• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Mkuu wa Mkoa Awaapisha Wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Bukoba Ili Kupunguza Migogoro ya Ardhi Katika Mkoa a Kagera

Posted on: May 5th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu amewaapisha wajumbe wanne wapya wa Baraza la Aardhi na Nyumba la Bukoba na kukamilisha wajumbe sita wanaotakiwa katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ili kuongeza ufanisi katika baraza na kuondoa migogoro ya ardhi mkoani Kagera.

Akiwaapisha ofisini kwake Mkuu wa Mkoa Mei 4, 2017 aliwaasa wajumbe hao kuzingatia miiko ambayo imo katika Kanuni za Mahakama za Migogoro ya Ardhi, Tangazo la Serikali namba 174 ya mwaka 2003 ambazo ni; Moja, Mjumbe wa Baraza awe mtu mwenye kujishimu na heshima yake ionekane kwake na kwa Baraza.

Pili, Aishi na aonekane kuwa ni mtu asiye na upendeleo wa aina yoyote na waadawa (Pande zinazoshitakiana)  wakimuona waondoe shaka kuwa ni mtu mwenye kuweza kupendelea. Tatu, Asishiriki kutoa maamuzi au kusikiliza kesi yoyote inayomhusu yeye binafsi au mtu yeyote katika familia yake. Nne, Ajue mipaka ya kazi yake na kwa namna yoyote asijaribu au kuonyesha umma kuwa yeye anafanya kazi za Mwenyekiti.

Tano, Mjumbe wa Baraza wakati wote awe msiri kuhusiana na kesi ambazo bado kutolewa uamuzi. Harusiwi kusema nje ya Baraza, chochote kinachohusu undani wa kesi ambayo bado haijaamuliwa. Sita, Hairuhusiwi kuwa na urafiki na upande wowote katika kesi inayoendelea kusikilizwa. Saba, Ajiepushe kuzungumza au kufanya mawasiliano yoyote na wadaawa katika eneo la Baraza na kwa hali yoyote haruhusiwi kutoka nje ya jengo la Baraza na kwenda kuzungumza na wadaawa au jamaa zao kabla au baada ya saa za kazi.

Nane, Mjumbe haruhusiwi kuwa wakili wa upande wowote katika kesi, haruhusiwi kutoa ushauri au kuwaandikia wadaawa kitu chochote.Tisa, Awahi na kuhudhuria katika vikao kama itakavyokuwa imepangwa na Mwenyekiti na asikose kuhudhuria mfululizo wa vikao kwa kipindi kinachozidi mwezi mmoja bila sababu ya kuridhisha.

Kumi, Mjumbe asimshawishi Mwenyekiti wa Baraza ili apangiwe kuketi katika kesi fulani. Kumi na Moja, Baada ya kukamilika kesi yoyote, mjumbe atatoa maoni yake kwa maandishi bila kuchelewa. Mwisho Mjumbe asipokee au kuomba zawadi kama hongo au takrima kutoka upande wowote wa waadawa.

Akitoa shukrani Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Bukoba Mheshimiwa Rogate Assey alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa  kuwaapisha wajumbe pia aliwasistiza wajumbe hao walioapishwa kuzingatia miiko na kuzingatia viapo vyao katika kutekeleza majukumu yao.

Mhe.  Assey alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa Mkoa wa Kagera ni mkoa wenye migogoro mingi ya ardhi lakini kutokana na umakini katika utendaji wa Baraza la ardhi na Nyumba la Bukoba umeimarika na kupitia Baraza hilo migogoro mingi ya ardhi imetatuliwa kwa kiwango kikubwa, mlundikano wa Kesi umepunguzwa sana aidha, malalamiko na kero za wananchi kuhusu ardhi zimetatuliwa.

Pia alitoa rai kwa wajumbe kuwa hawaruhusiwi kushawishi kwa njia yoyote isipokuwa watekeleze wajibu wao kulingana na kanuni na taratibu za sheria na kuzingatia miiko waliosomewa na Mkuu wa Mkoa.

Wajumbe walioapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera ni Bw. Nestory Makwaya, Bw. Henry Mutayanga, Bi Fortunata Rutabanzibwa na Bi Leonada Mpanju. Katika Mkoa wa Kagera kuna Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Manne ambayo ni Bukoba, Muleba, Ngara na Karagwe. Aidha Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya Karagwe linahudumia pia Wilaya ya Kyerwa. Wajumbe wa Mabaraza hayo wanachaguliwa na kudumu kwa kipindi cha miaka mitatu na wanaruhusiwa kuteuliwa zaidi ya muhula mmoja.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.