- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
MWENGE WA UHURU MWAKA 2025 KUPITIA MIRADI YA SHILIONI BILIONI 23.8 KAGERA
Mwenge wa Uhuru leo Septemba 7, 2025 waanza mbio zake Mkoani Kagera tayari kukinbizwa katika Halmashauri nane za Mkoa huo.
Mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela katika Kijiji cha Nyakabango Wilayani Muleba Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma A. Mwassa alisema kuwa Mwenge huo wa Uhuru ukiwa mkoani Kagera utafungua, kuzindua, kuweka Mawe ya Msingi na kufungua miradi ya Maendeleo 58 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 23.8
Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2025 ni "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Mwaka 2025 kwa amani na Utulivu." Aidha, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ni Ndugu Ismail Ali Ussi ambaye atawaongoza wenzake kumkimbiza Mwenge wa Uhuru kwa kilometa 1040 mkoani Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma A. Mwassa katika mapokezi hayo alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera kujitokeza kwa wingi katika maeneo yao kuupokea kuushangilia na kuufurahia Mwenge wa Uhuru katika utakakopita kwani Mwenge wa Uhuru ni kichocheo kikubwa cha kuwaletea wananchi maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.