- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
RASMU YA BAJETI YA MKOA YA MWAKA 2017/2018 YAPITISHWA NA VIKAO VYA KISHERIA MKOANI KAGERA
Kikao cha Balaza la Wafanyakazi na Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) Mkoani Kagera ambavyo ni vikao vya kisheria vimefanyika kwa kupitia na kuridhia rasmu ya bajeti ya mkoa kwa mwaka 2017/2018 ambapo Mkoa wa Kagera unaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 335,198,197,649.
Kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 233,562,036,745 ni Mishahara ya Watumishi (PE), Shilingi bilioni 20,495,137,000 ni Matumizi Mengineyo (OC), Shilingi bilioni 64,769,162,413 ni fedha za Miradi ya Maendeleo. Aidha, shilingi bilioni 16,371,861,491 yatakuwa ni makusanyo ya vyanzo vya ndani (Own Source) na maduhuli ya Sekretarieti ya Mkoa.
Vikao hivyo vya kisheria vilifanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambapo kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilifanyika Machi 1, 2017 na Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichoongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kilifanyika Machi 3, 2017.
Pamoja na vikao hivyo kupitia na kuridhia rasmu ya bajeti ya mkoa ya mwaka 2017/2018 Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu alitoa rai kuwa hali ya hewa ya Mkoa wa Kagera ni nzuri na mvua zimeanza kunyesha kwa wastani wa milimita 800 – 1,100 kuanzia mwezi Februari, 2017.
Pia Mkuu wa Mkoa aliwaomba wajumbe na viongozi wa kikao cha (RCC)kuendelea kuwahamasisha wananchi kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kulima mazao yanayostawi kwa muda mfupi ili kutatua changamoto za upatikanaji wa chakula kwenye mkoa.
Aidha, aliwaagiza wataalamu wa kilimo wawasimamie wananchi wazalishe kwa wingi na kuuza ziada ili wajikwamue na umasikini wa kipato. Pia Mhe. Kijuu alisistiza uhamasishaji wa upandaji miti uendelee kutolewa kwa wananchi wote ili kutunza na kulinda tunu ya mazingira ya Mkoa wa Kagera.
Mwisho Mhe. Kijuu aliziagiza Kamati za Maafa za Wilaya ziendelee kuchukua tahadhari ya kutosha kukabiliana na athari za mafuriko, mmomonyoko wa ardhi na uharibifu wa miundombinu mbalimbali ili kujihami na athari zinazoweza kutokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Kagera.
Mwaka wa fedha 2015/2016 Halmashauri za Mkoa wa Kagera zilikadiriwa kukusanya jumla ya Shilingi 15,988,022,000 toka vyanzo vyake vya ndani. Kwa kipindi cha Julai, 2015 hadi Juni 2016 makusanyo halisi yalikuwa ni shilingi 11,585,454,840.84 sawa na asilimia 72.46 ya lengo la mwaka. Aidha kwa mwaka 2016/2017 Mkoa ulipanga kukusanya jumla ya shilingi 16,424,163,859 ambapo hadi kufikia mwezi Disemba, 2016 zilikuwa zimekusanywa Jumla ya Shilingi 6,863,000,367.97 sawa na asilimia 43.83 ya lengo kwa mwaka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa