• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Aagiza Watumishi Wawili Kusimamishwa Kazi na Watano Kuchunguzwa Juu ya Ubadhilifu wa Fedha Za Serikali - Biharamulo

Imewekwa : August 17th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti aiagiza Mamlaka ya Nidhamu za Watumishi ya Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kuwasimamisha kazi mara moja watumishi wawili kupisha uchunguzi na wengine watano kuchunguzwa juu ya upotevu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 690 zilizokusanywa katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani na fedha hizo hazikuwasilishwa Benki kwenye akaunti ya Halmashauri kama kanuni, taratibu na sheria  za fedha zinavyoelekeza.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa maagizo hayo leo Agosti 7, 2018 katika kikao Maalum cha Kamati Fedha, Uongozi na Mipango ambacho kililenga kupokea taarifa ya uchunguzi wa awali na ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato ya ndani iliyoundwa na Katibu Tawala Mkoa wa Kagera CP Diwani Athuman baada ya kupata taarifa kutoka katika vyanzo vyake vya ndani  juu ya upotevu wa fedha kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo.

Watumishi walioagizwa kusimamishwa kupisha uchunguzi na ikithibitika wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ni Bw. Salanga Mahendeka  (Mhasibu wa Mapato) ambaye alibainika kuwa na hoja ya mashaka ya fedha zaidi ya shilingi milioni 276 ikiwa ni pamoja na: Kutosimamia utaratibu wa mapato ya fedha yaliyoondolewa  katika mfumo wa mapato bila idhini ya Afisa Masuuli, Kusababisha madeni ya wakusanyaji kutotambuliwa kwa kutofanya usuluhishi wa miamala ya mapato  katika mashine za kukusanyia mapato, Kukusanya fedha bila kuziwasilisha benki.

Mtumishi wa pili aliyeagizwa Mamlaka ya Nidhamu  kumsimamisha kazi ili kupisha  TAKUKURU kufanya  uchunguzi juu yake ni Bw. Emmanuel Maleo (Afisa Ushirika) ambaye alibainika kuchukua fedha taslimu kwa wafanyabiashara kwa nyakati tofauti mwezi Februari hadi Machi, 2018 bila kuziwasilisha Benki na kushindwa kuhitimisha mchakato wa kuwapatia leseni wafanyabiashara hadi Mei, 2018.

Aidha, Watumishi wengine watano walioagizwa kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua za kinidhamu  na Mamlaka zao za Nidhamu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu  endapo itathibitika tuhuma zao ni za kweli  ni pamoja na: Bw. Alexander Bashaula (Mweka Hazina) ambaye ni mkuu wa idara ya fedha ambaye alifanya uzembe katika kuwasimamia ipasavyo watumishi walioko chini yake kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu pia na kushindwa kumsahuri ipasavyo Afisa Masuuli kuhusu masuala ya fedha.

Pili ni Bi Beatrice P. Garusya (Afisa Biashara) ambaye hakutoa leseni za biashara kwa wafanyabiashara waliolipia na kusababisha malalmiko yasiyo ya lazima kwa wafanyabiashara hao . Tatu ni Bw. Rogers H. Simkoko (Afisa Tehama) aliyefanya miamala ya kihasibu badala ya kufanya kazi yake ya ufundi kwenye mfumo wa kukusanya mapato na kukiuka  taratibu kwa kutoa haki kwa Afisa mmoja kukamilisha miamala peke yake.

Wengine ni Bi Saphina Malimba (Mtunza Fedha) ambaye hakuwasilisha benki kiasi cha shilingi milioni 32, 098,800/= alizokusanya kwa kutumia mashine ya kukusanya mapato. Mwisho ni Bi Specioza Mikole (Mhasibu) aliyekuwa Mhasibu na kuhamishiwa TARURA  na aliondoka na mashine ya kukusanyia mapato bila kuikabidhi ambayo ilikuwa na madeni makubwa ya fedha na fedha  alizokuwa amekusanya zinatiliwa mashaka matumizi yake pia haijulikani kama fedha hizo ziliwasilishwa benki.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kumrejesha  Mtumishi huyo na kumtaka akabidhi mashine hiyo ifikapo saa 10:00 jioni Agosti 17, 2018 ili usuluhishi ufanyike na endapo kuna deni atakiwe kulipa mara moja pia alimwagiza Kamanda wa TAKUKURU Mkoa kufuatilia na kuchukua hatua pia hatua  za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti aliagiza wakusanyaji 59 wa mapato ya ndani kwa kutumia mashine za kielektroniki waliokuwa hawajawasilisha mapato benki ya jumla ya shilingi milioni 427,130,100/= hadi ufuatiliaji unafanyika ifikapo Jumatatu Agosti 20, 2018 wawe wamewasilisha mashine zao kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ili zifanyiwe usuluhishi  chini ya usimami wa Katibu Tawala Mkoa na kiasi kitakachothibitika kudaiwa kipelekwe benki mara moja. Pia Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi wenye madeni hayo iwachukulie hatua za kinidhamu.

Aidha, vibanda 25 vya Soko la Kabindi vilivyobainishwa kwenye taarifa ya uchunguzi kuwa havikuwa na mikataba ya kukodishwa Mkuu wa Mkoa Gaguti aliagiza Halmashauri kuandaa mikataba hiyo mara moja kulingana na bei ya soko ya kukodi vibanda vya biashara  kulingana na na mazingira vilipo pia viboreshwe kwa kuwekewa umeme ili kiwe chanzo cha mapato cha Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo.

Maamuzi hayo yalifikiwa na Mkuu wa Mkoa Gaguti baada ya Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Kagera Bw. David Lyamboko Kuwasilisha taarifa ya uchunguzi wa awali uliofanyika chini ya uongozi wake baada ya Katibu Tawala Mkoa kuunda Kamati hiyo na kuipa adidu za rejea ili kufanya uchunguzi na Kamati hiyo ilianza kazi yake  Mei 28, 2018 na kuikamilisha kazi hiyo Juni 18, 2018.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa kagera CP Diwan Athuman katika kikao hicho maalum aliwakumbusha wviongozi na Wakuu wa Idara ya Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kujitathimini na kujitafakari kama wanamsaidia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Maguli kufanikisha adhima ya kuwahudumia wananchi kwa uadilifu.

Pia aliwaasa watumishi popote walipo katika Halmashauri za Wilaya kujitafakari kwa dhati juu ya utendajikazi wao, kuwa na mtazamo wa viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano nini wanakilenga katika kutekeleza majukumu yao, na tatu ni kushirikiana kuwa na upendo pia na kuwa wakweli. Aidha, kila mtumishi alitakiwa kujitafakari kulinagana na Kaulimbiu ya Mkoa wa Kagera Isemayo Kagera Kazi, Amani na Maendeleo na ajipime kama anatimiza wajibu kulingana na kaulimbiu hiyo.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa