- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akabidhiwa Ofisi Tayari Kuwahudumia Wananchi
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Yahya Ramadhani Kido akabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake Hajjat Fatma Abubakar Mwassa tayari kutekeleza majukumu ya kuwaletea wananchi wa Mkoa wa Kagera maendeleo.
Akitoa salaam mara baada y a makabidhiano hayo Februari 13, 2026 Mkuu wa Mkoa Kanali Yahya R. Kido aliweka wazi vipaumbele vyake katika kuuongoza mkoa wa Kagera, kwanza alisema atahakikisha anaendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha usalama wa mkoa kutokana na mkoa huo kuwa na mipaka mingi.
Pili, alisema kuwa atasimamia utekelezwaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa ili itekelezwe kwa viwango na thamani ya miradi hiyo iandane na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali na kuisimamia miradi hiyo ikamilike kwa wakati ili iwahudumie wananchi kama yalivyo matarajio yao.
Aidha, Mkuu wa Mkoa Kanali Kido aliwahakikishia wananchi kuwa atatekeleza majukumu yake kwa kufuata kanuni, sheria na miongozo ya uongozi na aliwaomba ushirikiano wananchi na viongozi wote ili kutimiza malengo ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa mstaafu Hajjat Fatma A. Mwassa mara baada ya kukabidhi ofisi katika salaam zake awashukuru viongozi na wananchi wa mkoa wa Kagera kwa ushirikiano na upendo waliompatia wakati akihudumu kama mkuu wa Mkoa wa Kagera.
"Tangu nifike katika mkoa huu mwaka 2023 nilipata ushirikiano wa kutosha, tumefanya mengi mkoa umesonga mbele kimaendeleo katika sekta mbalimbali, kwa miradi mingi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa naamini ikikamilika Kagera itakuwa kama Ulaya." Alihitimisha Hajjat Fatma A. Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mstaafu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa