- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Yahaya Ramadhani Kido awasili na kupokelewa rasmi Mkoani Kagera Februari 11, 2026 tayari kuanza kazi ya ukuu wa Mkoa.
Kanali Yahaya Ramadhani Kido aliteuliwa tarehe 6 Februari, 2026 na kuapishwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 6 Februari, 2026. Kanali Yahaya R. Kido anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa 27 tangu uhuru mwaka 1961.
Aidha, Kanali Yahaya Ramadhani Kido anachukua nafasi ya Hajjat Fatma Abubakar Mwassa (Mkuu wa Mkoa mstaafu) aliyehudumu katika nafasi hiyo ya ukuu wa Mkoa tangu mwaka 2023.
Baada ya kuwasili Mkoani Kagera Kanali Yahaya R. Kido anatarajia kukabidhiwa ofisi na Mtangulizi wake Hajjat Fatma A. Mwassa tarehe 13 Februari 2026 na kuanza kutekeleza rasmi majukumu yake ya kikazi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa