- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Agizo la Rais Magufuli Laanza Kutekelezwa Kulifanya Pori la Burigi Kuwa Kivutio Cha Utalii Mkoani Kagera
Agizo la Rais Magufuli la kuufanya Mkoa wa Kagera kuwa kitovu cha utalii Kanda ya Ziwa kwa kuyalinda Mapori ya Akiba na Misitu ya Hifadhi hasa Mapori ya Biharamulo, Burigi na Kimisi laanza kutekelezwa rasmi na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ili kuzifanya hifadhi hizo kuwa maeneo ya utalii.
Katika kutekeleza agizo hilo la Rais Magufuli, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko alitembelea Pori la Akiba la Burigi Novemba 16, 2017 na kulikagua pori hilo ambapo alijionea mwenyewe wanyamapori walivyorejea katika pori hilo na kuona ni sehemu gani wawekezaji wanaweza kuwekeza hasa katika hoteli za kitalii na miundombinu mingine.
Meja Jenerali Mstaafu Semfuko baada ya kutembelea pori hilo kwa njia ya anga (Ndege) na kutembelea kwa njia ya gari pia na kuzunguka katika ziwa Burigi kwa boti alifurahishwa na kurejea kwa wanyama wengi katika Pori la Akiba la Burigi baada ya kuondoshwa ng’ombe wote waliokuwa wamevamia pori hilo.
“Nimejionea hali halisi na naupongeza uongozi wa Mkoa kwa kusimamia operesheni ya kuondoa mifugo yote, nimepita juu na ndege na sikuona ng’ombe hata mmoja bali nimeona wanyama wengi ambapo wakati nilipokuja wakati wa operesheni sikuwaona kabisa mfano Twiga,Tembo, Swala, Pundamilia na wengine wengi wamerea sasa,” alististiza Mwenyekiti wa Bodi Semfuko.
Meja Jenerali Mstaafu Semfuko alisema kuwa baada ya Rais Magufuli kuagiza eneo hilo kufanywa eneo la utalii wao kama Bodi ndiyo watekelezaji wa agizo hilo. Pia alisema kuwa yeye alikuja kujihakikishia ili akatoe taarifa kwenye bodi ambapo tayari Bodi hiyo imeishampata mwekezaji ambaye atawekeza katika eneo la Nkonje kwa kujenga sehemu za kupumzikia na ujenzi ambao utahusisha mahema ya kisasa.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania Bw. Imani Nkuwi alisema kuwa bado wanaangalia wanyama wote warejeree katika pori hilo na kuona uwezekano wa hapo baadae kupandikiza wanyama wengine kama vivutio.
Rais Magufuli akiwa Mkoani Kagera katika ziara ya kikazi ya siku nne Novemba 6, 2017 akiwahutubia wananchi na Taifa kwa ujumla Katika Manispaa ya Bukoba alipokuwa akizindua uwanja wa Ndege wa Bukoba alikemea vitendo vya kuvamia Misitu ya Hifadhi na Mapori ya Akiba hasa pori la Burigi Wilayani Biharamulo ambapo aliagiza pori hilo kulindwa na kulifanya sehemu ya utalii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa