,330 ambazo kwa ujumla zilikuwa na thamani ya Tshs Bilioni 1,602,860,500 kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali namba 4. Pia watuhumiwa 86 walikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.
Aidha watendaji wote wa Vijiji na Mitaa wameandikiwa barua zenye maagizo yanayolenga kudhibiti vitendo vyote vya matumizi ya zana haramu za Uvuvi kuanzia ngazi ya Vijiji/Mitaa na kuhakikisha kuwa wavuvi haramu wanasalimsha zana zao haramu za Uvuvi kwa hiari. Zoezi hili linaenda vizuri ambapo hadi kufikia mwezi Juni 30, 2017 wavuvi 43 wamesalimisha zana haramu za Uvuvi walizokuwa wakizitumia kwa shughuli za Uvuvi na wengine waliokaidi walikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Pia vikundi vyote vya usimamizi wa raslimali za Uvuvi (BMU) vimeagizwa kutekeleza Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003 katika mialo.
Jedwali Na. 8: Takwimu ya Zana Haramu za Uvuvi zilizokamatwa
WILAYA
|
Idadi ya Doria
|
IDADI YA ZANA HARAMU ZILIZOKAMATWA
|
|
Samaki Wachanga (Kg)
|
Watuhumiwa
|
||||||
Kokoro za sangala
|
Nyavu ndogo za dagaa
|
Nyavu za Timba
|
Nyavu za makila |
Kimea (Cast net)
|
Ndoano
|
Katuli
|
Mitumbwi
|
||||
BUKOBA (M)
|
4
|
18
|
0
|
243
|
728
|
0
|
0
|
6
|
32
|
607
|
2
|
BUKOBA (W)
|
24
|
43
|
29
|
63
|
169
|
0
|
0
|
0
|
8
|
3,236
|
3
|
MULEBA
|
69
|
379
|
188
|
3,327
|
3,173
|
0
|
0
|
0
|
129
|
10,694
|
93
|
MISSENYI
|
3
|
18
|
4
|
160
|
190
|
0
|
0
|
0
|
28
|
600
|
4
|
KYERWA
|
25
|
0
|
0
|
146
|
750
|
0
|
720
|
8
|
30
|
1,450
|
15
|
KARAGWE
|
6
|
4
|
0
|
250
|
290
|
0
|
100
|
3
|
8
|
28
|
9
|
JUMLA
|
131
|
462
|
221
|
4,189
|
5,300
|
0
|
820
|
17
|
235
|
16,615
|
126
|
N.B: Wilaya za Biharamulo na Ngara hazipakani na Ziwa Victoria hivyo hakuna shughuli za Uvuvi ziwani bali ufugaji wa samaki kwenye mabwawa.
Mkoa wa kagera una jumla ya viwanda vitatu ambapo viwanda viwili ni vya kusindika minofu ya samaki na kiwanda kimoja cha kuchakata mapanki na kutengeneza soseji za samaki. Viwanda hivi ni kiwanda cha Kagera Fish Company kilichoanza kazi mwezi Oktoba 2003, Kiwanda cha VICFISH Co. Ltd kilichoanza uzalishaji Juni 2005 na kiwanda cha Mapanki Company Limited. Mkoa wa Kagera umeendelea kuhakiki viwango vya ubora na usalama wa mazao ya Uvuvi kwenye viwanda, masoko na maghala ya kuhifadhi mazao ya Uvuvi ambapo jumla ya kaguzi 167 zimefanyika ikiwa ni pamoja na kuangalia ubora na usalama wa samaki kabla ya kusafirishwa kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi. Matokeo ya kaguzi hizo yalionesha kukidhi viwango vya ubora wa samaki.
Jedwali Na. 9: Takwimu zaViwanda vya Kuchakata Samaki
Na
|
Jina La Kiwanda
|
Uzalishaji Kwa Siku (Tani)
|
Uwezo Wa Kiwanda (Tani/Siku)
|
Aina Ya Samaki
|
Mahali Kilipo
|
01.
|
Kagera Fish Company Ltd
|
2
|
20
|
Sangala
|
Bukoba (W), Kemondo
|
02.
|
Supreme Perch Co. Ltd
|
15
|
60
|
Sangala
|
Bukoba (M)
|
03.
|
Mapanki Company Limited
|
1
|
10
|
Sangala
|
Bukoba (W)
|
Mkoa wa Kagera una jumla ya masoko na magulio ya samaki119. Wastani wa bei ya samaki aina ya sangala wabichi kwa kilo ni shilingi 6,200/=, 6,600/= sato wabichi, 3,000/= dagaa wabichi na shilingi 90,000/= kwa mabondo ya sangala. Mkoa wa Kagera umeendelea kuratibu na kusimamia miundombinu ya masoko ya mazao ya Uvuvi kwa kufanya kaguzi kwenye masoko makubwa na madogo ya Samaki yaliyopo Manispaa ya Bukoba, Muleba, Bukoba vijijini, Missenyi, Kyerwa, Ngara, Karagwe na Biharamulo. Pia ukaguzi umefanyika kwenye masoko madogo katika maeneo ya vijijini, mjini na katika mialo ya Ziwa Victoria, maziwa madogo (Satelite lakes) na mito. Mkoa unawawezesha wavuvi na wafanyabiashara halali juu ya soko la samaki kwa kuwepo viwanda vitatu ambavyo ni VIC-Fish, Kagera Fish na Kiwanda cha Mapanki Co. Ltd ambao hununua samaki aina ya sangara kwa uhakika, hivyo kuwawezesha wananchi kupata kipato na kuwainua kiuchumi.
Jedwali Na. 10: Takwimu za bei ya samaki Mkoa wa Kagera
NA
|
WILAYA
|
Idadi Ya
Masoko/ Magulio |
WASTANI WA BEI YA SAMAKI KWA KILO (Tshs/Kg)
|
|||||||
Sangala (kg)
|
Sato (kg)
|
Dagaa (kg)
|
Samaki wengine (kg)
|
|||||||
Bichi
|
Kavu
|
Bichi
|
Kavu
|
Bichi
|
Kavu
|
Bichi
|
Kavu
|
|||
1
|
Bukoba (M)
|
4 |
5,500 |
4,500 |
7,500 |
0 |
1,500 |
2,500 |
5,000 |
8,000 |
2
|
Bukoba (W)
|
5 |
6,000 |
7,500 |
8,500 |
9,000 |
1,500 |
2,500 |
4,000 |
1,500 |
3
|
Muleba
|
56 |
6,000 |
5,000 |
5,000 |
6,000 |
3,000 |
4,000 |
2,000 |
3,500 |
4
|
Missenyi
|
7 |
5,500 |
5,000 |
7,000 |
10,000 |
4,000 |
5,000 |
3,500 |
4,000 |
5
|
Kyerwa
|
35 |
0 |
10,000 |
5,000 |
12,000 |
0 |
8,000 |
1,600 |
7,000 |
6
|
Karagwe
|
12 |
8,000 |
10,000 |
7,000 |
10,000 |
5,000 |
9,000 |
5,000 |
8,000 |
|
WASTANI
|
119 |
6,200 |
7,000 |
6,600 |
9,400 |
3,000 |
5,100 |
3,500 |
5,300 |
KatikaMkoa wa Kagera jumla ya BMU’s 93 zimeundwa kwa sheria ya Uvuvi Na. 22 yaMwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009ambapo Manispaa ya Bukobakuna BMU 5, Wilaya ya BukobaVijijini BMU’s 11, Wilaya ya Muleba BMU’s 70Wilaya ya Missenyi BMU’s 2na Karagwe BMU’s 5. Baadhi ya BMU zimetoa mchango mkubwa katika ulinzi wa rasilimali ya Uvuvi katika mialo mbalimbali, ingawa zipo BMU’s chache zinazofanya vibaya kwa sababu kadhaa, kwa kuwepo BMU’s shughuli zifuatazo zimefanyika.
7.0 UTEKELEZAJI WA MIRADI MBALIMBALI |
Hadi kufikia mwezi Juni 2018, Mkoa wa Kagera umetekeleza miradi mbalimbali kwa lengo la kuendeleza Sekta ya Uvuvi na ufugaji wa samaki ili kuwaletea maendeleo wananchi hasa wavuvi na wafugaji wa samaki. Baadhi ya miradi hiyo imefadhiliwa na Serikali na mingine imetekelezwa kwa ufadhili wa mashirika yasiyo ya kiserikali zikiwemo Ngo’s. Ifuatayo ni baadhi ya miradi iliyotekelezwaMkoani Kagera.
Jedwali Na. 11: Takwimu za miradi mbalimbali Mkoa wa Kagera
Na
|
WILAYA
|
AINA YA MRADI
|
UFADHILI
|
UTEKELEZAJI
|
1
|
Bukoba (M)
|
Kujenga banda la kupokelea samaki kisiwa cha nyabesiga.
|
DADP’S
|
Mradi umekamilika
|
2
|
Bukoba (W)
|
Ujenzi wa Vizimba (Cages) kwa ajili ya ufugaji wa samaki Ziwa Victoria.
|
UNDP, ESRF na JKT
|
Mradi umekamilika.
|
3.
|
Muleba
|
Ununuzi wa boti 1 (fibre boat) kwa ajili ya doria ya shughuli za uvuvi.
|
H/Wilaya
|
Mradi umekamilika
|
Ujenzi wa jengo la kupokelea samaki mwalo wa Katembe.
|
H/Wilaya
|
Mradi umekamilika
|
||
4
|
Missenyi
|
Ujenzi wa karo la kupokelea na kupimia samaki mwalo wa Kabindi na Kaishebo
|
LVEMP II
|
Mradi umekamilika
|
Ujenzi wa mwamba wa kuanika dagaa mwalo wa kibindi.
|
LVEMP II
|
Mradi umekamilika
|
||
5.
|
Karagwe
|
Kuwezesha vikundi vya kufuga samaki kwa kuchimba mabwawa 2
|
World Vision
|
Mradi umekamilika
|
Kudhibiti magugu maji katika mto kagera, Ziwa Rwakajunju kijiji Kafunjo
|
H/Wilaya na LVEMP II
|
Mradi umekamilika.
|
||
6
|
Kyerwa
|
Hakuna mradi
|
Hakuna
|
Hakuna
|
7.
|
Ngara
|
Kuchimba mabwawa 79 ya kufuga samaki kata ya Mugoma, Bugarama, Rulenge, Bukiriro, Ngara mjini na Ntobeye.
|
CHEMA, TCRS,
TASAF,
|
Mradi umekamilika
|
8
|
Biharamulo
|
Hakuna mradi
|
Hakuna
|
Hakuna
|
8.0 UWEZESHAJI WAVUVI WADOGO |
Serikali imeendelea kuwawezesha wavuvi wadogo kwa kufuta baadhi ya tozo, kutoa ruzuku na kuboresha miundombinu ya Uvuvi ambapo jumla ya Vikundi 9 vimewezeshwa kwa kupewa ruzuku na mikopo ya shughuli za Uvuvi katika Mkoa wa Kagera. Pia Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri imesimamia vyema shughuli za Uvuvi na kutoa ulinzi kwa kufanya kaguzi katika maeneo ya Uvuvi. Usimamizi na uhamasishaji umewezesha kuanzishwa kwa Vyama vya Ushirika wa Wavuvi 7, BMUs 93 pamoja na vikundi vya wavuvi wadogo wadogo 6 katika Mkoa wa Kagera.
9.0 UTEKELEZAJI WA MPANGO WA NCHI WANACHAMA WA ZIWA VICTORIA |
Mkoa wa Kagera umetekeleza mpango kazi wa kanda wa nchi wanachama kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na nchi za jirani katika mapambana ya kudhibiti Uvuvi haramu, kuboresha uratibu wa shughuli za Uvuvi na doria. Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya tumekuwa tukiendesha shughuli za doria katika maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria katika mialo yote ya Mkoa wa Kagera na dhana haramu za Uvuvi zimekamatwa.
10.0 KUELIMISHA JAMII JUU YA ATHARI ZA UVUVI HARAMU NA UKIMWI |
Katika kuhakikisha Uvuvi haramu unakomeshwa na kuwafanya wavuvi kufanya Uvuvi endelevu, wataalamu wa Uvuvi Mkoa wa Kagera wamekuwa wakitoa elimu juu ya matumizi bora ya zana za Uvuvi zinazokubalika kisheria na kuwaelimisha wavuvi kufanya Uvuvi endelevu ili kulinda rasilimali za majini kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho.Kwa kipindi chaMwaka wa fedha 2017/2018kuanzia mwezi Julai2017hadi Juni, 2018 njia zifuatazo zimekuwa zikitumika kutoa elimu kwa jamii ya wavuvi juu ya Uvuvi haramu na maambukizi ya VVU/UKIMWI.
11.0 MAFANIKIO YALIYOPATIKANA |
Kwa kipindi cha Mwaka wa fedha 2017/2018, Sekta ya Uvuvi Mkoa wa Kagera imepata mafanikio mengi ikiwa ni pamoja na kudhibiti Uvuvi haramu ili kulinda raslimali ya Uvuvi. Hatua mbalimbali za kisheria zimechukuliwa katika kuzuia Uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na wahalifu kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na wengine kupewa onyo kali. Aidha, jumla ya doria 131 zimefanyika kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2017 hadi Juni 30, 2018 na hivyo kuwezeshwa kukamatwa zana haramu za Uvuvi ambazo ni kokoro za sangala 462, nyavu ndogo za dagaa 221, nyavu za timba 4,189, nyavu za makila 5,300, katuli 17, Ndoano 820 mitumbwi 235, samaki wachanga wenye uzito wa kg16,615 na watuhumiwa 126.
Sambamba na hilo Sekta ya Uvuvi inachangia kwa kiasi kikubwa katika kutoa ajira ambapo zaidi ya wananchi26,830 wameajiriwa au kujiajiri kutokana na Shughuli za Uvuvi Mkoani Kagera. Pia katika uchumi kwa kipindi cha Mwaka wa fedha 2017/2018 kuanzia Mwezi Julai 2017 hadi Juni 2018 jumla ya tani 4,651.8 za samaki zenye thamani ya Tshs Bilioni 27.75, zilivuliwa katika Ziwa Victoria, maziwa madogo madogo (Satellite Lakes) na kwenye mabwawa ya kufugia Samaki yaliyopo Mkoani Kagera.
Pia miradi mbalimbali imetekelezwa Mkoani Kagera ambayo ni miradi ya ufugaji bora wa samaki, miradi ya ujenzi wa vyoo na maeneo ya kupokelea samaki kwenye mialo, miradi ya kudhibiti magugu maji katika Ziwa Victoria, Mto Kagera na maziwa madogo madogo yaliyopo Mkoa wa Kagera. Aidha, jumla ya Shilingi Bilioni1,860,593,416/= zimekusanywakutokana na ada za leseni za Uvuvi na vibali vya kusafirisha samaki, tozo za faini, ushuru, maduhuli na makusanyo mengine ambayo ni sawa na asilimia 128.9 ya malengo yaliyowekwayakukusanyakiasi cha shilingi 1,443,423,000/= kwa Mwakawa fedha 2017/2018 katika Mkoa wa Kagera.
Sambamba na hilo, mwanya wa kutorosha mazao ya Uvuvi kwenda nchi jirani umedhibitiwa kwa kutumia vizuizi vilivyopo mipakani maeneo ya Kyaka na Kashenye Wilaya ya Missenyi, Bugabo na Rubafu Wilaya ya Bukoba vijijini pamoja na Vituo vitano ambavyo ni Bukoba, Rusumo, Kabanga na Murusagamba Wilaya ya Ngara naKanyigoWilaya ya Missenyi.
Mafanikio mengine ni kuendeleza Ukuzaji viumbe hai kwenye maji (aquaculture) ambapo jumla ya mabwawa 619 yamechimbwa katika Mkoa wa Kagera na kupandikizwa vifaranga bora vya samaki pamoja na wananchi kuelimishwa mbinu za Ufugaji bora wa samaki.
Pia tumefanikiwa kulinda mazingira na kuendeleza uhifadhi wa Ziwa Victoria, Mito, maziwa madogo madogo(Satelite Lakes) na maeneo tengefu ambayo shughuli za Uvuvi zinafanyika ikiwa ni pamoja na kulinda Viumbe hai vilivyomo majini kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
12.0 CHANGAMOTOZILIZOPO |
Pamoja na mafanikio yaliyopo Sekta ya Uvuvi ina changamoto zifuatazo:-
13.0 Mkakati wa Kutatua Changamoto zilizopo |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa