- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma A. Mwassa azindua rasmi uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu ujulikanao kama Nsekela Stadium uliojengwa na Bw. Abdulmajid Nsekela Mwenyekiti wa taasisi ya Abdulmajid Nsekela Foundation.
Akizindua uwanja hou uliojengwa Wilayani Kyerwa katika eneo la Rwenkorongo Agosti 22, 2025 Mkuu wa Mkoa Mwassa alimpongeza Bw. Abdulmajid Nsekela mzaliwa wa Kyerwa kutekeleza kwa vitendo wito wake wa "Ijuka Omuka" kwa kukumbuka nyumbani na kuwekeza katika mradi mkubwa unaokwenda kuinufaisha jamii ya Wanakagera.
"Uwanja huu nauangalia kwa jicho la tatu wananchi wa Wilaya ya Kyerwa wamepata fursa ya kufanya mazoezi wakiwemo wanafunzi wa shule jirani hapa, pia taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi aidha kupitia mashindano mabalimbali tutaweza kupata burudani hapa badala ya kwenda mbali na Wilaya yetu." Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Mwassa.
Naye Bw. Abdulmajid Nsekela alisema kuwa uwanja huo ameujenga kupitia Taasisi aliyoianzisha mwaka 2024 ya Abdulmajid Nsekela Foundation na ujenzi wa uwanja huo ni lengo mojawapo kati ya malengo nane yaliyomfanya kuianzisha taasisi hiyo.
Akiyataja malengo nane ya taasisi ya Abdulmajid Nsekela Foundation Bw. Nsekela alisema ni Elimu, Ujasiliamali, kuwezesha vijana kiuchumi, Afya ya mama na mtoto, Uongozi, Utawala bora, Ustawi wa jamii na Michezo na burudani. Aidha Bw. Msekela alisema kuwa amenza na michezo kwa kuwa inawaleta watu wengi kwa muda mfupi.
Ujenzi wa uwanja wa Nsekela Stadium ni uwanja wa mpira wa miguu ambao utajumuisha pia viwanja vya mpira wa mikono na kikapu ikiwa ni pamoja na eneo la kukimbilia mashindano ya riadha. Pia kukamilika kwa uwanja huo utajumuisha ujenzi wa majukwaa ya watazamaji na uzio wa ukuta.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.