• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Vyeti Vya Kuzaliwa Kwa Watoto Chini ya Miaka Mitano Vyapatiwa Ufumbuzi na Serikali Kwa Kuondoa Usumbufu Kwa Wananchi Kwenda Wilayani

Imewekwa : September 14th, 2018

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) yaja na Mpango Mkakati wa kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa sasa na wale ambao tayari wamezaliwa chini ya umri wa miaka mitano wanapata Vyeti vya Kuzaliwa kwa mfumo mpya wa Wakala (RITA) kupeleka huduma hiyo ya utoaji vyeti katka ngazi ya Vituo vya Afya pamoja na ngazi ya Ofisi za Watendaji wa Kata.

Mpango Mkakati huo wa RITA uliwasilishwa Septemba 14, 2018 katika semina ya siku moja iliyofanyikia katika Ukumbi wa Hoteli ya Kolping Manispaa ya Bukoba ili kuwaelimisha Viongozi wa Mkoa na Wilaya kuhusu utaratibu mpya wa utoaji Vyeti vya Kuzaliwa  kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Kagera.

Akitoa maneno ya utangulizi katika Semina hiyo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu RITA Bibi Emmy Kalomba Hudson alisema kuwa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umeamua kuja na Mpango Mkakati wa kupeleka huduma ya utoaji vyeti kwa watoto chini ya miaka mitano katika ngazi ya Kata na Vituo vya Afya ili kuondoa kero zilizokuwepo awali kwasababu ya vyeti hivyo kupatikana katika Ngazi ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya tu.

“Serikali kupitia RITA imeanza kufanya maboresho ya jumla ya mfumo  mzima wa usajili chini ya Mkakati wa Kitaifa wa Kuboresha Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu  na Takwimu. (National Strategy on Civil Registration and VitalStatistics). Mkakati wa CRVS una mipango mbalimbali ya utekelezaji ikiwa ya muda mfupi na mrefu kwa makundi yatokanayo na umri ili kufikia ufanisi unaotarajiwa.” Alifafanua Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Bibi Emmy Kalomba.

RITA wamekuja na Mpango Mkakati wa kusajili watoto chini ya miaka mitano baada ya Tanzania kuwa na asilimia 13.4% ya usajili ambapo kiwango hicho ni cha chini sana ukilinganisha na mataifa mengine Barani Afrika . Aidha, kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa Mkoa wa Kagera una watoto waliochini ya umri wa miaka mitano 542,806 (NBS 2018)  na watoto wenye vyeti ni asilimia 12.4% ambapo  kwa Sensa ya mwaka 2012 ilikuwa ni asilimia 12.2%  na watoto ambao hawajasajiliwa ni 475,498.

Akifungua Semina hiyo ya siku moja Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti aliwataka wajumbe wa semina hiyo kufuatilia kwa umakini mafunzo hayo na kutoa maoni ya kuboresha mkakati wa RITA katika kuhakikisha unafanikiwa katika maeneo yao na kuwa na tahadhari juu ya Wananchi wasiokuwa raia wa Tanzania kutokana na Mkoa wa Kagera kuwa na mipaka mingi na nchi jirani.

Wakiboresha Mkakati wa RITA wa kusajili watoto chini ya umri wa miaka mitano katika Semina hiyo wajumbe walipendekeza kuwa uwepo pia mpango wa kusajili miaka 5  hadi 18 kwasababu bado hitaji ni kubwa katika jamii la upatikanaji wa Vyeti vya Kuzaliwa. Kuzingatia suala la ulinzi na usalama wa nchi katika zoezi hilo kwa kuanzisha usalama wa nyumba kumi ili kila mwananchi ktambulika kisawasawa katika nyumba kumi.

Vigezo vya Mtoto anayesajiliwa kupitia Mpango wa Usajili wa watoto: Kwanza, Mtoto awe amezaliwa katika ardhi ya Tanzania Bara (Bila kujali uraia wa wazazi wake). Pili, Mtoto awe na umri usiozidi miaka mitano. Tatu, Mtoto awe na kiambatisho kimojawapo kati ya vifuatavyo: (Tangazo la kizazi au Kadi ya Kliniki. Nne, Vitambulisho vya wazazi (Kimojawapo kwa kila mzazi kati ya vifuatavyo, Kadi ya kupiga kura au Kitambulisho cha Taifa)

Namna zoezi litakavyendeshwa Mkoani Kagera.

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) utaendesha mafunzo ya siku tatu  kwa Maafisa sita (Afisa Ustawi wa Jamii, Mipango, Tehama, Maendeleo ya Jamii, Ugavi na Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto) kutoka kila Halmashauri ya Wilaya ili kujifua namna ya kutekeleza zoezi la usajili watoto chini ya miaka mitano katika Vituo vya Afya na Ofisi za Afisa Watendaji wa Kata.

Vvyeti vya Kuzaliwa vitakavyotolewa katika zoezi hilo vitakuwa vya kuandika kwa mkono tofauti na vinavyotolewa kwa kuchapwa na mshine lakini vitakuwa halali na vitakuwa vimesajiliwa katika mfumo wa Serikali. Zoezi hilo litaanza rasmi Oktoba Mosi, 2018 na litaendeshwa kwa wiki mbili lakini pia baada ya wiki hizo mbili kuisha zoezi litakuwa endelevu kwa kila mtoto atakayezaliwa.

Ikumbukwe kuwa hakutakuwa na gharama yoyote ya Cheti cha Kuzaliwa kwa mtoto chini ya umri wa miaka mitano wazazi wanatakiwa kuwapeleka watoto katika vituo watakavyokuwa wameelekezwa katika Halmashauri zao. Aidha, kwa uataratibu huu mpya watoto chini ya miaka mitano vyeti vyao havitatafutwa tena katika Ofisi za Wakuu wa Wilaya bali wale wenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa