- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
TRA MKOA WA KAGERA YAFUNGUA DAWATI MAALUM LA UWEZESHAJI WAFANYABIASHARA
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kagera wazindua Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara kwa wafanyabiashara hususani wadogo ili kuendelea kuweka mazingira bora zaidi ya kufanya biashara.
Akizindua na kufungua huduma hiyo Septemba 3, 2025 katika ofisi za mkoa za TRA Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma A. Mwassa aliushukuru uongozi wa TRA kwa kuwa wabunifu na kuanzisha huduma ya kuweka mazingira bora na rafiki ili wafanyabiashara wafanye shughuli zao kwa uhuru zaidi huku wakilipa mapato ya Serikali bila usumbufu wowote.
"TRA ya sasa ni rafiki sana, si kama ya zamani, unakaribishwa, unaelekezwa unakadiriwa kulingana na biashara yako, unapewa muda wakulipa kodogo kidogo kama umelimbikiza kodi lakini pia kama kuna jambo hulielewi unaelimishwa." Alisema Mkuu wa Mkoa Mwassa
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Mwassa aliwakumbusha TRA mkoa wa Kagera kuhakikisha wanawafikia walipa kodi wote ili kukusanya mapato ya Serikali hususani kwa wafugaji ambao wanamiliki ng'ombe wengi katika ranchi za mkoa wa Kagera. Pia aliwataka wafanyabiashara kutumia fursa ya dawati maalum la uwezeshaji biashara kupata ushauri ili kukuza zaidi biashara zao.
Naye Bi Husna Abdul Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamachinga mkoa wa Kagera akiongea katika uzinduzi huo aliushukuru uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kagera kwa kuwa karibu na wafanyabiashara wadogo hususani wamachinga kwa kuwapokea na kuwaelimisha huku wakiwaongoza ili nao wakuze mitaji yao na biashara zao pia.
Aidha, Bw. Castro John Meneja wa Mamlaka ya Mapatoa Tanzania Mkoa wa Kagera alisema huduma ya Dawati la Uwezeshaji Biashara imefunguliwa na kuzinduliwa rasmi katika mkoa wa Kagera lengo kuu likiwa ni kuwatambua, kuwasikiliza na kuwawezesha wafanyabiashara wakiwemo wale wadogo kabisa kukuza biashara zao na kulipa mapato ya Serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.