- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Wilaya ya Kyerwa ni kati ya Wilaya mpya nchini lakini naiona Wilaya hii kwa miaka michache ijayo mbele kidogo itakuwa na nguvu kubwa kiuchumi kutokana na raslimali zinazopatikana hapa, itaongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa katika mkoa wa Kagera na nchini kwa ujumla kutokana na madini ya TIN yanayopatikana hapa pamoja na zao la kahawa, ndizi na mazao mengine.
Maneno ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi makao makuu ya Wilaya ya Kyerwa Rubwela Septemba 20, 2021 mara baada ya kutembelea kiwanda cha African Top Minerals Limited cha kuchenjua madini ya TIN yanaoyopatikana mkoani Kagera wilayani Kyerwa tu.
Ni baada ya kufurahishwa na uwekezaji wa kiwanda hicho chenye thamani ya Shilingi bilioni nne ambacho kina uwezo wa kuchenjua tani 10 kwa siku na tani 250 kwa mwezi za madini ya TIN. Waziri Mkuu Kassim majaliwa alitoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa hiyo kwani madini ya TN Wilayani Kyerwa ni ya kutosha na kutokana na utafiti uliofanyika mwaka 2017 na Taasisi ya Utafiti wa Madini Tanzania iligundulika kuwa katika eneo moja tu kuna madini ya TIN tani milioni nne ambazo zinaweza kuchimbwa kwa miaka 40 hadi 50
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwepo kwa viwanda vya TIN Wilayani Kyerwa vya Afican Top Minerals Limited na TANZA PLUS Limited vyenye u wezo wa kuchenjua tani 16 kwa siku na tani 450 za TIN kwa mwezi ni fursa kubwa kwa vijana kujiajili kwa kuchimba madini hayo ambayo yamepanda bei mara baada ya wawekezaji hao wa viwanda kujenga viwanda hivyo na kuanza uchenjuaji Wilayani humo.
“Hii ni ajira vijana changamka unachimba mawe haya kilo moja unauza hapa hapa na bei imepanda baada viwanda hivi kuwa vimejengwa na kuhitaji mzigo wa kutosha ili vifanye kazi, mwaka 2019 madini haya ya TIN yalikuwa yanauzwa shilingi 6,000/- kwa kilo leo mwaka 2021 yanauzwa shilingi 34,000/- kwa kilo. Kyerwa tukitumia fursa hii wilaya itakuwa na maendeleo makubwa sana na itaongoza kwa uchumi mzuri mkoa wa Kagera.” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wananchi Wilayani Kyerwa.
TANESCO Waagizwa Kuachana na Wakandarasi Katika Ujenzi
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa Wilayani Kyerwa alikataa kuzindua majengo ya ofisi za TANESCO wilaya yaliyojengwa na Mkandarasi kwa gharama ya shilingi milioni 483,422,328.02 mara baada ya kusomewa taarifa amabyo ilitaja gharama za ujenzi wa kibanda cha mlinzi kugharimu shilingi milioni saba ambapo alisema kuwa angeweza kuchukua hatua lakini ni kutokana na majengo hayo kujengwa kwa kutumia Mkandarasi.
“Ningeweza kuchukua lakini kwa kuwa mlitumia Mkandarasi basi nawaagiza kuacha mara moja mfumo huo na kwa majengo mnayoyajenga katika Wilaya 12 nchini tumieni mfumo wa FORCE AKAUNTI. Haiwezekani Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia Halmashauri za Wilaya tujenge Vituo vya Afya vyenye majengo matano kwa gharama ya shilingi milioni 500 halafu hapa mmejenga jengo moja uzio, kibanda cha mlinzi na stoo kwa gharama ya shilingi milioni 483,422,328.02.” Aliagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Serikali Kuuangalia Upya Mfumo wa Ushirika Mkoani Kagera
Ni baada ya kutembelea kiwanda cha Ngara Coffee kilichopo Wilayani Ngara ambacho hakifanyi kazi kutokana na kukosa malighafi ambayo ni kahawa, aidha malalamiko ya wananchi kuwa bei ya shilingi 1,300 ni ndogo ukilinganisha na mikoa mingine nchini. Baada ya kupokea malalamiko hayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaeleza wananchi katika mikutano ya hadhara kuwa anakusudiwa kuunda timu ya wataalam kwenda mkoani Kagera kupitia upya mfumo wa Vyama vya Ushirika ili kuona namna ya kumnufaisha mkulima zaidi badala ya Vyama vya Ushirika.
"Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa atatuma timu ya wataalam kufanyia kazi tatizo la bei ya kahawa, Kuhakiki Mali za Vyama vya Ushirika vinavyonunua na kuuza kahawa ya wakulima, kushughulika na mfumo wa kununua na kuuza kahawa, Kushughulikia suala la bei ya kahawa mkoani Kagera kuwa ya chini, na Kwanini tozo ni nyingi zinafika hadi 12 badala ya tozo tano tu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa baada ya mradi wa kuzalisha umeme wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 898 unaotekelezwa na nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi kukamilika Desemba 2021 na kuanza kuzalisha umeme Mkoa wa Kagera utaunganishwa kwenye gridi ya taifa na matatizo ya umeme Kagera yatakuwa yamefikia mwisho.
Mwisho, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwataka viongozi wa Mkoa wa Kagera kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo hasa miradi inayolenga kutoa huduma kwa wananchi ambayo imetolewa fedha nyingi na Serikali, mfano ujenzi wa Hospitali za Wilaya na Vituo vya Afya ili miradi hiyo ijengwe kwa ubora unaotakiwa na ujenzi uendane na thamani ya fedha iliyotolewa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa