- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
LENGO LA SEHEMU YA MIUNDOMBINU
|
Kuwezesha utoaji wa ushauri wa kitaalam katika maendeleo ya miundombinu kwa Halmashauri
Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-
SEKTA ZA MIUNDOMBINU (ARDHI, BARABARA, MAJI, ANGA, NISHATI NA MADINI)
|
SEKTA YA ARDHI
|
Upimaji wa Viwanja na Mashamba na Umilikishaji |
Kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi kufikia Septe,mba 12, 2018 viwanja vilivyopimwa ni 14,171 (Bukoba Manispaa 9,991 Bukoba Vijijini 179, Biharamulo 101, Karagwe 832, Ngara 194, Missenyi 859, Muleba 792 na Kyerwa viwanja 1,203) na jumla ya viwanja 4,014 vimemilikishwa kwa wananchi.
Adha, upimaji wa mashamba yenye ukubwa wa hekta 6,613.522 yameweza kupimwa hadi Juni, 2018 (Bukoba Vijijini hekta 67.15, Karagwe hekta 1,877.565, Ngara hekta 776.222, Missenyi hekta 4,204.294, Muleba hekta 14.761 na Kyerwa hekta 36.689).
Matumizi Bora ya Ardhi |
Mkoa una jumla ya vijiji 667 kati ya hivyo Vijiji 535 vimepimwa na Vijiji 132 havijapimwa. Mipango ya matumizi bora ya ardhi imeandaliwa katika Vijiji 68 na jumla ya mashamba 11,213 yameweza kupimwa na hati 5,523 kutolewa kwa wananchi (Bukoba hati 207, Missenyi ni mashamba 566 na hati 566, Karagwe ni mashamba 3,238 na hati 2,100, Ngara ni Mashamba 4,138 na hati 2001 na Muleba ni mashamba 3,271 na hati 649).
Uboreshaji wa Makazi. |
Michoro ya mipango miji ipatayo 345 imeandaliwa katika maeneo ya mijini na vituo vya kibiashara katika maeneo mbalimbali ya halmashauri kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi kufikia mwezi Aprili, 2018 (Muleba Michoro ya mipango miji 65, Missenyi 19, Ngara 9, Bukoba 22, Manispaa ya Bukoba 128, Biharamulo 39, Kyerwa 32 na Karagwe 31).
Miji ya Mutukula, Kyaka-Bunazi na Kyerwa katika halmashauri za wilaya za Missenyi na Kyerwa imeweza kutangazwa katika gazeti la serikali kama maeneo ya mpango (Planning Area).
Mabaraza ya Ardhi
|
Kufuatia hali ya kuwa na migogoro mingi ya ardhi katika Mkoa wetu, Serikali iliona ni vyema kuwa na Mabaraza karibu ili yaweze kutatua migogoro, katika Wilaya zilizo na migogoro mingi ni Wilaya ya Muleba ambapo Baraza lilizinduliwa tarehe 19 Agosti, 2016, Wilaya nyingine ni Bukoba na Karagwe, hata hivyo Wizara ilishachukua hatua ya kufungua Mabaraza ya Ardhi na Nyumba katika Wilaya ya Muleba, Karagwe na Ngara.
SEKTA YA BARABARA
|
Mkoa una jumla ya kilometa 7,827.24 za barabara ikiwemo kilometa 5,909.65 zilizo chini ya Halmashauri za Wilaya na Manispaa (TARURA), Kilometa 1,917.59 za Barabara Kuu na za Mkoa zilizo chini ya TANROADS. Kati ya hizo kilometa 674.05 ni barabara za lami, kilometa 2,805.16 ni barabara za changarawe na kilometa 4,348.03 ni barabara za udongo.
Na.
|
Aina Ya Barabara
|
Lami (Km) |
Changarawe (Km) |
Jumla (Km) |
1
|
Barabara Kuu
|
551.22 |
311.66 |
862.88 |
2
|
Barabara za Mkoa
|
84.60 |
970.11 |
1054.71 |
Jumla
|
635.82 |
1281.77 |
1917.59 |
Mtandao wa Barabara Kuu na za Mkoa
Hali ya Barabara Kuu na Barabara za Mkoa
|
Kwa kiasi kikubwa hali ya barabara Mkoani Kagera ziko katika hali nzuri kwa barabara zote isipokuwa barabara ya Rusumo – Lusahunga ambayo imeisha muda wake, hivyo kunahitajika Ukarabati mkubwa (Rehabilitation). Aidha barabara chache hupitika kwa taabu wakati wa mvua nyingi hasa sehemu zenye miinuko mikali.
Hali ya Barabara hizi wakati wa masika zinapitika kwa asilimia 95, wakati wa kiangazi zinapitika kwa asilimia 100 na wakati wote wa mwaka zinapitika kwa asilimia 98. Asilimia hizo 2 zinatokana na sehemu chache korofi za barabara kuu ya lami ya Rusumo – Lusahunga ambayo imechakaa na kuhitaji ukarabati mkubwa na sehemu chache za barabara za Mkoa zenye miinuko.
Miradi Mikubwa ya Maendeleo ya Barabara Mkoani
|
Baadhi ya Miradi mikubwa ya barabara inayotekelezwa hapa mkoani ya Barabara Kuu ni kama ifuatayo;-
Na
|
Jina la Mradi
|
Tarehe ya Kuanza
|
Gharama Tshs.
|
Mkandarasi
|
Mhandisi Msimamizi
|
Utekelezaji
|
1
|
Ukarabati wa Barabara ya Ushirombo- Lusahunga (110Km) Kagera ni Km 52
|
18/02/2010
|
114,556,919,193
|
MS Strabag International GmbH
|
M/S Smec International (Pty) Ltd
|
53.29%
|
2
|
Ujenzi wa Barabara ya Bwanga- Biharamulo (Km 67)
|
28/12/2012
|
57,755,740,000
|
M/S Sinohydro Ltd Works Ltd
|
M/S Tanroads Engineering Consulting Unit
|
68%
|
3
|
Ujenzi wa Barabara ya Nyakanazi – Kidahwe (Km 50)
|
13/06/2014
|
45,985,780,766.87
|
M/S Nyanza Road Works Ltd
|
M/S Intercontinental Consultants and Technocrats Pvt Ltd
|
36.33%
|
4
|
Ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi (ONE STOP INSPECTION STATION) – OSIS Nyakanazi
|
15/05/2017
|
Euro
9,582,090.10
|
M/S Impressa si Contruzioni Ing. E Montavani S.p.a con socio unico of Italy
|
M/S Trade Mark East Africa (TMEA) and M/S NimetaConsults (T) Ttd
|
1.2%
|
Aidha, ipo miradi inayosimamiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kupitia mradi wa ULGSP chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia wa uboreshaji miji. Barabara hizi zimeanza kujengwa mwaka huu wa fedha 2018/2019 kwa kiwango cha rami nzito na utagharimu billion 7.03, barabara hizi ni zifuatazo;-
Bajeti ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2018/19
|
Bajeti ya matengenezo ya barabara toka fedha za Mfuko wa Barabara kwa Mkoa wa Kagera kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika barabara Kuu na Barabara za Mkoa ni shilingi bilioni 14,239,917,000. Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 5,734,437,000 ni za matengenezo ya barabara Kuu na shilingi bilioni 8,505,480,000 ni za matengenezo ya barabara za Mkoa. Bajeti ya maendeleo kwa ajili ya matengenezo ya barabara ni shilingi bilioni 9,285,000,000.
Barabara zinazosimamiwa na TARURA
|
Mkoa wa Kagera una jumla ya Kilometa 6,137.20 za barabara zilizo chini ya Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba ambazo zinasimamiwa na TARURA.
Mtandao wa Barabara zilizo chini ya TARURA Mkoani Kagera
Na
|
Mamlaka
|
Lami (Km) |
Changarawe (Km) |
Udongo (Km) |
Jumla (Km) |
1
|
Biharamulo
|
- |
106.00 |
317.55 |
423.55 |
2
|
Bukoba Vijijini
|
0.35 |
252.45 |
246.70 |
499.50 |
3
|
Bukoba Manispaa
|
27.20 |
35.70 |
66.60 |
129.50 |
4
|
Karagwe
|
4.30 |
322.60 |
1,044.60 |
1,371.50 |
5
|
Kyerwa
|
- |
198.90 |
524.60 |
723.50 |
6
|
Missenyi
|
1.00 |
219.00 |
504.90 |
724.90 |
7
|
Muleba
|
- |
139.52 |
1,265.48 |
1,405.00 |
8
|
Ngara
|
3.80 |
250.80 |
377.60 |
632.20 |
Jumla Kuu
|
36.65 |
1524.97 |
4,348.03 |
5,909.65 |
Aaidha, TARURA kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 imetengewa kiasi cha Tsh. 10,152,737,884.68 kwa ajili ya matengenezo ya barabara zilizopo chini yake katika Halmashauri za Mkoa wa Kagera.
USAFIRI WA MAJI
|
Usafiri wa Majini umeendelea kuwa kikwazo cha Maendeleo ya Mkoa wa Kagera, Meli ya MV Victoria ilisitisha huduma zake baada ya kuharibika na inafanyiwa matengenezo makubwa Jijini Mwanza. Meli ya MV Serengeti imekuwa haifanyi kazi vizuri na mara ya mwisho kuwa safarini ni mwezi Machi, 2016.
Bandari ya Bukoba |
Bandari ya Bukoba ni moja katika vituo vinavyounda Bandari ya Mwanza ambayo ndio makao makuu. Bandari hii inatoa huduma kwa abiria na mizigo ya kwenda na kutoka Mwanza na Nchi jirani kutokea Bandari ya Kisumu kwa Nchi ya kenya na Bandari ya Portbell kwa Nchi ya Uganda.
Kwasasa hivi zipo meri za mizigo kutoka Mwanza na kwa mwezi bandari hupokea wastani wa tani 113 na kwa mwaka ni wastani wa tani 1356 za mizigo. Julai, 2018 bandari imepokea mizigo kutoka Uganda tani 461 zenye bidhaa za madukani. Aidha meri za mizigo zinazotoka mwanza hupeleka wastani wa tani 2,600 za sukari Mwanza kila mwezi
Miundombinu na Vifaa vya Bandari Bukoba |
Bandari ya Bukoba ina miundombinu na vifaa vifuatavyo;-
Gati mbili kwa ajili ya meli za mizigo na abiria; moja ikiwa na urefu wa mita 82 ambayo hutumika kuegesha meli za mizigo; gati ya pili ina urefu wa mita 70 hii hutumika kuegesha meli za abiria.
Maghala mawili yenye uwezo wa kuhifadhi tani 500 za mizigo, sehemu ya kupakua/kupakia mafuta (oil jetty) ambayo kwa sasa haitumiki, jengo la abiria ambalo hutumika na abiria wanaposubiri kupanda melini.
USAFIRI WA ANGA
|
Kiwanja cha Ndege Bukoba
|
Kiwanja cha Ndege Bukoba ni miongoni mwa viwanja 58 vinavyo simamiwa na kuendeshwa na Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Viwanja vingine vilivyo katika Mkoa wa Kagera na vinasimamiwa na Mamlaka ni Biharamulo kikiwa chini ya usimamizi wa Meneja wa kiwanja cha Ndege cha Bukoba. Aidha kipo kiwanja kingine cha Ngara ambacho kutokana na sababu za kijiographia kinasimamiwa na Meneja wa kiwanja cha ndege cha Mwanza.
Kiwanja cha Ndege Bukoba inasemekana kilijengwa miaka ya sitini (1960). Kwa kipindi hicho ujenzi ulikuwa ni wa kiwango cha changarawe na kilikuwa na njia ya kurukia na kutua ndege chenye Urefu wa Mita 1,200 na upana wa mita 20.
Kiwanja hiki kimefanyiwa maboresho katika awamu mbili; awamu ya kwanza yalifanyika marekebisho makubwa ambayo yaliyohusisha kazi ya kuongeza urefu wa njia ya kuruka na kutua ndege kutoka mita 1,200 na kufikia mita 1,700 kwa kiwango cha changarawe (Cement stabilization) kuanzia Mwanzoni mwa mwaka 2009 na kukamilika 2011.
Maboresho ya awamu ya pili yaliyoanza mwanzoni mwa mwaka 2013, yalihusisha upanuzi wa upana wa njia ya kuruka na kutua ndege toka mita 20 na kufikia upana wa mita 30 kwa kiwango cha Lami (alsphat) ikihusisha Ujenzi wa jengo la abiria la kisasa lenye uwezo wa kuchukua abiria 150 kwa saa, uboreshaji wa Mitaro ya maji, (Airside drainage System) Ujenzi wa uzio mpya wa usalama kiasi cha mita 1,200 na ujenzi wa eneo la maegesho (Apron) lenye kuweza kuegesha ndege nne kwa wakati mmoja tofauti na eneo la awali lenye uwezo wa kuegesha ndege moja ndogo.
Kiwanja cha Ndege cha Biharamulo kilijengwa miaka ya 1950 kwa ajili ya matumizi ya wamisionari na kilikabidhiwa Serikalini baada ya vita vya Tanzania na Uganda mnamo mwaka 1979. Kina urefu wa mita 935 na upana wa mita 18 na ni cha kiwango cha nyasi, kina jengo moja tu linalotumika kwa shughuli za utawala na abiria. Jengo hilo lina uwezo wa kuhudumia abiria 40 kwa saa.
Kwa hiyo Mkoa wa Kagera unavyo viwanja vitatu ambavyo ni Bukoba, Ngara na Biharamulo vinavyoendeshwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.
Hali ya Miundombinu ya Kiwanja cha Ndege Bukoba
|
Kiwanja cha Ndege Bukoba kina barabara mbili za kutua na kuruka ndege (“Runways”). Barabara hizo zina urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30, njia hizi huitwa 13/31, njia hizi za kuruka Ndege ndio zinazotumika hivi sasa. Kiwanja hiki hakina taa za kuongozea ndege nyakati za usiku hivyo huduma za kiwanja hiki ni muda wa mchana pekee yaani (sunrise and sunset operations). Aidha kiwanja hiki kina maeneo mawili ya maegesho ya ndege “Apron” ambayo ni ya lami, eneo la maegesho la zamani lenye uwezo wa kuegesha ndege 1 aina ya ATR 42 na eneo la maegesho kuu la jengo Jipya lina uwezo wa kuegesha ndege 2 aina ya ATR 42 na ndege mbili aina ya Caravan.
Pia kiwanja kina jengo la abiria la kisasa (Terminal building) moja la kuhudumia abiria na ukumbi wa watu mashuhuri (VIP). Ukumbi wa abiria wanaoondoka una uwezo wa kubeba abiria 150 kwa wakati mmoja na ukumbi wa abiria wanao wasili unauweza wa kuhudumia abiria 100, hivyo kuwa kiwanja chenye kiwango cha daraja la 3C (aerodrome code). Kiwanja cha ndege Bukoba kinapata huduma ya Usalama wa waongoza ndege kutoka Mwanza Control Tower.
Safari za Ndege na Abiria Kiwanja cha Ndege Bukoba
|
Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, kumekuwa na ongezeko la safari za ndege kutoka miruko ya ndege 1,957 kwa mwaka 2012 hadi kufikia miruko 2,706 mwaka 2016 sawa na ongezeko la asilimia 38.3. Aidha idadi ya abiria kwa mwaka 2012 ilianza kuongezeka kutoka abiria 29,736 hadi 33,128 kwa mwaka 2016 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 11.42. Kwa mwaka 2017/2018 miruko ya ndege ni 1810 ikionyesha kupungua kwa miruko lakini pia kukiwa na ongezeko la abiria hadi 47,959 sawa asilimia 18.2
NISHATI
|
Mkoa wa Kagera una jumla ya wateja waliounganishiwa umeme 64,453 ambapo kati yao, wateja wa LUKU ni 61,562 na wateja wa kulipia baada ya matumizi ni 2,891.
Kutokana na idadi ya wateja tulionao hadi sasa (64,453), wananchi 484,992 tayari wanafaidi huduma ya umeme moja kwa moja, ambacho ni takribani asilimia 17.2% ya wananchi wote wa Mkoa wa Kagera.
Mahitaji ya juu ya umeme kwa Mkoa sasa yamefika MW 20.1 (Bukoba 6.4 MW kutoka grid ya Uganda, Missenyi 6.3 MW kutoka grid ya Uganda, Karagwe 2.2 MW kutoka grid ya Uganda, Muleba 2.9 MW kutoka grid ya Uganda, Biharamulo 1.2MW kutoka grid ya Taifa na nguvu ya mafuta “generator” na Ngara 1.1 MW kutokana na nguvu ya mafuta “generator”
Upatikanaji wa Nishati ya Umeme
|
Mkoa wa Kagera kwa sasa unapata umeme kutoka vyanzo vikuu vitatu kama ifuatavyo:-
Umeme Kutoka Shirika la Umeme la Uganda
Umeme kutoka nchi jirani ya Uganda kupitia laini kubwa ya msongo wa kilovolti 132 (132 Kv).
Umeme Kutoka Gridi ya Taifa
Wilaya ya Biharamulo inapata umeme wa Grid ya Taifa kwa msongo wa kilovoti 33 (33 Kv) kutokea Mkoa wa Geita.
Umeme wa Nguvu ya Mafuta
Wilaya ya Biharamulo, licha ya kuwa na umeme wa Gridi ya Taifa, pia ina mitambo ya kufua umeme yenye uwezo wa megawati 2.5 (2.5 MW). Mitambo hii huwashwa kwa dharura pale inapobidi. Wilaya ya Ngara kwa sasa ina chanzo kimoja tu cha umeme, nacho ni mitambo ya kufua umeme yenye uwezo wa megawati 2.5 (2.5 MW).
Miradi ya Umeme
|
Miradi ya Kufua Umeme
|
Mkoa ulikuwa na miradi mitatu (3) ya kufua umeme ipo kwenye hatua za awali za utekelezaji ambayo yote kwa pamoja ikikamilika itaweza kuongeza uwezo wa upatikanaji wa umeme katika Mkoa, na ziada kutumika katika maeneo mengine kupitia Gridi ya Taifa pindi itakapokamilika.
Mchanganuo wa Miradi hiyo ni kama ifuatavyo
Jina la Mradi
|
Chanzo
|
Eneo
|
Uwezo |
Hatua ya Utekelezaji |
Rusumo
|
Nguvu ya Maji
|
Ngara
|
80 MW |
Uko hatua za awali |
Kakono
|
Nguvu ya Maji
|
Missenyi
|
53 MW |
Uko hatua za awali |
Murongo/Kikagati
|
Nguvu ya Maji
|
Kyerwa
|
16 MW |
Uko hatua za awali |
Kukamilika kwa miradi hii kutaondoa kabisa uhitaji wa Shirika na Nchi yetu kununua umeme kutoka nchi jirani ya Uganda ili kuhudumia Mkoa huu.
Miradi ya Kusafirisha Umeme
|
Mradi wa kuunganisha Mkoa kwenye Gridi ya Taifa kupitia ujenzi wa line ya msongo wa kilovolti 220 kutoka Geita kupitia Runzewe mpaka Nyakanazi kama awamu ya kwanza. Mradi huu upo kwenye hatua za awali na Mhandisi Mshauri amekwisha patikana. Awamu zitakazofuata muda mfupi baadaye zitahusisha ujenzi wa laini ya msongo wa kilovoti 220kutoka Nyakanazi mpaka Rusumoa na BENACO (Ngara) hadi Kyaka (Missenyi).
Kukamilika kwa miradi hii kutaimarisha zaidi upatikanaji wa umeme katika maeneo yote ya Mkoa wa Kagera bila kutegemea umeme kutoka nchi jirani.
Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)
|
Mradi wa REA Awamu ya tatu Mzunguko wa Kwanza (Round-1) ulifunguliwa tarehe 11 Julai, 2017 ambao unahusisha;-
Ujenzi wa Km 299.01 wa laini za 33KV
Ujenzi wa Km 574 wa laini za LV
Ujenzi wa Transfoma 287
Uunganishaji wa Wateja 9,136 katika Vijiji 141.
Mawanda ya Mradi
|
Mradi wa REA (REA III ROUND I) unatarajiwa kujenga laini ya msongo wa kilovolt 33 yenye urefu wa kilomita 299.01, laini ndogo yenye msongo wa volt 230/400 yenye urefu wa kilomita 574 na kunufaisha jumla ya Vijiji 143 na jumla ya wateja 9,141 (ikiwa wateja 8,226 wa njia moja na wateja 916 wa njia tatu) watanufaika wa Mkoa wa Kagera.
Mradi huu utagharimu kiasi cha takribani (Tshs. Bilioni thelathini na nane nukta tano) 38,499,922,525.73/= Chini ni jedwali linaloonyesha mchanganuo wa usambazaji wa umeme kwa kila Wilaya na Idadiya Vijiji vitakavyounganishwa, ikionyesha urefu wa laini, transfom na Idadi ya Wateja watakaounganishwa katika mzunguko wa kwanza wa (REA III Round I)
Jedwali Na. 27: Mawanda ya Mradi wa REA III
NA. |
WILAYA |
IDADI YA VIJIJI |
UREFU WA LAINI KUBWA |
UREFU WA LAINI NDOGO |
TRANSFOMA |
WATEJA TARAJIWA |
JUMLA |
|||||||||
50 KVA |
100 KVA |
NJIA MOJA |
NJIA TATU |
|||||||||||||
1. |
Ngara
|
21 |
52.64 |
100 |
50 |
0 |
1541 |
171 |
1712 |
|||||||
2. |
Missenyi
|
14 |
26.37 |
36 |
18 |
0 |
468 |
52 |
520 |
|||||||
3. |
Kyerwa
|
22 |
47.36 |
94 |
47 |
0 |
1296 |
144 |
1440 |
|||||||
4. |
Muleba
|
21 |
9.02 |
78 |
39 |
0 |
1061 |
118 |
1179 |
|||||||
5. |
Bukoba
|
23 |
51.58 |
98 |
48 |
1 |
1361 |
153 |
1514 |
|||||||
6. |
Biharamulo
|
21 |
75.31 |
92 |
42 |
4 |
1414 |
157 |
1571 |
|||||||
7. |
Karagwe
|
21 |
36.73 |
76 |
36 |
2 |
1084 |
121 |
1205 |
|||||||
Jumla ya Wigo |
143 |
299.01 |
574 |
280 |
7 |
8225 |
916 |
9141 |
||||||||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Kazi inayotekelezwa kwa sasa
|
Hadi hivi sasa Mkandarasi amefanya kazi ya kupima njia ya Miundombinu ya umeme ili kuwafikia wateja, kazi ambayo imefikia asilimia 100 (100%) kwa Vijiji vyote na hivi sasa ameanza kusimamisha nguzo katika maeneo mbalimbali. Aidha tayali vijiji vitatu (4) vimewashiwa umeme kama ifuatavyo;-
Jedwali Na. 28: Kazi Iliyotekelezwa Hadi Sasa REA III
WILAYA |
KIJIJI |
Karagwe
|
Katanda
|
Kyerwa
|
Kyerwa
|
Missenyi
|
Rushana
|
Muleba
|
Buhaya
|
Vijiji vinavyotaraijwa kuwashiwa umeme hivi punde |
|
Bukoba Vijijini
|
Burugo
|
|
|
Biharamulo
|
Nyarubungo na
|
|
Kakoma
|
Nguzo za laini ya msongo wa umeme mkubwa(kilovolt 33) zilizosimamishwa ni 8.27km
Kilometa za waya kwa nguzo za msongo mkubwa (kilovolt 33) zilizovutwa ni 3.036km
Nguzo za laini ya msongo wa umeme mdogo(230/400) zilizosimamishwa ni 28.30km
Kilometa za waya kwa nguzo za msongo mdogo zilizovutwa ni 2.7km
Mpaka sasa Mradi umetekelezwa kwa asilimia tano nukta saba (5.7%) Kimkoa. Mradi wa REA III mzunguko wa kwanza ni Mradi ambao unatakiwa kukamilika ndani ya miaka miwili (2) toka kuzinduliwa kwake.
Changomoto iliyopo ni kuwa kazi hii inatekelezwa na Mkandarasi mmoja katika Mkoa ambaye anatakiwa kuhudumia Wilaya zote saba (7) za Mkoa.
MADINI |
Madini Yapatikanayo Mkoani Kagera |
Mkoa wa Kagera una madini yafuatayo kama yalivyo tofautishwa kutokana na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010:-
Madini aina ya chuma: dhahabu, bati ghafi, wolframite (WO3), Nickel, Manganese n.k.
Madini ya viwandani: Kaolini, Silica Sand na diatomite.
Madini ya ujenzi: Mchanga, mawe, moram, udongo mfinyanzi, mawe ya vigae
Madini mengine yanaendelea kugundulika kadri taarifa za utafiti zinavyoendelea kutolewa.
Utafiti wa Madini Katika Mkoa |
Kwa takwimu zilizopo hadi kufikia mwezi Agosti, 2018, Katika Mkoa wa Kagera kuna jumla ya leseni hai 52 za utafiti mkubwa wa Madini. Leseni hizi zilizotolewa katika Wilaya mbalimbali kama inavyonyeshawa kwenye jedwali hapa chini:
Idadi ya Leseni za Utafiti wa Madini
S/N |
Jina la wilaya |
Jumla ya Idadi ya Leseni za utafiti |
Aina ya Madini na Idadi ya leseni |
|||||||
Gold
|
Nickel
|
Tin
|
Zinc
|
Wolfram
|
Tantalite
|
Tangsten
|
Silica sand
|
|||
1 |
Biharamulo
|
22 |
19 |
3 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
2 |
Kyerwa
|
15 |
0 |
1 |
9 |
0 |
2 |
2 |
1 |
0 |
3 |
Ngara
|
10 |
1 |
6 |
1 |
1 |
0 |
1 |
0 |
0 |
4 |
Karagwe
|
2 |
0 |
0 |
2 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
5 |
Muleba
|
1 |
0 |
1 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
6 |
Missenyi
|
1 |
0 |
0 |
1 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
7 |
Bukoba
|
1 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
1 |
Jumla |
52 |
20 |
11 |
13 |
1 |
2 |
3 |
1 |
1 |
Leseni za Madini Zilizopo Katika Mkoa |
Aina za leseni za uchimbaji zilizopo Mkoani Kagera zimegawanyika katika makundi matatu ambazo ni Leseni kubwa za Uchimbaji (SML), Leseni ndogo za Utafiti na Uchimbaji (PML) pamoja na Leseni za kushikilia eneo yaani Retention License (RL). Idadi ya leseni hizo ni kama ifuatavyo:
Leseni za Madini Zilizopo Katika Mkoa
Aina ya Madini
|
Idadi
|
Mmiliki
|
Leseni kubwa za Uchimbaji (SML)
|
1 |
STAMIGOLD
|
Leseni ndogo za uchimbaji (PML)
|
535 |
Wachimbaji wadogo
|
Retention License (RL)
|
1 |
Kabanga Nickel
|
Uchimbaji na Uzalishaji wa Madini Mkoani |
Madini yanayochimbwa na mchimbaji mkubwa ni dhahabu. Madini haya yanachimbwa na kampuni ya Stamigold Company Ltd Gold Mine huko Biharamulo. Madini mengine yana chimbwa na wachimbaji wadogo ni pamoja na Bati, Kaolin na Madini ujenzi (mchanga, kokoto).
Uzalishaji wa Dhahabu na Madini ya fedha (Silver) |
Uzalishaji waMadini ya dhahabu na fedha kwa kiasi kikubwa umekuwa ukifanyika katika leseni namba SML 157/2003 inayomilikiwa na Kampuni ya STAMIGOLD wilayani Biharamulo. Katika kipindi cha mwezi Julai 2014 mgodi huo ulipoanza kuendeshwa na Serikali hadi mwezi Agosti, 2018, Uzalishaji wa Madini ulikuwa kama ilivyoainishwa kwenye jedwali hapa chini:
Uzalishaji wa Madini katika Mgodi wa Stamigold
Mwaka |
Uzalishaji/Mauzo kwa Kgs |
Jul-Des, 2014
|
188.33
|
Jan-Des, 2015
|
726.24
|
Jan-Des, 2016
|
655.42
|
Jan-Des,2017
|
289.71
|
Jan-Agu,2018
|
238.26
|
JUMLA
|
2,097.96
|
Jumla ya thamani ya Madini hayo ni Dola za Kimarekani 66,745,042.04. Uzalishaji Madini katika mgodi huo umechangia Serikalini mapato ya jumla ya Dola za Kimarekani 2,809,621.75 ambapo Dola za Kimarekani 2,705,897.42 ni mrabaha na Dola za Kimarekani 103,724.33 ni ada ya ukaguzi ambayo ilianza kutozwa mwezi Julai, 2017 baada ya marekebisho ya Sheria ya Madini.
Madini ya dhahabu pia yanachimbwana wachimbaji wadogo katika maeneo ya Busiri, Mavota na Kalukwete Wilayani Biharamulo. Wachimbaji hao wanakabiliwa na changamoto mbalilmbali zikiwemo vitendea kazi na elimu duni ya masuala ya utafiti na na uchimbaji.
Tangu shughuli hizo zianze kushamiri katika maeneohayo mwezi Februari 2017 hadi Agosti, 2018, jumla ya Gramu 1,875.27 za Madini ya dhahabu yenye thamani ya jumla ya shilingi za kitanzania 126,505,000/= ziliripotiwa kuzalishwa na kulipiwa Mrabaha wa kiasi cha jumla ya shilingi 4,881,260/=.
Uzalishaji wa Bati Ghafi (Tin) |
Madini haya yanachimbwa na wachimbaji wadogo hususani katika Wilaya ya Kyerwa. Katika kipindi cha mwaka 2015/16 hadi Januari 2017/ 2018 jumla ya tani 181.305 za bati ghafi zenye takribani thamani ya shilingi 3,368,168,680/= zilizalishwa katika maeneo mbalimbali wilayani Kyerwa.
Uzalishaji wa Madini ya Ujenzi na Kaolin |
Uzalishaji wa madini ya kaolini unafanyika katika Wilaya ya Biharamulo na Madini Ujenzi ni katika Wilaya zote za Mkoa huu. Uzalishaji wa madini haya kuanzia 2015/16 hadi Agost, 2018 ni kama ifuatavyo:
Jedwali Na. 32: Uzalishaji wa Madini ya Ujenzi na Kaolin
Na. |
Aina ya Madini |
Kiasi (Tani) |
Thamani (Tsh) |
Mrabaha uliolipwa (Tsh) |
1.
|
Kaolin
|
1,770.75 |
148,257,333.33 |
4,334,480 |
2.
|
Madini Ujenzi
|
162,187.83 |
2,081,920,184.59 |
55,659,242.46 |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa