- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika msimu wa kilimo 2016/2017 Mkoa ulijiwekea lengo la kulima na kutunza jumla ya hekta 650,706 za mazao mbalimbali ya chakula zilizotarajiwa kuzalisha jumla ya tani 2,218,990 za ndizi, tani 413,049 za nafaka, tani 154,995 za mikunde na tani 1,166,268 za mazao ya mizizi.
Aidha, Mkoa ulilenga kulima na kupanda jumla ya hekta 62,079 za mazao mbalimbali ya biashara zilizokadiriwa kuzalisha tani 82,674 za kahawa maganda ,tani 337 za tumbaku, tani 1160 za pamba mbegu na tani 4543 za majani mabichi ya chai.
Hadi kufikia Juni, 2017 Mkoa ulikuwa umelima na kutunza jumla ya hekta 600,632 za mazao mbalimballi ya chakula na kuzalisha jumla ya tani 1,420,445 za ndizi, tani 115,200 za nafaka ambapo kati ya tani hizo zao la mahindi limechangia uzalishaji wa tani 109,440, tani 61,748 za mikunde na tani 758,00 za mazao ya mizizi hata hivyo katika Mkoa wa Kagera kuna baadhi ya maeneo ya Wilaya uvunaji na uzalishaji wa mazao ya mizizi huwa ni endelevu kwa msimu wote wa mwaka
Mazao ya biashara, Mkoa umelima na kutunza jumla ya hekta 50,581 za mazao mbalimbali ya biashara na kuzalisha tani 28,050 kahawa safi, tani 200 za tumbaku, tani 900 za pamba mbegu na tani 1,500 za majani mabichi ya chai.
Katika mazao ya kipaumbele kitaifa Mkoa wa Kagera unazaliza mazao ya kahawa, chai, pamba na tumbaku. Kwa umuhimu wa mazao hayo uzalishaji ni kama ifuatavyo:
Mkoa wa Kagera ni moja ya Mikoa inayozalisha kwa wingi zao la kahawa hapa nchini ambapo wastani wa uzalishaji wa kahawa ya maganda kwa mwaka ni tani 50,000. Kutokana na takwimu za uzalishaji kahawa kitaifa, Mkoa wa Kagera unaongoza katika uzalishaji wa kahawa.
Zao la pili la biashara linalozalishwa Mkoani Kagera ni Chai inayolimwa katika Wilaya za Bukoba na Muleba. Wastani wa uzalishaji wa zao la chai kwa mwaka ni tani 1,000 hadi 1,500 kwenye eneo la hekta 1,132.
Zao la tatu ni pamba ambayo huzalishwa katika Wilaya za Biharamulo na Muleba. Wastani wa uzalishaji kwa mwaka ni tani 900 ambazo huzalishwa kwenye eneo la hekta 2,000. Idadi ya wakulima wanaojihusisha na kilimo cha pamba Mkoani Kagera ni takribani 5,700.
Zao la nne kwa umuhimu katika Mkoa wa Kagera ni Tumbaku ambayo huzalishwa katika wilaya ya Biharamulo kwenye eneo la hekta 237 na wastani wa mavuno kwa mwaka ni tani 230.
Mazao mengine ya biashara yanayolimwa Mkoani Kagera ni pamoja na vanilla na miwa. Wastani wa uzalishaji wa zao la vanilla ni tani 45 kwenye eneo la hekta 50 ambapo wakulima wanaojiuhusisha na kilimo cha vanilla ni takribani 6,000 wengi wao wakiwa chini ya usimamizi wa MAYAWA (Maendeleo ya Wakulima).
Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la kahawa iliyopitishwa na Kikao cha Wadau Mkoani ni kama ifuatvyo:-
Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la chai:
Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la pamba:
Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la tumbaku:
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Mkoa wa Kagera una idadi ya wakazi wapatao 2,458,023 na wastani wa ongezeko la asilimia 3.1 linalopelekea idadi ya watu kufikia 2,762,818 hadi Desemba, 2016. Kwa uwiano wa mahitaji ya mtu mmoja kwa siku ambayo ni gramu ya utomwili na gram 650 za vyakula vya wanga, Mkoa wa Kagera unahitaji tani 655,479 ya vyakula vya wanga na tani 65,547 ya vyakula vya utomwili kwa mwaka.
Uhakika wa Chakula katika Mkoa wa Kagera
Hadi mwishoni mwa mwezi Juni, 2017 Wilaya zote zinazozalisha ndizi zilikuwa zimezalisha zaidi asilimia 64 ya lengo, sawa na tani 1,420,445 za ndizi ambazo ndiyo chakula kikuu kwa wananchi walio wengi katika Mkoa wa Kagera, hivyo kiasi hicho pamoja na mazao mengine yaliyozalishwa kipindi hicho kilitosheleza mahitaji kwa kipindi husika na hatukuwa na ziada ya kutosheleza kuuza maeneo mengine. Aidha Mazao mengine ya chakula kama vile Mihogo, Viazi na Magimbi yameendelea kuzalishwa katika kiwango cha wastani.
Upatikanaji wa Pembejeo bora za kilimo za Ruzuku
Wakulima wameweza kutumia pembejeo bora kama vile mbolea, dawa pamoja na mbegu bora zikiwemo za ruzuku na ambazo si za ruzuku. Mkoa ulipokea pembejeo za ruzuku msimu wa mwaka 2016/2017 za aina mbili ambazo ni mbegu ya mahindi Kilogram 50,000 na mbole ya kukuzia Kilogram 100,000. Mbolea hizi zilishasambazwa katika Halmashauri tano zilizopo kwenye mpango wa ruzuku. Halmashuri hizo ni Biharamulo (Kg 10,000 mbegu na Kg 20,000 mbolea), Ngara (Kg 10,000 Mbegu na Kg 15,000 mbolea), Karagwe (Kg 12,500 mbegu na Kg 25,000 Mbolea), Missenyi (Kg 10,000 mbegu na Kg 20,000 Mbolea) na Kyerwa (Kg 7,500 Mbegu na Kg 20,000 mbolea).
Hatua Zinazochukuliwa na Mkoa Kuimarisha Sekta ya Kilimo
Katika kuendeleza Sekta ya kilimo, Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri imekuwa ikibuni Mipango mbalimbali ya Kisera na Kimkakati mfano maonesho ya kilimo (Nanenane) Kimkoa, Lengo likiwa ni kubadilisha kilimo kutoka kilimo cha mazoea na kukifanya kiwe kilimo cha kibiashara na endelevu kutokana na teknolojia mbalimbali wanazozipata kupitia maonesho hayo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa